kbm
JF-Expert Member
- Oct 5, 2012
- 5,224
- 1,677
Shughuli gani huweza kumfanya mtu kuwa tajiri
Siku moja niliwahi kumuuliza tajiri mmoja anitajie jambo moja kuu analofikiria ndilo lililomfanya akawa tajiri na kuwa na mafanikio katika maisha yake. Alinijibu kuwa jambo lililomletea maendeleo hayo ni uamuzi wake wa kujibadili akajifanya yeye mwenyewe kuwa chombo cha maendeleo yake.
Nilipomdadisi zaidi alisema; Nilipokuwa nimeajiriwa nilikuwa chombo cha maendeleo ya mwajiri wangu. Nilikuwa nafupishwa uwezo wangu kwa kuelekezwa nifanye kazi na wenzangu na kupangiwa baadhi tu ya kazi nilizotakiwa nifanye.
Kufuatia maelezo ya huyu milionea na utafiti wangu, niligundua kuwa matajiri wote ni watu waliojiajiri wenyewe kwa kufanya shughuli za uzalishaji mali.
Shughuli wanazofanya ni kama vile biashara ya kuuza bidhaa au huduma; kilimo, ufugaji uchimbaji madini na nyingine nyingi.Hata hivyo kabla ya kuamua kuingia kwenye biashara kuna mambo kadhaa unayopaswa kuyafikiria. Kubwa zaidi ni kujichunguza hali yako wewe mwenyewe kama kweli unaweza kubadilika ukawa chombo cha maendeleo yako binafsi.
Baadhi ya maswali yanaweza kuwa kama vile; Hali ya maendeleo yako ya sasa ikoje? Je, shughuli unayofanya sasa inakuendeleza kiasi gani? Kwa kutazama uzito wa kazi unayofanya sasa unafikiri unaweza kuongeza kazi zaidi kiasi? Je, unaridhika kwa kila hali na kazi yako ya sasa?
Je, utaendelea kuridhika na hali hii hata baada ya miaka 5 au 10 kutoka leo? Kama hauridhiki na unataka kuwa tajiri amua kuanza kujiajiri mwenyewe. Fanya uamuzi leo usingoje kesho kwa sababu wakati mwingine kesho huwa haiji.
Mambo ya kuzingatia katika harakati za utajiri
(a) Chunguza uwezo wako
Pamoja na kuwepo kanuni na mambo mengi ya kuzingatia katika harakati za kutafuta utajiri, cha kwanza kabisa ni wewe mwenyewe. Jiulize kama kweli umedhamiria kwa dhati kuanza safari ya kuelekea kwenye kutafuta utajiri, hasa kujiari kwa kufanya biashara. Jiulize unahitaji nini ili uweze kujiajiri.
(b) Jizatiti na hamasisha
Kuchangamana na watu na kuwatia moyo watu watu ni moja katika masharti makuu ya biashara. Mfanyabiashara huwa mcheshi na mwenye tabasamu wakati wote. Atawajibika kuwatia moyo watu watakaokuwa wadau wake, mathalani wamiliki na watendaji wa mabenki na kampuni ya bishara watakuwa muhimu sana kwake iwapo atahitaji mkopo kuanzisha biashara. Kujishaijisha mwenyewe au kujitia moyo ni jambo la muhimu kwa sababu litamsaidia kujiamini kujituma na kujizatiti.
(c)Fikiria kabla ya kutenda
Wakati ukifikiria kuingia katika biashara chunguza nyanja zote zinazohusika na ufanisi katika biashara. Pengine huenda isiwe vyema kuacha ghafla shughuli unayofanya. Kuna waajiriwa walioanza biashara huku wakiendelea na kazi zao. Mishahara marupurupu imewasaidia kuimarisha mitaji ya biashara zao.
Wakati mwingine kuamua kuacha kazi na kuingia katika biashara huweza kikawa kitendo chenye kiwango fulani cha mashaka, lakini vile vile kuacha kujiuzulu na kuendelea na kazi ya kuajiriwa huweza kuwa uamuzi wa mashaka zaidi, hasa kwa mtu mwenye ari ya kuwa tajiri.
Kuongojea hadi kustaafu ni uamuzi dhaifu kwa sababu harakati za kutafuta mali zinahitaji nguvu na akili za ujana zaidi kuliko hata kazi ya kuajiriwa.
(d)Kuamua biashara unayoweza kufanya
Watu wengi huanzisha biashara ambazo baada ya muda mfupi tu hofa na pengine wakati zikiwa bado changa. Jambo hili ni la hatari sana hasa kwa wajasiriamali wapya. Pamoja na changamoto mbalimbali zinazoweza kuathiri biashara, mara nyingi tukio hili hutokana na uchaguzi wa biashara usio sahihi.
Wanasaikolojia wamebuni utaratibu unaomwezesha mtu anayeamua kuingia katika biashara kwa mara ya kwanza.
Kwanza andaa orodha ya aina ya biashara ambazo ungependelea kuanzisha. Kisha andaa orodha nyingine ya aina za biashara ambazo unafikiria unaweza kuzimudu kuziendesha vizuri. Baadaye andaa orodha ya tatu ya biashara ambazo zina mvuto na soko kwa jamii ya mahali unakotaka kuanzisha biashara. kwa kuchunguza kwa makini orodha hizi tatu utaweza kufanya uamuzi sahihi na biashara itakayofaa kuanzishwa. Kwa mfano aina ya bia=shara itakayokuwa imetokea katika orodha zote tatu.
Chanzo: MCL