Hapa tu bongo kumuona Rais Samia ni shughuli pevu, mpaka ukaribie karibu na jukwa alipo kuna vizuizi vingi vya ukaguzi mpaka inakuwa kero na udhalilishaji mtu mzima na akili zako unakaguliwa mwili mzima na maaskari/walinzi. Jukwaa lenyewe aliko Rais nalo limetengwa mbali yuko yeye na watu wake wa karibu tu. TV kubwa zimewekwa uwanjani wananchi wamuone huko. Tofauti na zamani Rais tuliweza kumuona kwa karibu na hata kumshika mkono kumsalimia tu, siku hizi hata kumuona kwenye gari lake barabarani kunako msafara wake hatumuoni akipungia mkono wananchi waliojipanga barabarani walau awapungie mkono tu. Kwanza haijulikani yupo gari gani na magari yote matatu yanafanana na yana nembo yake, meusi tii mpaka vioo na vimefungwa