Wapenzi wa michezo ya video wanaendelea kujiuliza kama ni bora kununua PlayStation 5 sasa au kusubiri PlayStation 6 ili kucheza GTA 6.
Kwa mujibu wa taarifa rasmi kutoka Rockstar Games, mchezo wa Grand Theft Auto VI (GTA 6) unatarajiwa kutolewa tarehe 19 Novemba 2026 kwa PlayStation 5 na Xbox Series X|S.
Rockstar Games .
Wataalamu wengi wa michezo wanaamini kuwa kama lengo lako kuu ni kucheza GTA 6, basi kununua PS5 sasa kunaweza kuwa chaguo bora zaidi.
Hii ni kwa sababu GTA 6 imetengenezwa mahsusi kwa kizazi cha PS5, na kusubiri PS6 kunaweza kumaanisha kukosa kushiriki moja ya uzinduzi mkubwa zaidi katika historia ya michezo ya video.
Aidha, GTA 6 tayari imeonyesha kiwango kikubwa cha hamasa duniani, huku wachambuzi wakiripoti kuwa imevunja rekodi za awali za oda za mapema (pre-orders) katika sekta ya michezo ya video.
Hata hivyo, kwa wale ambao hawana haraka ya kucheza GTA 6 na wanapendelea kusubiri teknolojia mpya zaidi, PS6 inaweza kuwa na uwezo mkubwa zaidi wa picha, utendaji na teknolojia za kisasa. Lakini hadi sasa Sony haijatangaza rasmi tarehe.