Je Uovu wetu unamgusa Mungu?

Je Uovu wetu unamgusa Mungu?

Shayu

Platinum Member
Joined
May 24, 2011
Posts
608
Reaction score
1,655
Kitu kimoja ambacho nimejifunza katika maisha, huwezi ku control matendo ya watu wengine. Unaweza ku control matendo yako pekee, ambayo uko responsible nayo.

Na maisha yetu yanategemea maamuzi na matendo yetu. Hiki ndicho ninacho kijua, mwisho wetu unategemea matendo yetu. Kama tutaelekeza mawazo yetu na matendo yetu katika mambo yenye tija. Tija itafuatia.

Mwisho wangu utakuwaje kama nitatenda uovu? Wanasema utavuna ulichopanda huu usemi una ukweli ndani yake.
Akili zetu na mioyo yetu ni shamba ambalo mbegu za mawazo hupandwa na kukua katika ukamilifu wake. Mawazo mabaya huzaa matendo mabaya.

Kwasababu kabla ya kutenda uovu binadamu hufikiria kwanza kisha hutenda. Wanasema fikiri mawazo yaliyo mema kila wakati ili upande mbegu njema ndani yako.


Unaweza kumshauri mtu kuhusu mambo kadhaa, Ni uamuzi wake kutenda au kutokutenda.

Hilo liko mbali na uwezo wa mshauri juu ya mabadiliko ya tabia ya mtu.

Ninaweza kukushauri leo uwe mtu mwema lakini sina ubavu wa kukulazimisha kutenda mema. Una haki ya kuchagua njia ambayo unafikiria ni bora kwako.


Lakini kila matendo ambayo tuna tenda binadamu yana mwisho wake uwe mbaya au mzuri. Kila uamuzi tunaofanya unatupeleka mbele au kuturudisha nyuma.


Lakini kwa mtu mwenye busara uchagua njia ambayo itampelekea kufika sehemu salama na yenye amani. Ambayo ni kutenda yaliyo sahihi. Mtu ambaye amepevuka kiakili huetenda yaliyo sahihi.


Kila siku tunawajibu wa kutafakari ili tukue kiakili. Tusitende bila kutafakari. Kwasababu matendo mengi yale tunayotenda na kujikuta tumeingia kwenye matatizo ni yale tuliyotenda bila kutafakari kwa kina.

Mungu anaposema kwenye biblia kwamba ni lazima tuchague njia tupaswayo kupita na kutupa uhuru wa kuchagua, hakudanganya. Njia ya uovu ambayo hupelekea kwenye maangamizi au njia ya haki ambayo huleta amani , maisha na ustawi. Tunapochagua uovu, tunachagua maangamizi.

Sheria zote ambazo Mungu amewapa binadamu ni kwa faida yetu. Mungu haguswi na uovu wetu. Matendo yetu yakiwa maovu haya mdhuru yeye ila ni sisi wenyewe. Sheria za Mungu ni kwaajili yetu ni kwaajili ya amani yetu na tukizivunja ni sisi tutakaoumia. Ni sisi tutakaoumizana.


Unapokuwa sio muaminifu unafanya binadamu mwenzako asimuamini binadamu mwingine na watu kujaa kutokuaminiana ni nani ina mdhuru? sisi au Mungu?


Unapoiba, unapozini, unapoua na matendo mengine yote hayamdhuru Mungu bali sisi wenyewe. Dunia hii iliundwa in a very good order ni sisi tunaoibomoa. Unapotoka nje ya ndoa unafanya familia yako isiwe stable ni nani anadhurika ni
Mungu au wanadamu. Na tunajua watoto wasiolelewa vyema ni disaster kwa jamii yeyote.

Kwahiyo tunatakiwa kuangalia tabia zetu kwa ukaribu sana. Tabia zetu ndizo zinazotufanya tuwe karibu na Mungu. Na sio kitu kingine chochote. Tunaweza kusema tuko tunampenda Mungu kwa maneno yetu lakini matendo yetu yakawa mbali.

'' Watu wangu wananiheshimu kwa midomo yao lakini mioyo yao iko mbali na mimi '' Anasema Mungu katika kitabu cha Mathayo 15:8. Anaendelea;

'' Wananiabudu sio katika ukamilifu , mafundisho yao ni mafundisho ya kibinadamu''
Kwahiyo kitu ambacho kina mjulisha mtu wa Mungu ni matendo sio maneno.
Kitu kimoja ninachokijua na kukiamini watu wanaweza kubadilika na kuacha njia zao na kuja karibu na Mungu. Watu wanaweza kubadili akili zao. Na kuamua kumfuata Mungu. Kwasababu anapatikana. Na kuacha mabaya na kutenda katika usahihi.
'' Ikiwa watu wangu walioitwa kwa jina langu (katika haki yake), ili wawe watenda haki. Watajinyenyekesha, na kuomba, na kunitafuta uso wangu,na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia kutoka mbinguni, na kuwasamehe dhambi zao, na kuiponya nchi yao. Macho yangu yatafumbuka na masikio yangu yatasikia maombi ya watu hao''
2 mambo ya nyakati 7 :14 -15.

Ni wakati sasa wa kubadilisha njia zetu ili familia zetu, jamii zetu na taifa letu liponywe.

Mimi kama mtu ambaye nimejitolea maisha yangu katika kusoma na kutafakari siwezi kupinga uwepo wa Mungu na umuhimu wa njia zetu kuwa bora kwa mustakabali wetu wenyewe. Ili mwisho wetu kama binadamu uwe mwema na sio mbaya. Ushahidi wa uwepo wa Mungu umetuzunguka kila mahali. Na utegemezi wetu wa kwa kwa nature ni ushahidi tosha.

Mbuzi hawafanyi kazi majani yanaota yenyewe kwaajili yao. Wanayala wana nawili na kustawi, tunapata kitoweo na maziwa.


Tumepata mbegu kwaajili ya mazao yetu ni nani aliyeziumba? Kwa vizazi vingi toka karne na karne watu wanakula mahindi na mchele ni nani aliyeviumba vyote? Tunajua bila mazao yanayozalishwa na ardhi hii hatuwezi kuishi.


Ni nani adondoshaye mvua na kufanya majani yakue na yastawi kwaajili mifugo yetu na wanyama wa mwituni? Sio yeye alishaye simba na chui? Bila ya majani hakuna swala chakula cha simba na chui. Jua hili ni Mungu atukuzaye.


Kitu kimoja ambacho tunapaswa kujifunza ni kumtegemea Mungu katika kila kitu na kuweka tumaini letu kwake. Na hiyo ni njia ya mtu mwenye busara.

Na Plato anasema in phaedo; Ni vizuri kujinyenyekesha kwa mtu mkubwa na mwenye uelewa upana zaidi yako. Anasema sisi ni mali ya Mungu na Mungu ni mwenye uelewa mpana zaidi yetu hatuna budi kujishusha na kumfuata yule mwenye maarifa na akili zaidi yetu.
 
Back
Top Bottom