Je, upi ni msingi wa falsafa ya Freemason?

Je, upi ni msingi wa falsafa ya Freemason?

Undava King

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2017
Posts
3,422
Reaction score
5,659
Tunaanzia katika jamii za Wachaldeans na Wamisri ambao waliamini kuwa hapo kabla Mungu aliumba MWANGA (ikiwakilisha dunia ya malaika).

Nje ya ule mwanga wakaumbwa daraja la viumbe wasioonekana ambao wengine huwaita NYOTA, na nje ya zile nyota zikaundwa elementi nne na ndani ya elementi hizo (maji,hewa,fire na udongo) dunia inayoonekana ikaundwa.

Hivyo basi yote kwa yote baada ya kutimia kwa maumbile hayo, kila kinachoonekana au elementi huwa ndani ya Nyota zisizoonekana au elementi za kiroho, wakati Nyota ni kinyume chake katika miili yao wao ukaa ndani ya malaika na malaika ndani ya nyota; na malaika huwa ndani ya Mungu na Mungu ndani ya vyote.

Hivyo basi vyote ni Umungu katika Mungu, Umalaika katika Malaika na Umwili katika dunia ya mwili na kinyume chake kama vile mbegu ya mmea ufumbatwa, hata dunia pia ufumbatwa na Mungu.

Kulingana na alichokinena CHiram Abiff (Master Buider)

"Endapo KIKUNDI (mob) kikiongoza, basi binadamu atatawaliwa na UJINGA;

Endapo ni KANISA likiongoza, basi binadamu atatawaliwa na USHIRIKINA;

Endapo ni SERIKALI ikiongoza, basi binadamu atatawaliwa na HOFU."

Kabla binadamu ajafikiria kuishi kwa amani na maelewano, UJINGA lazima ubadilishwe katika HEKIMA.

USHIRIKINA lazima ubadilishwe kuwa katika IMANI YENYE MWANGAZA.

HOFU lazima ibadilishwe katika UPENDO.

Pamoja na kuwa kauli hizi uonekana kuenenda kinyume,
MANSONRY ni dini inayotafuta uwezekano wa kumuunganisha Mungu na Binadamu kupitia kuinua daraja la ufahamu wa utambuzi kwa namna ambayo italeta taswira ya mtazamo wenye maono yaliyokwisha kufafanua vyema kazi ya "the Great Architect of the Universe"

Ambapo katika vyote; utakatifu na elimu dunia kuhusiana na fumbo la maisha vitaruhusiwa kufundishwa (pasipo vikwazo/kificho) kwa wote watakaokubali kuenenda na filosofia hii ya maisha.

Katika hili IMANI na MAFUNDISHO YA DINI hayatokuwa na nafasi tena; mambo yasiyo na uhalisia yataondolewa na kiini tu ndicho kitakachotunzwa.

Dunia itaongozwa na mwangaza wa fikra pevu zaidi ambapo kila fikra itajitwalia nafasi nzuri zaidi inayoifaa.

Chuo kikuu kitagawanywa kwa alama(grades), admission ambazo zitakuwa zikipimwa kupitia daraja la ufahamu lililofikiwa na mlengwa (pstominary tests au unyago(initiations))

Hapa binadamu ataelekezwa katika Utakatifu mkuu(most sacred), Siri kuu (the most secret), na fumbo kuu zaidi ya yote (the most enduring of all mysteries)- SYMBOLISM (lugha ya Alama)

Hapa unyago utafundishwa kwamba kila kinachoonekana, kila chakufikirika, kila mwemko wa kihisia siyo kingine bali ni Alama ya kanuni ya umilele.

Hapa binadamu atajifunza kuwa CHiram (ukweli) uongo wake umefukiwa au kuzikwa katika kila atom ya kosmos; ya kwamba kila muundo ni alama na kila alama ni kaburi la ukweli wa milele.

Kupitia elimu- kiroho, kimwili, kimaadili na kifizikia..binadamu atajifunza kutambua ukweli wa kuishi na kuondokana na ile hali ya kutojiweza wenyewe.

Muongozo wa kidunia utafata huo muundo itapotokea mwongozo huu wa kiungu utasimikwa kufanya kazi yake kupitia namna ambavyo ulimwengu uongozwa. Katika siku hiyo ambayo agizo kamili (perfect order) litasimikwa, pamoja na amani ya ulimwengu na kwa ushindi mkubwa, binadamu atoangaika tena kutafuta furaha yake, kwa kuwa wataipata, kuwa iko ikiwaelemea ndani yao.

Matumaini yaliyokufa, matarajio yaliyokufa, malengo yaliyokufa yote yatafufuliwa kutoka katika makaburi yao na roho nzuri na uzuri ambao umekuwa ukichinjiliwa mbali na ujinga wa binadamu utakuwa tena kwa mara nyingine Master of work.

Itapotokea hivyo sages wataketi katika viti vya Bwana na miungu wataongozana na binadamu.

Itaendelea..."
 
SEHEMU II: Filosofia ya Masonia

Alama ya Fimbo iliyomjeruhi Nyoka wa 'Hermes'(ufahamu)- Siku zote tokea kale imebaki kuwa ishara ya utabibu duniani.

Miongoni mwa kila jamii ya kale zaidi Nyoka alikubalika kama alama ya Hekima au Wokovu.

Chuki juu yake iliyobebwa na Wakristo inatokana na uelewa mfinyu juu ya kuelewa mafumbo ya nini kilimaanishwa katika simulizi ya bustani ya Edeni.

Nyoka (Serpent) ni mkweli katika kanuni za Hekima, kwa kuwa alimjaribu mwanadamu ili kumfanya haweze kujifahamu mwenyewe.

Hivyo basi ujuzi wa Nafsi (baada ya kujitambua) kulipelekea binadamu kutoku-mtii Demiurgus, Jehovah.

Je Nyoka ilikuwaje mpaka akawepo katika bustani ya Mungu?

Wakati Mungu mwenyewe alithibitisha kuwa kila alichokiumba katika siku ya sita ya uumbaji kilikuwa kizuri. Jambo hili halijawahi pata majibu ya kuridhisha na watafsiri wa maandiko.

Mti ambao ulimea katikati ya bustani ni symbolism ya uti wa mgongo (spinal fire); Na ujuzi au maarifa ya kuutumia uti wa mgongo au spinal fire ndiyo zawadi aliyopewa mwanadamu na the great serpent.

Hata hivyo kauli hii yaenda kinyume na kile tulichokidhania katika kile tunachokijua katika maandiko.

Kwani Nyoka ni alama na mfano wa wokovu wa ulimwengu, ambaye hukomboa dunia kwa kumpa muumbaji (binadamu) ujuzi wakujitambua na kutofautisha kati ya jema na baya.

Kama sivyo; wadhani kwanini Musa alinyanyua fimbo ya Nyoka wa shaba katika msalaba jangwani ili kwamba kila atakaye itazama apate kupona, ile sumu waliyong'atwa na nyoka wenye sumu kali ipate kuwatoka.

Je, uoni kwamba Nyoka huyu wa shaba msalabani ni unabii wa mtu atayekuja kusulubiwa hapo baadae?

Ikiwa kama Nyoka ni kiumbe kiovu, kwanini Yesu aliwaelekeza wanafunzi wake kuwa na busara kama za Nyoka?

Hivyo basi kwa msingi huo ile nadharia inayoshikilia kuwa Nyoka ni muovu haiwezi kuthibitishwa.

Nyoka kwa kipindi kirefu amebakia kuwa ishara ya umilele(immortality).

Ni alama ya reincarnation au metempsychosis, kwa sababu kila mwaka Nyoka ujivua magamba, ujirudi kama alivyokuwa katika mwili mpya.

Kuna ushirikina wa kale ukilihusisha tendo hili na kutokufa kwa Nyoka milele endapo hatopata jeraha la aina yeyote uishi milele.

Nyoka na mkia wake ukiwa mdomoni ni ishara ya eternity (umilele wa) kiroho na dunia yetu, kifizikia.

Nyoka mwenye vichwa saba, uwakilisha supreme deity (miungu mkuu) na ujidhihirisha kupitia Elohim (mungu muumba) au roho saba, ambazo kwa msaada wake aliweza kusimika ulimwengu wake.
 
SEHEMU YA III: Ufafanuzi wa siri kuu nyuma ya alama za Kimasonia.

Angalizo: Tafadhali hakikisha kuwa umeitizama kwanza picha niliyobandika katika uzi huu hapo chini[emoji116][emoji116][emoji116] kwa umakini mkubwa na kubaini kila alama iliyochorwa ndani ya mchoro huo, hili uweze kuelewa na kupata tafsiri ya ninachokwenda kukizungumzia bila ya hivyo utoelewa kabisa naongelea nini.

TUANZIE HAPA: "Kuzungumza na bubu ni kwa njia ya ishara ila kumwelewesha kipofu juu ya asivyoviona kwahitaji maarifa, kwa maana uwezi kuutwika mzigo wa hekima kichwani mwa mpumbavu, vivyo hivyo huwezi kumfukuza ujinga pasipo kumpinga."

Na tuuchambue mchoro huu kwa lugha ya kibinadamu hili wanadamu watuelewe kwa kuwa huu ni wakati wa aquarius "I know"

Mchoro huu kwa chini kabisa (angalia katikati ya mchoro) kuna alama mbili Jeneza na Mti
A) Jeneza-ni ishara ya KIFO
B) Mti- Ishara ya UZIMA

Kwa pamoja ni mwanzo wa Nadharia ya kifilosofia/masonia juu ya "UZIMA WA MILELE" na sayansi ya siri ya kiroho.

C) Ishara ya Tufe mbili juu ya nguzo ndefu (kushoto na kulia)

"..Hapo mwanzo tuliziumba dunia katika mbingu nazo dunia zilikuwa mbili katika umoja, nazo dunia zilikamilishwa katika ukamilifu wake.

Dunia iliyoonekana iliangaziwa na mwangaza wa jua na ile isiyoonekana (hivi sasa) iliangaziwa na mwangaza wa mwezi na nyota zake.

Kwa kuwa tulipoziumba hatukuzitenganisha na hata tulipolala hatukuziendea katika usaulifu wetu.

Hivyo yampasa mjenzi kuziendea zana zake, kupima upya na kuhakiki jengo lake, wapi pana nyufa na wapi palipokumbwa na dhoruba na arekebishe ili haweze kujitwalia pahali katika jengo alilolijenga."

D) Nguzo Kuu mbili ndefu zilizoisimika misingi ya dunia na kuibeba (Jachin na Boaz)
-Uwakilisha nguvu ya kiume (dunia ya kifizikia) na nguvu ya kike (dunia isiyoonekana kifizikia)

E) Nguzo ya Kushoto (Jachin)
-Masculine force ndiyo nguvu dorminant katika dunia ya kifizikia na viumbe wake.

Upande huu ukianzia chini kabisa katika ujenzi wa hekalu letu utaona alama ya NYUNDO na RULA kumaanisha mwanzo wa kutindua/kugongelea, kunyoosha na kupima kwa usahihi foundation ya jengo (tokea kuzaliwa- ishara ya mti)

MUNDU- Kung'oa au kukata, kuvuna na kukusanya mavuno
lengwa. (Kujitwalia waamini)

NANGA- Kujinasisha na kushindwa kujinasua lakini pia kuwa na uthabiti katika ulichoaminishwa kiasi cha kutoyumbishwa na mawimbi ya dhoruba yeyote.

BOX 3 KUUNDA PEMBE TATU 1- boksi ni lugha ya picha kumaanisha dimensions 3 za ufahamu kuanza kujengewa kumwandaa mwamini kuelekea katika kuunda UTATU.

KIUMBE KISICHOELEWEKA/KUELEZEKA CHENYE MBWAWA MBILI- umaanisha utatu katika tumaini kuu juu ya viumbe vya Kiroho (Kivyovyote vile utakavyokiita iwe ni Mungu au Malaika)

SAFINA YA NOAH NA ALAMA YA UPINDE WA MVUA- agano la uzazi la ki-umilele kati ya binadamu na viumbe roho.(Mtazishika sheria hizi na kuzirithisha kizazi hata kizazi kinyume na hapo mtaangamia)

NGAZI YENYE STEPU TATU- Kwa kanuni ya utatu ufahamu ukweao uendelea kupanda hata hatua ya juu zaidi(3) ya kidunia (Ishara ya TUFE lenye mfanano na sayari)

KIMONDO AU NYOTA IPANDAYO KUELEKEA JUU LILIPO JUA (fallen angel, nyota ya asubuhi, bright star, sophia n.k)-ishara ya kunyanyuliwa kwa ufahamu huu ambao ulishuka/kudondoka kurejea mahali pake katika ufahamu wenye mwangaza.

F) Nguzo ya Kulia (Boaz)- Feminine force ndiyo nguvu inayotawala ulimwengu huu usiyoonekana kifizikia.

Kama tulivyokwisha kutangulia kuona katika kipengele kilichopita, hapa napo tuanze kupachambua tukianzia chini kabisa upande wa kulia wa nguzo kuu ya hekalu.

NYUNDO NA SEPETU- zana za ujenzi zitumiwazo na wajenzi (hawa wamekwisha kuandaliwa au uzaliwa kuwa mafundi)-hivyo popote pale utakapoona ishara au michoro hiyo regardless ya tumeweka kifaa gani na tumekitafsiri kwa maana gani, jua tupo kazini kuandaa kizazi kipya.i.e jembe na nyundo.

RULA ILIYOKUNJWA NA MCHORO WA MITHILI YA MTU ALIYEKAA- umaanisha MEDITATION

MAKERUBI (Me&Ke) au Mabawa mawili-ishara ya muunganiko pacha wa nguvu mbili za kimamlaka yaani YING&YANG kupata mjumuisho mmoja wa maarifa yenye nguvu isiyokinzana i.e bibi na bwana kwenye nembo ya...,american seal, UK seal, taji la maua mithili ya bawa kwenye nembo za jeshi, BOT n.k

KOMBE LINALOFUSHA MVUKE WA MOTO- ishara ya uvuvio wa moto wa kiuungu/kiroho-nguvu ya kuweza kuharibu endapo isipokuwa under control (Kundalini fire) i.e ishara ya mwenge, dragon kule china n.k

KONDOO- Ishara ya kubatizwa kwa roho wa moto wa mwanakondoo (kristo)

KIATU- Mwanzo wa safari ya kiroho na kupiga hatua za kiroho kuelekea katika utimilifu.

KOFIA 1 yenye nyota 5 na meza 1 jumla yake 7-ishara ya tunzo ya ukamilifu na ukomavu katika kuanza ujenzi.

ALAMA YA KITABU NA MDUARA WENYE DOTI KATIKATI-Ishara ya utambuzi mizania katika nguvu pacha kinzani za ying&yang pamoja na black&white witch.

KIZIBAO- ishara ya utumishi au ushirika.

TUFE LA DUARA JUU KABISA YA NGUZO ni ishara ya umbile la dunia ya pili.
Zodiaki na nyota zinazoonekana ndani ya tufe hili ndiyo makazi na mabara au mataifa ya viumbe hawa waishio katika dunia isiyoonekana kifizikia.

MWEZI WENYE SURA YA BINADAMU NA NYOTA- umaanisha nguvu ya ufahamu (KE) yaani nguvu ya uponyaji (healing) wenye kuangaza katika kiza cha dunia isiyoonekana.

G) Kapeti au Zulia la draft; chini sakafuni katikati ya nguzo kuu mbili za jachin na boaz- Ishara ya kusakafia hekalu letu kwa ulinganifu sahihi wa black and white magic au mema na mabaya n.k

H: Mishumaa mitatu ni utatu wa jachin, boaz na moto
Mshumaa wa kati kati ni mrefu zaidi kuashiria-nguvu kuu ya moto (Kundalini)

I: Box- ni sanduku la agano ilipoifadhiwa mikataba ya mapatano

J. Msahafu& alama ya bikari na rula(meditation)- kwa pamoja huo ndiyo mwongozo au katiba itakayofuatwa katika kufikia lengo kwa upande wowote ule utakaojumuishwa katika hili iwe ni kuamini mwongozo wa misahafu au meditation jambo ni lile lile.

K. Matofali Mawili yanayoelekea katika mshumaa wa katikati ni ishara ya nguvu mbili za ying&yang kuungana kuamsha kundalini.

L) Kijiko cha ujenzi(kulia)-ishara ya kuendelea kujijenga katika ufahamu na kujitambua

M)Mikono iliyoshikamana kwa ishara ya kusalimiana- ni kula kiapo cha kuwa wamoja au brotherhood

O) Visu viwili virefu vyenye makali pande zote- (cha kushoto)-kupambana pasipo kuhofia chochote au kujibainisha moja kwa moja (cha kulia)-kilichokita katika katiba au msahafu akitoonekana bayana katika utekelezaji wake kwa jicho la nje.

P) Alama ya Kopa- ishara ya silaha kuu itakayotumiwa katika vita au mapambano haya ya kuunganisha nguvu hizi mbili ambayo ni UPENDO

Q) Msahafu (Kushoto)-imani za kidini kifizikia, msahafu na bikari(kulia) ishara ya meditation.

R) G- gnosticism doctrine- dhihirisho la ulimwengu wenye mapungufu na suluhisho la kurudia u-mwanzo

S) Nyota-spiritual awakening and self actualization (Kujitambua)

T)Jicho (the watcher) -above all,no limits and the know all a.k.a mtazamaji huyu ndiye mlengwa wa yote haya na kumfikia umaanisha kufanikiwa kwa project yetu. But as below as above ukipindua jedwali juu chini then utabaini kuwa UZIMA NA MAUTI (jeneza + mti=Jicho linaloona muda wote) vitakuwa vimeungana na ile filosofia ya UMILELE itakuwa imefanikishwa.

NB: Usisahau pia kuwa kwa kanuni hiyohiyo ya "kwa jinsi ilivyo juu na chini pia ni hivyo hivyo" wale walio upande wa kulia yaani Boaz wakitaka kufikia Jachin kwa maana ya kujiimarisha itawabidi kupitia daraja la hekaluni kwa kutumia zana za kazi zilizo katika mkono wa kushoto ndani ya nguzo kuu au temple na viseversa.

Namaanisha nini kusema hivi? Ukweli ni kuwa walioko mwangani ndiyo walioko gizani na walioko gizani ndiyo walioko mwangani.

Hivyo basi wakifizikia hili uone vyema vilivyomo ndani ya nyumba wakati wewe huko exposed kwa nje katika mwanga wa jua, yakupasa kuingia ndani ya nyumba yako kuona vyema kupitia dirishani kinachoendelea nje ya mazingira yako na viseversa ni sawa pia kwa upande wa pili kwa walioko gizani na ushuhudia kwa usahihi lakini hawawezi kuvibadili vinavyoendelea mwangani.

Kinachowakwamisha wawili hawa katika umoja na kutofikia malengo ni kukinzana kwao kwa kushindwa kutambua kuwa wa wamoja na hakuna anayeweza bila mwenzake na huo ndiyo mwanzo wa msingi wa kuuelewa umasonia katika step ya kwanza.

Tukutane katika sehemu nyingine panapo majaliwa....."







Screenshot_20230712-083742~3.jpg
Screenshot_20230712-083742~3.jpg
 
Endelea mkuu nakusoma vizuri sana swali langu je Mungu ni jua ? Kwa sababu ndilo liangazalo sehemu zote naomba nijibu plz
 
Endelea mkuu nakusoma vizuri sana swali langu je Mungu ni jua ? Kwa sababu ndilo liangazalo sehemu zote naomba nijibu plz
"Na hili ndilo fumbo la imani..." naamini ni juu yako kurudia mara kwa mara kusoma uzi huu kwa umakini kung'amua hilo kulingana na kile ninachokielezea hapa kwa mifano na picha, na nitaendelea kuleta makala ya elimu hii mpaka utakapombaini Mungu halisi anayetambuliwa na jamii ya masonia ya kuwa ni nani.
FB_IMG_16897439536452312.jpg
 
"Na hili ndilo fumbo la imani..." naamini ni juu yako kurudia mara kwa mara kusoma uzi huu kwa umakini kung'amua hilo kulingana na kile ninachokielezea hapa kwa mifano na picha, na nitaendelea kuleta makala ya elimu hii mpaka utakapombaini Mungu halisi anayetambuliwa na jamii ya masonia ya kuwa ni nani.View attachment 2694410
Shusha vitu
 
THE ORIGIN OF FREEMASONRY.

CHIMBUKO LA FREEMASONRY

NJAMA ZA BWANA LUSIFERI.

Kwenye somo hili juu ya chimbuko la Freemasonry nimependa niongezee kionjo hiki kukuwekea uelewa wako sawa.

Kuna aina mbili za UASHI au MASONRY

1. FREEMASONRY - WAASHI HURU

2.SHRINERDOM - USHRINER

FREEMASONRY au WAASHI HURU - Ni U-Freemason wa kikristo .. katika Nyumba za ibada yaani Lodges utaona kuna Biblia yaani Holy Bible ikijumuishwa kama miongoni mwa zana muhimu za kazi za Mjenzi ambazo zipo tatu (Dira, Mraba na Biblia Takatifu) na katika ibada zao za kuanzishwa yaani Initiation Ritual Biblia na baadhi ya maneno hutumika kama Symbol au alama kwenye Kiapo kuelezea maadili na Sio Imani au Dini yoyote kwa mujibu wao.

Huu ni U-Freemason wa Kikristo.

Freemason ilikuwepo kabla ya Ukristo. Swali je, Kabla ya Biblia Freemason wa kale walitumia nini?

U-Freemason wa Kikristo ulianzishwa na wazungu ni U-Freemason wa Kizungu watu weupe na ndio Freemasonry ya kisasa (Modern Freemasonry). Na ndio Freemason Kuu yaani Main stream Freemasonry... ndiyo inayo julikana leo kama Freemasonry.

Baadhi ya watu wanasema Freemadonry ni aina ya Ukristo... lakini ujue tu kuwa Freemasonry Waashi huru ni Ufreemason wa kikristo.

SHRINERDOM - USHRINER

inayo julikana kama ANCIENT ARABIC ORDER AND NOBLE OF THE MYSTIC SHRINE

Huu ni Ufreemason wa kiislamu. Baadhi ya watu wanasema ni aina ya Uislamu.

Hii ni aina ya Freemason ya Kiislamu. Ya waarabu ndio maana kwenye jina lao kuna neno "ARABIC".

Ni aina ya Freemason ya kizungu pia ndio maana WAARABU humo ndani kwenye Lodge zao utaikuta QUR'AN yenye nembo yao.

MUUNGANIKO

Kabla ya Ukristo na Uislamu kulikuwepo na Freemason kabla ya Ukristo na uislamu kabla ya Biblia.

Ukristo na Uislamu uliingizwa na kuhusishwa ndani ya Freemasonry na Wazungu ili kuunda aina yao mpya kutawala wenyeji.

Aina hiyo ya Freemason ndio wale walio chini ya Makao makuu ya Dunia ya Freemasonry yaani UNITED GRAND LODGE OF ENGLAND.
U.G.L.E

Freemason ya Dar Es Salaamau Kanda ya Africa Mashariki iliyopo Posta na Kule KENYA SERENA HOTEL barabara ya nyerere inayojulikana kama DISTRICT GRAND LODGE OF EAST AFRICA - D.G.L.E.A

Ni Freemason ya Wazungu ..hata kama wanachama wake ni waKenya au waTanzania weusi lakini wapo chini ya CHAPA au HATI ya KIZUNGU yaani F & AM na wanaongozwa na Katiba ya chama ya UINGEREZA.

Hizi ndizo Freemasonry zilizopo na ndio Freemasonry Halali. Legal Freemasonry.

Ufreemason wa Kiislamu Hii Tanzania Haipo.

Ipo Kule ghana na kuna Bwana maarufa anaitwa Ibrahim kuna U-SHRINER huko Ghana.

[emoji117]SASA kuna aina zingine za Freemasonry. Ambazo zimepinga na kukataa Utaratibu wa Uingereza na Katiba yao .. maana katiba yao ni Bandia iliandikwa na ALBERTUS MAGNUS kwa kukopi baadhi ya mambo kutoka kwenye katiba asilia ya awali ya kale aliyo ipata Misri.

Kuna hayo makundi yalikataa kujisalimisha kwa Wazungu waingereza. Maana waingereza waliunda Freemason ya kinamna ambapo utaratibu wake unanyang'anya mamlaka na nguvu za wanachama inatengeneza aina fulani ya Utumwa na haitoi Ukweli kwa asilimia 100. Hukuti mtu mweusi anafanikiwa kupewa Digrii ya 33. Wanaishia 32 Digrii wakikupenda sana.

Na Lodge Inayotoa Ufundi au maarifa ama ujuzi wa Digrii ya 33 ni Lodge moja tu ipo Ulaya inafahamika kama 33 DEGREE SCOTTISH RITE FREEMASONRY.

[emoji117]Kwasababu u-Freemason wa Ulaya ulichukua udhibiti wa Freemasonry kwahiyo Ukawa na mamlaka na Uka Banish piga marufuku Freemason aina nyingine. Kwahiyo Aina zingine za Freemasonry zipo ila Hazitambuliki ni ILLEGAL yaani Haramu.

[emoji117]Freemasonry Ki-asilia ni Jamii ya Siri. Secret Society. Leo hii Freemason wanajieleza kuwa "Freemasonry sio Siri bali Kilicho siri ni maana katika ishara zake na Ibada zake za Tambiko" Hii ni kauli ya Freemason ya Uingereza.

Freemason kiasilia ni SIRI (MYSTERY)

Kuna msemo mmoja kwenye Freemasonry unasema

"Always Conceal and Never Reveal"

"Kila wakati muda wote Ficha / fukia / fumba usifunue/usiseme/usitoe siri"

Unaona?

Hao wanao sema sio siri tena na wale wa Kujitangaza ni Freemason Bandia pia sio tu Freemason Bandia ya Ulaya bali pia inaweza kuwa ni Utapeli.

[emoji117]Miongoni mwa Kikundi au aina ya Freemasonry ambayo imekataa kujisalimisha kwa Waingereza na ni Freemason au aina ya Freemason ambayo ni Tishio kubwa kwa Freemasonry ya Ulaya ya wazungu (EURO FREEMASON) inaitwa

EGYPTIAN FREEMASONRY, aiina hii ya Freemasonry inayofahamihamika kama U- FREEMASON WA MISRI awali au jina lake la asili inajulikana kama

ESOTERIC FREEMADONRY. Kuifahamu aina hii ya U-Freemasonry rejea kitabu kinaitwa "ESOTERIC FREEMASONRY".

Katika aina hii ya Freemason ni ya tofauti kabisa, Hakuna Biblia hakuna Qur'an hawamtaji mkristo au dini hizo. Hawatumii Biblia au Qur'an kuwafundisha maadili wanachama wake. Ni aina ya Fresmason kabla ya ukristo na uislamu na ndiyo Orijino Freemasonry.

Freemason hii imejikita kuwafanya wanachama wake kuwa wenye uwezo wa juu . Inafundisha mbinu za kale za siri za kufungua uwezo wa mwanadamu kwa asilimia 100, Kumbadilisha mwanadamu kuwa kutoka katika ubinadamu kuwa Mungu, Wanafundisha kupata uwezo wa maajabu (Pschic Abilities), freemason hii pia wanafundisha kuzungumza kufanya mawasiliano au kukutana na viumbe wasio onekan wa ulimwengu mwingine (Paranormal Experience), Kusoma DNA, kufungua DNA

Kiujumla wanajikita kwa kina kwenye uwezo wa mtu. Inaitwa ESOTERIC FREEMASON.

Freemason hii ilijikita kwenye jukumu la asili la kutoa maarifa.

Kwasababu Freemasonry kiuhalisia tofauti na watu wanavyo ichukulia leo "Is just a mystery school in our modern days" ni shule ya Siri au mystical school katika zama zetu hizi mpya hakuna lingine.

Kwa mujibu wa Waingereza Freemasonry ya Ulaya Ni Freemason Haramu.

FREEMASONRY YA UINGEREZA

[emoji117]Kwa kuzingatia masharti yao au sifa za kumfanya mtu awe mwanachama wao

-"You must be a man of a good repute"

Ili kuwa mwanachama wa Freemason ya Uingereza lazima uwe mwanaume...mwenye tabia njema.

Alafu ngoja niseme "Freemason ni kwa ajili ya Wanaume tu"

Freemason ya WanaWake ilianzishwa mwaka 2015 inaitwa THE ORDER OF WOMEN ilianzishwa huko Uingereza.

Hakuna Freemason ya wanawake popote isipokuwa Uingereza.

Swali: "Mbona kuna picha nyingi zinaonyesha kuna Freemason Wanawake?"

Hiyo ni Aina nyingine ya Freemason ambayo ipo kwenye kundi la USHRINA - SHRINE.

Lodge yao ni inakuwa na watu mchamganyiko wanaume na wanawake na inajulikana kama "EASTERN STAR LODGE" Ni aina Ya Ufreemason wa kiislamu yaani USHIRINA.

Lengo lao kuu la hawa Freemason ya Ulaya ya Wazungu wanasema

"To make a good man into better man"

kwamba Lengo lao ni Kumfanya mwanaume mzuri kuwa bora zaidi.

Umeielewa ni kauli mbiu ya Freemasonry ya wazungu.

Ndani ya Lodges za Freemasonry kuna makundi au vikundi ikiwepo THE WHITE BROTHERHOOD , Hiki ni kikundi katika Lodge cha watu wanao pewa siri zote wanajua yote kuhusu Lodge yao na ukweli wao na wanapewa uwezo wa kudhibiti wengine.

Kwahiyo wanachama wengine wasio ndani ya kikundi hicho Wanakuwa wakitumika tu kama SLAVES without their notice.Hili limefafanuliwa zaidi katika Kitabu kiitwacho "Esoteric Freemasonry"

Freemason ya Ulaya wanaposema lengo lao ni kumbadili Mwanamume MZURI kuwa Bora zaidi.

Kupitia Ufahamu wa Jicho la tatu kutoka ndani:-

Freemason hawa wana maana hii; Freemason hutafuta watu ADIMU (Mwanaume mzuri) wenye zawadi au kitu fulani Special ndani yao au MaGenius wanawaingiza ndani ya Jumuiya yao ili utaalamu wao uwe faida kwa Freemasonry.

Watu wenye nyota na uwezo fulan huwa wanawachukua na watu hao hufanya mambo makubwa katika jumuiya kupitia uwezo wao na Sifa na utukufu unakuwa wa Jumuiya.

Mambo yote makubwa yanayo aminika yamefanywa na Freemasonry si kweli yamefanywa na watu wenye uwezo ambao hapo swali walichukuliwa na kuunganushwa Freemasony na kuacha faida katika Jumuiya yao miongoni mwao.

Hali hiyo inaashilia unyonyaji, utumwa Tofauti na Esoteric Freemasonry inayo toa uwezo kwa watu.

FREEMASON hawajaja kubadili maisha yenu au kuwaletea Mafanikio ni Uongo...

FREEMASON Hawajaja kumfaidisha yoyote wamekuja kwa maslahi yao wao ndio wanatafuta huo ukuu mafanikio wanayatafuta kwa kuwatumia nyie wenyewe bila kujielewa.

Kwasababu Funguo za Siri wanazo wao, mtu wa nje huwezi kujua, wanakutumia na si kwamba wanakuhitaji bali wanakutumia kwa manufaa yao.

[emoji117]FREEMASON MEMBERS wanao pata Raha wanapokuwa ndani ya Freemason ni wale tunaowaita BLOODLINE wenye Damu yao. Ndio maana Freemason wanaitana NDUGU, BROTHERS, KAKA au DADA kwanini?

FREEMASON ni Ndugu ni Ukoo wana damu moja. Ukoo huo wenye damu moja ni Ukoo wa wajanja .. Na ni ndugu wanakusanyana wao kwa wao wanakula maisha. Ila kama huna damu yao na wakikualika basi una kitu special wanataka wakutumie wakishapata faida yao unatoweka unakuwa huna kazi tena.

SO BE CAREFUL YE MEN OF KHEM

[emoji117]Sasa Freemason hii ya Ulaya ndio tunaita WALUCIFERI au LUCIFERIANS.

Hapo Dr Malachi Z. York amewadadavua kwa kina. Ambapo yeye mwenyewe Malachi Z york hapo awali alikuwa mwanachama mwaminifu wa Freemasonry ya Ulaya ya Wazungu ambapo akaamua kurejea kwenye Freemasonry Ya Afrika huko Misri - Egypt na kuanzisha kikundi chake mwenyewe cha U-Freemasonry wa Africa.

[emoji117]Martin Luther King ni miongoni mwa member wa Freemasonry ya Africa na alianzisha Lodge yake aliita MARTIN LUTHER LODGE NO...

Bob Marley ni Freemason ila sio Freemason ya Ulaya.

ELIJAH MUHAMMAD ni Freemasonry member wa Freemasonry Ya Afrka aliangazia sana katika enzi zake USHRINA WA AFRIKA Ufreemason wa Kiislamu wa Afrika, ambao asili yake ni Usislamu wa kale wa WAMOA au MOORS

MTUKUFU DREW ALLY ni Freemason muanzilishi wa Taifa la Kiislamu NOI yaani Nation Of Islam. Alikuwa ni Mwanachama wa Uislamu wa Kifreemason au Ushrina wa Afrika.

Watu hao na wengineo walikuwa wakijaribu kuleta mapinduzi kwenye Freemasonry Ya Ulaya.

Taratibu Watu weusi walianza kuruhusiwa kujiunga na Freemasonry.

Hapo awali hawakuruhusiwa.

Hilo pia unaweza kulipata hapa Tanzania kwenye kitabu cha SIR JAYANTILAL KESHAVJ CHANDE au maarufu kama SIR ARNDY CHANDE katika kitabu chake kiitwacho A KNIGHT OF AFRICA, A JOURNEY FROM BUKENE... Anaeleza historia na misuko suko aliyo ipitia katika harakati za kujiunga Freemasonry.

Chande Anaeleza wazi kuwa kwenye Freemasonry kulikuwa na Ubaguzi wa wazi. Wahindi na Waafrika hawakuruhusiwa kabisa kujiunga Freemasonry.

Lakini Hapo Baadae Wahindi waliruhusiwa akiwemo Rafiki yake MR PETEL mwanachama wa kikundi cha kibiashara cha matajiri kinacho fahamika kama ROUND TABLE, Lakini Wahindi hao walipewa nafasi ya kujiunga kwenye Daraja la Chini Kabisa lililo itwa "NYOTA YA JUHA"

Hilo linathibitisha nilicho toka kuongea.

[emoji117]Tuna maanisha nini tunaposema mtu ana damu ya Freemasonry (The Bloodline) au hana. Ikumbukwe Hapa Duniani sisi sote ni Miseto au Hybrids. Kwanini? Kama tunaenda pamoja katika nakala zangu za zamani kwamba Hakuna aliye umbwa kw Udongo ... wanadamu tumetokana na Mchakato wa kisayansi wa uchanganyaji wa Jeni (Genetic Splicing) au Uhandisi wa kijenetiki (Genetic Engineering) ..

Kazi hii imewekwa vizuri sana na Malach Z york ..kwamba katika tamaduni zote inaaminika hapo awali kabla yetu Dunia hii ilitembelewa na viumbe kama wanadamu kutoka kwenye Nyota.

Hadithi hizo zipo hadi leo Nigeria, Mali, Misri, Rwanda...pale Rwanda viumbe hao wanawaita au waliwaita KINYAMUKELA ... Hadithi kama hizi za ujio wa viumbe wageni walikuja kutuzaa kupitia Genetic Manipulation ,ipo katika Tamaduni zote Duniani.

Kwahiyo baadhi ya makundi ni wajanja wamejitenga wanakusanyana wenyewe wakiwa wameshika funguo za siri za ulimwengu wanapeana siri za mafanikio wao kwa wao chini ya kivuli cha nguvu isiyo onekana na huku kinyume chake WANATAWALA ULIMWENGU.
FB_IMG_17180084436675791.jpg
FB_IMG_17180084372638608.jpg
 
Endelea kutiririka kiongozi

Halaf naomba kufahamu wewe ni mwanachama au ni mtu tu uliyena elimu juu ya masonic ?🙏🙏
 
Back
Top Bottom