SoC02 Je, upi wajibu wa Serikali kwa Vijana?

SoC02 Je, upi wajibu wa Serikali kwa Vijana?

Stories of Change - 2022 Competition

Gandhi

New Member
Joined
Jul 25, 2022
Posts
3
Reaction score
1
Ni swali adimu leo hii kuliskia viongozi wakiulizwa leo hii, pamoja na ukweli kwamba vijana wamefikia 70% ya Watu wote nchini. Isitoshe pale unaposkia vijana wakitajwa au kuzungumziwa mara nyingi unaskia wajibu wao tu kama vijana.

Na katika Mkwamo mkuu wa Ajira vijana bado vijana atarudishiwa mpira ajiajiri!, utadhani aliandaliwa vyema na kupewa misingi itakayompelekea kujiajiri.je kwenye afya kijana hana changamoto huko wajibu upi achukue? Je kwenye sekta madini?

Je kwenye uongozi?
Kwenye Maadili na Tamaduni bado yeye tu?

Je, huyu kijana anazijua Haki zake? Kijana ametengwa kama kifaranga cha kuku kienyeji anayepaswa kutafuta chakula bila kuwa na Mama wala Baba Lakini anafarijiwa kuwa yeye Ndiye Baba ajaye na Mama ajae sijui atawezaje kukua katika mazingira yenye changamoto nyingi mno na Adui kunguru akimsubiri kwa hamu.

Sehemu pekee ambayo wajibu wa Serikali kwa Vijana ubainishwa ni kwenye Sera. Mwaka 1996 ndipo kwa mara kwanza kama Taifa tulikuwa na Sera ya vijana binafsi hii ni kati ya Sera bora kabisa ya Vijana kuliko ya Mwaka 2007, japo pamekuwa na mabadiliko makubwa ya kitechnologia (tehama) na Utandawazi (Globalization )

Lakini ilikuwa Sera yenye draft nzuri mno kwanza iliandikwa kwa lugha rahisi ya kiswahili, pili ili eleza umuhimu wa sera na malengo ya sera na kubainisha wajibu wa kila sekta kuanzia Ngazi ya Familia, Sekta ya Afya, Maaliasili na Utalii, Biashara, Makazi na Ardhi, Fedha, Elimu, kilimo, Madini na Nishati, Maendeleo ya watoto na wanawake, Tume ya Mipango, Makampuni binafsi, Baraza vijana na Kamati za Maendeleo ya Vijana toka Ngazi Mkoa mpaka kijiji nk.

Kila sekta na wajibu wake kutekeleza ulianishwa, hii sera ingekuwa rahisi hata kupima wapi tulipotoka na kufikia, wapi tuliteleza baada ya miaka kupita ikaja Sera ya vijana mwaka 2007 yenye Lugha ya kingeni (English ) yenye kuweka mambo kijumuishi (generalized ) na haikutumia sekta yenyewe ilipendelea kutumia Serikali kuu. Hapa ndipo kijana alipotelekezwa , hata hivyo yapata miaka 13 toka Sera yadanganya toto ya mwaka 2007.

Hakuna Toleo jingine hakuna cha Baraza la vijana walolisema baada ya kuondoa hata kamati ya vijana maendeleo ilokuwa toka mkoa mpaka kijiji, Mbaya zaidi vijana waleo ni zao la mfumo mbovu hivyo wengi wao sio wadadisi, kwakuwa hawana Tabia za Mtu aliyelimika, wapo hawajui hata kwamba kuna Sera ya Vijana, wamebaki kushangilia tu kila wanasemayo wanasiasa, wamekunywa maji ya Bendera ya vyama


Ndimi :- Mathew Ambajo Nyadack

Mawasiliano :- 0762279474 / mathewambajo@gmail.com
 
Upvote 1
Back
Top Bottom