maishapopote
JF-Expert Member
- May 28, 2009
- 3,408
- 6,094
Kipindi cha nyuma walikua wakiitwa mashushushu,nowadays wanaitwa usalama,walikua wanaogopeka sana zamani lakini hv sasa tunaishi nao na pia wanajulikana wengi wao,siku hizi hata wengine huwa wanajisifia na kutoa silaha zao kwenye mabaa na sehemu za wazi kwa minajili ya kukuza jina,hebu wadau tusaidiane yafuatayo....
- Je Muundo wa Usalama wetu wa Taifa Ukoje?
- Je watu hawa huwa wanapata training za kutosha?
- Wanachaguliwaje hawa?
- Je hakuna hatari kwa kutokua na ofisi yoyote ya wazi ambapo kama una information unaweza kuwapa(Angalia C.I.A)
- Je wako Trained Enough?(Rejea tukio la Mhe.Kupigwa kibao wakiangalia)
- Je mfumo wao wa uendeshaji hauna upendeleo(Angalia umri wa walinzi wa viongozi wetu na maumbo Yao)
- Je ni kweli wanaprotect Usalama wa nchi au usalama wa viongozi wetu?