Je, ushawahi kuugua hadi ukawa unawaonea wivu ambao hawaumwi?

Je, ushawahi kuugua hadi ukawa unawaonea wivu ambao hawaumwi?

The Burning Spear

JF-Expert Member
Joined
Dec 23, 2011
Posts
4,118
Reaction score
9,864
Maisha ni fumbo na fumbo lenyewe Lina kuja pale unapougua na hujui utapona au ndo mazima.

Kuna magonjwa yanayoeleweka yanakupa hope kwamba ni suala la mda tu mambo yatakaa sawa. Ila Sasa kuna haya magonjwa ambayo mtu unakuwa uncomfortable mda mwingi unameza dawa hadi mwili unanuka dawa.

Yani ukimwona mtu mwenye afiya unamtamani sana.

Afya ndo kila kitu mazee. Ukiambiwa Linda afya yako Linda kwelikweli. Tujiepusha na maradhi yanayoepukika hasa haya ya mtindo wa maisha.

Ni hayo tu kwa leo.
 
Mwili utunzwe kwa gharama yoyote.Kwa sababu hata kidole tu kikiwa na maumivu utakaa kwa uchungu na hasira kila wakati.Afya ni mtaji wa mambo mengine yote kwa binadamu.
Very true. Wengi hustuka baada ya tatizo kujitokeza while it is too late.

Na mtu akiugua mda mrefu saikolojia huwa inaharibika
 
Very true. Wengi hustuka baada ya tatizo kujitokeza while it is too late.
Sahihi kabisa.Tusifanye mambo kwa uzembe.Matokeo huwa mabaya;-
-usiendeshe kifaa/chombo cha usafiri kwa uzembe,
-usitumie vitu vyenye ncha kali bila tahadhari/uangalifu,
-usitembee barabarani bila kuwa muangalifu,
-usilale,usikae,usisimame au hata kupita sehemu bila kuihakiki usalama wake,
-usichezee moto,vifaa vya gesi au vitoavyo moto na joto bila sababu,
-usilale kingono(kupigana hata denda)na mtu bila kujua usalama wa afya yake wala historia yake,
-usiguse vitu,mtu au sehemu bila tahadhari na kujua vema,
-usifanye jambo bila kutafakari matokeo yake katika uchanya au uhasi wake.
NB:ORODHA IENDELEE...
 
Maisha ni fumbo na fumbo lenyewe Lina kuja pale unapougua na hujui utapona au ndo mazima...
Kuna mshkaji mmoja alikuwa hanywi pombe Wala havuti sigara, anaumwa sasaivi amefeli Figo zote Hadi anatia huruma aisee,

Hivi kwanini haya maradhi ya kufeli Figo yamekuwa mengi sasaivi, yaani asilimia kubwa ya watu wanasumbuliwa na tatizo la Figo
 
Life style imebadilika sana mkuu.
 
Mwaka 2007 nilikua nacheza mpira winga hatari, siku moja kipa sijui aliingiaje mguu ukavunjika, nilikua nakaaa ndani Tu mpaka nikawa nawatamania kuku wanavyotoka nje kutembea na kurudi, nikataman hata ningekua jogoo. Nilitibiwa kiasili mifupa iliunga Safi japo ni kama mguu mmoja umekua mfupi kidogo
 
Yani ukimwona mtu mwenye afiya unamtamani sana
kuumwa kunakera sana, basi tu, huwazi chochote iwe hela, pu$$y, etc yaani unapambania ku get well

ukidaka say homa, kukaa huwezi, kulala huwezi, kula ndiyo kabisa, roho mkononi hasa iwe usiku na ipande
unasikia wengine wanakoroma fresh kabisa yaani unatamani uwe wao

ajabu ukishapona ivyo vyote unavisahau
 
Shida ni hapo kwenye kusahau.
 
sipendi kuumwa, naogopa kuuguza pia mie ni mbovu sana wa mafua nikiumwa kdg na homa inafata yaani nikiona dalili za pua kuwasha mawazo yana anza sema kuna dawa za aleji nikimeza napata nafuu
 
Kuna mshkaji mmoja alikuwa hanywi pombe Wala havuti sigara, anaumwa sasaivi amefeli Figo zote Hadi anatia huruma aisee,

Hivi kwanini haya maradhi ya kufeli Figo yamekuwa mengi sasaivi, yaani asilimia kubwa ya watu wanasumbuliwa na tatizo la Figo
Swali ni je,kunywa pombe na kuvuta sigara tu ndivyo husababisha kufeli kwa figo?
 
Back
Top Bottom