Je, ushawahi kuwa dreamer?

Je, ushawahi kuwa dreamer?

James Hungury

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2013
Posts
825
Reaction score
612
Habari wapendwa,

Leo nataka nilete mjadala kwenu kuhusu kuwa Muotaji Hai. Mimi binafsi hii hali ishanikumba na mpaka sasa hujitokeza, na ilikuwa kama hivi;

Nilikuwa nikipenda kuota nikiwa mtu tajiri na wakat mwingine nilikuwa nikiendesha mawazo yangu vile nilivyotaka. Kwa mfano natengeneza mazingra nikiwa rais, na nikiwa nafanya mambo makubwa tu.

Hali hii nilikuwa naipenda sana, kuna wakati nilikuwa natamani niende kitandani ili niote mambo makubwa akilini mwangu, lakini hali hii ilikuwa ikifanyika nikiwa najitambua kitandani.

Sasa ndugu, nataka kujua je, kitu hiki kishawahi kukutokea? Au wataalamu mnaweza kutusaidia.

Ahsante..
 
Je, hayo uliyokuwa unaota baadhi yake yameshatokea? Hasa suala la utajiri:, unadalili hata ya kuzimiliki? Au ulikuwa unazimiliki kwenye ndoto tu?
 
sheikh yahya alisema "ndoto mara nyingi hua kinyumenyume" unaweza ukaota utajiri kumbe utakuja kupoteza pesa nyingi kias chakua fukara
 
Tafuta hela ndugu yangu...........ukitaka ulale tu uote.....utakaa sana........kuna kuku mmoja alikula mchele mchana........jioni akaliwa na wali...
 
Tafuta hela ndugu yangu...........ukitaka ulale tu uote.....utakaa sana........kuna kuku mmoja alikula mchele mchana........jioni akaliwa na wali...

Wewe utakuwa ni Preta original 😀
 
Last edited by a moderator:
Je, hayo uliyokuwa unaota baadhi yake yameshatokea? Hasa suala la utajiri:, unadalili hata ya kuzimiliki? Au ulikuwa unazimiliki kwenye ndoto tu?

mkuu nakumbuka,kuna mambo ambayo nilikuwa nikiyafkilia yametimia.kitu ambacho nakuwa nahs ni kwel
 
kiufupi mimi binafsi naweza kusema ni mwanzo wa kumjua Mungu anavyofanya kazi ila kidunia nitakwambia ni mwanzo wa dalili za matatizo ya akili..kifupi utashuhudia mengi ila kama ungeota unapaa kama malaika ungetamani ugande hivyo milele maana ni raha sana
 
Back
Top Bottom