Pyaar
JF-Expert Member
- Feb 11, 2018
- 16,078
- 77,186
Mama anashauriwa kumnyonyesha mtoto wake maziwa pekee kipindi chote cha miezi 6 ya mwanzo. Mtoto atakapofikisha miezi 6 ndipo amuanzishie vyakula vya nyongeza huku akiendelea kumnyonyesha.
KWANINI MIEZI 6?
Baada ya kipindi hiki cha miezi 6 tayari kutakuwa na bacteria wa kutosha wa kuwezesha mmeng'enyo wa chakula pasipo kuleta shida yoyote kwa mtoto.
Na kwa wale waliojifungua watoto wao kabla ya muda wa miezi 9 wanashauriwa kuwaanzishia chakula cha nyongeza pindi watoto wafikishapo umri wa miezi 8.
VIASHIRIA VYA MTOTO KUWA TAYARI KWA CHAKULA CHA NYONGEZA.
01. Mtoto akibebwa/kukalishwa hukimudu kichwa chake (shingo kukaza sawasawa).
02.Kuanza kulamba/ kuweka vitu mdomoni i.e midoli, chochote akionacho mbele yake.
03. Anaonekana kutamani sana vyakula muda wa kula chakula.
04. Ukimsogezea kijiko karibu anaanza kuking'ata ama kusogeza mdomo wake karibu na kijiko.
Ukiona dalili hizi sasa mtoto yupo tayari kuanzishiwa chakula..
*Vile vile kuna watoto ambao wanakuwa wamefikisha miezi 6 lakini hawajawa tayari kula vyakula vigumu, hivyo ni vyema pia kuangalia na kuzingatia viashiria hivi.
[emoji110][emoji110]