Je,Utawala wa Rais Hassan ndio Umemfitini James Mbatia NCCR-Mageuzi, je, Tanzania Mpya yenye uponyaji

Je,Utawala wa Rais Hassan ndio Umemfitini James Mbatia NCCR-Mageuzi, je, Tanzania Mpya yenye uponyaji

Pang Fung Mi

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2022
Posts
6,653
Reaction score
13,919
Hello JF

Wote au baadhi tunafahamu namna James Mbatia alivyo na amejidhihiri kuwa mstari wa mbele kuonya, kushauri na kukemea maovu kwa namna ya heshima, unyenyekevu na staha yenye uzalendo kwa nchi yake.

Ni ajabu kuona yaliyotokea juu ya nafasi yake ya uenyekiti wa NCCR Mageuzi katika kipindi kinachoitwa cha ufunguzi na uponyaji wa nchi.

Ni vyema hao wanaoishi siasa na uongozi wa kijima na kimwinyi wajitafakari maana utofauti na ukinzani wa kifikra ndio usahihi wa uumbaji wa Mungu wetu sote.

Wapinzani wanaonufaika na awamu hii furaha zao yumkini si za kudumu pengine wawe na agenda binafsi na manufaa kumuunga mkono mfalme katika jitihada zake za kupambana na vita ndani ya kasri lake mwenyewe.

Kwa asili asiye na subra, uhimilivu, ukomavu, busara na ufahamu wa kutosha wa mambo katika nchi na watu wake hujigeuka mwenyewe.

Muda utaongea

Good morning.

Je, siasa ni yetu na nchi ni yao na utukufu ni wao? utengamano ni pamoja na haki na usawa.

Wadiz na fikra tunduizi kuelekea siasa za maigizo ya kimajukwaa.
 
Back
Top Bottom