GLOBAL CITIZEN
JF-Expert Member
- Jun 5, 2014
- 767
- 1,657
Greetings!
Leo nataka nikupe darasa muhimu kabisa jinsi unavyoweza kutengeneza digital product zako binafsi na kuanza kuuza mtandaoni mara moja.
Hili darasa ni muhimu kwasababu watu wengi wapo na maarifa fulani lakini hawana uelewa wakutosha kutumia maarifa hayo waliyonayo na kufanya iwe biashara inayowaingizia pesa.
Kama unapitia changamoto hii basi endelea kunisoma utanufaika kwa mengi siku ya leo.
Kwa kuanza naomba niseme kila mtu anakitu fulani anachopendelea.
Hii inaweza kuwa…
• uandishi
• masuala yanayohusu safari
• mambo yanayohusu utamaduni
• mambo yanayohusu teknolojia na ugunduzi
• mambo yanayohusu maisha binafsi na healthy living
• mambo yanayohusu Online Business
• mambo yanayohusu mitindo na mavazi
• kilimo na ufugaji wa kisasa
• mambo yanayohusu kusaidia wanafunzi wa college au university
• kutoa taarifa za mambo mengi yanayohusu sehemu unayoishi.
There so many hobbies you can turn them into business.
Sasa basi.
Iwapo unaufahamu kuhusu moja ya maeneo niliyoyataja hapo juu basi unaweza ukaanza Online Business na kukutengenezea side income.
Kwa kuanza inabidi ufuate hatua ninazoenda kuzielezea hapa chini.
1 • Jihabarishe zaidi kuhusu eneo unaloenda kuanzisha Online Business.
Hapa unahitaji kusoma zaidi au kufanya utafiti zaidi kuhusu hobby au eneo ulilochagua ili uwe na uelewa mpana.
Kwa mfano umechagua eneo la food & healthy living inabidi uongeze ufahamu wako kuhusu eneo hili ili uwe na authority.
2 • Tengeneza BLOG na pia Social Media Page.
Yep.
Very important.
Blog yako itakuwa ni uwanja wako wakuelezea mambo yote kuhusu eneo ulilochagua.
Hapa utaweza kuandika mambo mengi na mwisho wa siku watu watakufuata ili wajifunze kwako.
Na ukifikia stage hii utaanza kutengeneza pesa.
Pia kupitia blog yako utaweza kuruhusu Google Adsense waweke matangazo yao na wewe utalipwa kila mwisho wa mwezi.
Nikirudi kwenye Social Media Page niseme hii itasaidia sana kukuza brand awareness.
Social Media ambayo napendekeza kwajili yakukuza brand ni Instagram.
Ukiwa na Page yako utajifunza kutumia promotions ili kuongeza idadi ya watu wanaoona post zako na Page yako.
3 • Andika Quality Content kuhusu eneo ulilochagua kwaajili ya potential customers wako.
Hii ni muhimu sana.
Unahitaji kuandika vitu vinavyofundisha na si blah blah.
Readers wako wakiona hakuna value wanapata toka kwenye huduma unayojaribu kuanzisha watakukimbia.
Kwahiyo zingatia sana kuandika quality Content.
Pia ziwe original.
Uki-copy na ku-paste toka sehemu nyingine Google watafahamu kwasababu wanatumja algorithms kujua kila kitu kinachoendelea kuhusu Blog yako.
Na wakigundua hawatakuruhusu kutumia Google Adsense.
4 • Tengeneza Email List.
Hii ni very very powerful.
Ukiwa na Email List utauza huduma au product yako kwa urahisi sana.
(Niandikie iwapo unahitaji kujifunza zaidi hapa)
Pia unaweza jifunza zaidi kuhusu Email Marketing hapa
5 • Andaa course inayofundisha kuhusu jambo fulani katika eneo la interest yako.
Ok.
Ngoja nitoe mfano.
Labda eneo ulilochagua mwanzo ni kuhusu mambo ya kusafiri (hapa inamaana unauzoefu wa kusafiri nchi au sehemu nyingi tofauti)
Sasa hapa unaweza andaa maelezo ya kina kuhusu jinsi yakupata Visa kwa mara ya kwanza kwenye Ujerumani au sehemu yoyote ile.
Utaelezea mambo yote yamsingi yakuzingatia ili kweli mtu anayependa siku moja asafiri kwenda Ujerumani apate taarifa sahihi.
Hapa utapanga kiasi cha pesa unakacho toza kwaajili ya taarifa uliyotumia muda na ujuzi wako kuiandaa.
Pia unaweza kwenda mbele zaidi na kutoa huduma ya kuelekeza hahitaji kwa njia ya simu.
6 • Jiunge na Affiliate Program.
Hatua inayofuata ni kujiunga na affiliate Program ili ujitengenezee passive income.
Hapa utakachotakiwa kufanya ni kuwela affiliate link yako katika kila post unayoandika.
Kumbuka post zako zitaendelea kusomwa kwa muda mrefu kwahiyo hapa utaendelea kutengeneza passive income kila mara msemaji wa post yako atakapo nunua bidhaa kwakupitia affiliate link yako.
7 • Apply for Google Adsense.
Baada ya kuandika post za kutosha katika Blog yako (at least 30 original posts) sasa niwakati wakufanya application ili upate Google Adsense.
Lengo lakupata Adsense ni kuwezesha Blog yako kuingiza pesa kwakutumia matangazo (Content Ads) yatakayoonyeshwa na Google katika Blog yako.
Google Adsense ni nzuri kadiri unavyozidi kupata Visitors katika Blog yako.
Kwa mfano Blog yako ikiwa inatembelewa na 20,000 visitors kwa mwezi basi utatengeneza pesa nzuri tu bila jasho ( $ 200 – $ 400)
Hiko ni kiasi kizuri kwa life ya Tanzania [emoji1241]
8 • Endelea kuandika kuhusu eneo la biashara yako kila siku.
Yes.
Kwasababu sasa email list yako inaendelea kukuwa na pia blog yako inaendelea kukuwa basi jambo unaloweza kufanya hapa ni kuendelea kuandika zaidi.
Hii itaongeza traffic kwenye blog yako lakini pia business brand yako itafahamika zaidi.
Pia usiache kuendelea ku-post katika Page yako ya Instagram.
Ni matumaini yangu umefaidika na darasa la leo.
Iwapo unahitaji kujifunza zaidi niandikie.