Je utumiaji wa maneno haya ni udhalilishaji wa wanawake?

Je utumiaji wa maneno haya ni udhalilishaji wa wanawake?

Chapakazi

JF-Expert Member
Joined
Apr 19, 2009
Posts
2,874
Reaction score
316
Nimekuwa nikiangalia post mbalimbali hapa jamvini, na nimegundua kuna lugha inayotumika ambayo kwangu binafsi ningehisi inadhalilisha wanawake. Lugha hii inalenga hasa tendo la ndoa. Kwa mfano, utakuta mtu anatumia maneno kama:
Kumtenda, kumfanyizia, kumshughulikia, kumbamiza, kum-do, kum-mega, nk,nk
Sasa wandugu nashindwa kuelewa, maana katika post hizi utakuta kuna wanawake wanachangia kwa hali na mali. Je ni kuwa hawaoni hiyo lunga ya udhalilishaji, au ni mazoea, au ni kuwa wamekubaliana na hali halisa ya mfumo dume?
 
Chapakazi, ni kweli maneno haya ni ya udhalilishaji na yanatumiwa sana na wahuni au wale wasio na mapenzi ya kweli au wasiojua mapenzi nini, na huyafatumia kwa watu ambao hawana malengo nao, sidhani kama unaweza tumia maneno hayo kwa mtu umpendaye kwa dhati kama mkeo au mchumba... kwa kifupi ni maneno ya wahuni
 
Mbona yanatumika huku ndani na wanawake wanajibu posts bila shida?
 
Kwasababu wewe huyatumii, huwezi kusema niya kihuni au wanaoyatumia ni wahuni!!
 
Mbona yanatumika huku ndani na wanawake wanajibu posts bila shida?

sidhani kama kuna mwanamke wa kweli anaweza tumia maneno yenye ukakasi kama hayo, nadhani kama yupo atakuwa na matatizo, kuna maneno yenye staha ambayo ni mbadala wa hayo yasio na upako. Mfano unaposema unamega, nini kinamegwa hapo? na nani anayemega?
 
Mfumodume uko so deep katika system yetu wengine hata hawaujui.

Ushawahi kujiuliza kwa nini mwanaume ndiye "anayeoa" na mwanamke ndiye "anayeolewa", maana katika Kiswahili hatuna "kuoana" kwa maana ya kila mmoja kumuoa mwenzake.

Tamaduni na dini zetu nyingine hata mwanamke akitaka talaka inabidi amuombe mumewe amtaliki yeye mke, kwani mke hana nguvu ya kumtaliki mume, kwa logic ile ile ya kwamba mwanamke kaolewa tu, sasa atataliki vipi wakati yeye kaolewa tu, mwenye haki ya kutaliki ni aliyeoa, mwanaume.

Talk about mfumodume.
 
Kuna maneno huwa tunatumia sio kwa
tunaowapenda bali kwa milupo....
Huwezi sema bar maid una make love nae..
Bali una mmega sio?????????
 
Kuna maneno huwa tunatumia sio kwa
tunaowapenda bali kwa milupo....
Huwezi sema bar maid una make love nae..
Bali una mmega sio?????????
Excuse me The Boss , what if that bar maid is your wife or gf or whatever, being a bar maid doesn't mean that she's a mlupo as you said, i hope ni kazi kama alivyo secretary ni vema unge2100 neno lingine like prostitute or s'mthing.
sorry kama nimekukwaza Boss.
 
excuse me the boss , what if that bar maid is your wife or gf or whatever, being a bar maid doesn't mean that she's a mlupo as you said, i hope ni kazi kama alivyo secretary ni vema unge2100 neno lingine like prostitute or s'mthing.
Sorry kama nimekukwaza boss.

nashkuru kwa kunirekebisha....
I mean any loose woma.prostitutes na wengine kama hao...
 
ahaaaa!! kumbe mi nilidhani yametumiwa ili kupunguza ukali wa maneno
ambayo yangepaswa kutumiwa hapo, oook!!
 
Kuna maneno huwa tunatumia sio kwa
tunaowapenda bali kwa milupo....
Huwezi sema bar maid una make love nae..
Bali una mmega sio?????????
Boss,huko nchi gani? Unajua barmaid wa dunia ya kwanza wont even give you a look.
 
For a woman we call names...women of ill repute wajameni na hao wanaume tunawaitaje. ..Name calling should be both sides au ? Maana there men out there bad to the bone!~
 
sidhani kama kuna mwanamke wa kweli anaweza tumia maneno yenye ukakasi kama hayo, nadhani kama yupo atakuwa na matatizo, kuna maneno yenye staha ambayo ni mbadala wa hayo yasio na upako. Mfano unaposema unamega, nini kinamegwa hapo? na nani anayemega?

Hata mimi nimekuwa napata shida sana kuelewa haya maneno.Na siyo haya tu...yapo mengi na hayana mantiki yoyote! Ukijaribu kuangalia kitendo chenyewe.. sijui!
Ila ukishindana sana na hii misamiati..japo ya udhalilishaji..utajistukia unagombana na watu...watu wameshajiwekea utamaduni wa kutusi hilo tendo tena kwa kuwalenga wanawake..cha kufanya ni kuwarekebisha pole pole kwa upole... bila kuwatukana au kuwajia kwa jazba!
 
Ivi hili tendo linamfanya mwanamke kuwa inferior? Na kama sio, kwa nini wazazi wanaringa zaidi wakipata mtoto mwanaume? Kwa mfano utasikia wakitumia maneno kama nina madume kadhaa, nk. Je inabidi tubadilike hadi huko? Na tunabadilikaje?
 
sasa mimi huwa nabaki hoi nikiona mwanamke
anatumia maneno kama haya,
kumegwa.
kupakuliwa.
na mengineyo....

huwa nabaki mdomo wazi,unapokuta mwanamke mwenye heshima zake
anapotumia maneno hayo....
 
sasa mimi huwa nabaki hoi nikiona mwanamke
anatumia maneno kama haya,
kumegwa.
kupakuliwa.
na mengineyo....

huwa nabaki mdomo wazi,unapokuta mwanamke mwenye heshima zake
anapotumia maneno hayo....

Unaweza kutupa mfano wa mwanamke mwenye "heshima" zake anayetumia au aliyewahi kutumia maneno uliyoyaorodhesha hapo juu?
 
ukweli ni ule alousema engineer 2 maneno hayo ni ya kihuni tu mtu na staha zake huwezi kumsema eti umemmega, hata mume na mke hakuna biashara ya kumegana ila kufanya tendo la ndoa na kwa mahawara wanaoheshimiana hasa ni kufanya mapenzi na si kumegana kwa hiyo maneno hayo ni ya mtu ambaye humheshimu na umekutana nae kwa nia ya kukata kiu tu na sio uhusiano wenye malengo.

kuh mfumo dume na wazazi kujisifu kwa wanavidume kadhaa ni dhana potofu tu tena kwa wazazi wa kizamani, now days mtoto ni mtoto tu tene mie kwa uzoefu wangu ni kuwa watoto wa kike ndio hutunza sana familia zao na wazazi wao wanapokuwa watu wazima kuliko wanaume.
 
Back
Top Bottom