Je uvaaji wigi una madhara kwa afya?

Je uvaaji wigi una madhara kwa afya?

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Katika miongo kadhaa iliyopita, uvaaji wa wigi umekuwa fasheni katika sekta ya urembo na hutumika hususan na wanawake. Ingawa uvaaji wa wigi huwafanya wanawake hao kuonekana mithili ya mtu aliyevaa kofia ngumu (helmet), lakini yaonekana ni mapendeleo ya wengi.

Wanaume wengi hujiuliza , "Ni kwanini kinamama hupendelea kuvaa wigi na kusuka nywele za bandia?, wakati hupendeza na kuwa warembo zaidi wakiwa na nywele zao za asili"

Wigi huvaliwa zaidi na kinamama wenye asili ya Afrika au Wamarekani wa asili ya Afrika. Lakini tukiangalia moja ya chimbuko hasa la uvaaji wigi ni ubaguzi uliokuwepo wakati wa utumwa ambapo wale wenye ngozi nyeupe na nywele shombeshombe walipewa kazi za ndani na wale wasio na ngozi nyeupe na nywele zisizo shombeshombe walifanyishwa kazi ngumu za mashambani.

Watumwa waliopelekwa barani Amerika hawakuweza kuzihudumia nywele zao kutokana na hali ngumu, na mabwenyenye waliwashusha hadhi na kuwavunja moyo kwa kuwaambia hawakuwa na nywele bali ni "manyoya".

Lakini sababu nyingine inayodhaniwa kuwaathiri wanawake wa asili ya Afrika ni fikra kuwa mwanamke mwenye nywele ndefu pengine hadi mgongoni ni mrembo zaidi. Pia siku hizi warembo na wanaoshiriki katika mashindano ya urembo hujaribu kurefusha nywele zao ili kuwa na viwango na aina za mitindo ya ughaibuni.

Pamoja na kuwa wanawake wanajaribu kuwa warembo kwa uvaaji wa wigi, zifuatazo ni baadhi ya hasara au madhara kiafya ya uvaaji wigi na usukaji wa nywele za bandia. Uvaaji wa wigi au nywele za bandia waweza kukusababishia mzio(allergy), endapo malighafi au kemikali zilizotumika kutengeneza wigi hiyo zitasisimua mfumo wa kinga ya mwili wa mvaaji.

Kupata mba ni tatizo jingine kutokana na uvaaji wigi, hii hutokana na kukosekana kwa hewa ya kutosha ya Oksijeni katika ngozi ya kichwa(scalp hypoxia) na katika tishu za shina la nywele. Kwa hiyo kama utaamua kuvaa wigi uhakikishe imetengenezwa kwa viwango vya ubora unaotakiwa na inapitisha hewa ya kutosha ya Oksijeni.

Pia waweza kunyonyoka nywele hata kama una nywele nzuri zenye afya, na kama utachagua kuvaa wigi na unataka kuepuka madhara hakikisha kuwa nywele zako ni safi, usilazimishe kuvaa wigi iliyo ndogo na yenye kubana sana, hakikisha unapata muda wa kupata hewa na nywele zako zinapakwa mafuta kuepuka ukavu wa ngozi ya kichwa na nywele kukatika .

Maumivu ya kichwa ni tatizo ambalo laweza kusababishwa na uvaaji wigi au usukaji wa nywele bandia. Wigi iliyo ndogo husababisha mkandamizo kichwani na kusababisha maumivu ya kichwa ya mara kwa mara.

Upotevu wa muda na fedha ni dhahiri kwa kuwa ufumaji wa nywele za bandia waweza kuchukua muda mrefu, itamlazimu mvaaji wigi kubadili kwa kununua mpya kila baada ya muda fulani au kuwa na wigi nyingi kwa ajili kubadili kulingana na fasheni.

Harufu mbaya huweza kujitokeza endapo mba na jasho vitachanganyikana na hupelekea uwepo wa bakteria au fangasi na kusababisha muwasho mkali, hii yaweza kumkosesha raha mvaaji wigi na mwenye kufuma nywele za bandia hasa pale anapokuwa katika majumuiko ya kijamii.Kama utachagua kuvaa wigi hakikisha nywele zako zinasafishwa na shampoo au sabuni, zinakaushwa vizuri na kupakwa mafuta.

Endapo mwanamama atachagua kuvaa wigi, asisahau kuwa nywele zake za asili zinahitaji matunzo, na azingatie wakati wa kununua wigi au nywele za bandia, ahakikishe ananunua yenye ubora unaotakiwa ili kuepuka madhara ya kiafya anayoweza kutokana na uvaaji wigi au anapofuma nywele za bandia.

By Doctor Joh
 
Aiseeee team natural hapa.... manzi akiwa na wigi namshusha vyeo tho i don't judge.

Sent from my Siemens kidole juu using JamiiForum mobile app.
 
Hakuna madhara yoyote
Mba hupata wavaaji na wasiovaa pia.
Harufu kichwani ni uchafu na kutoosha vichwa pia huweza mpata mwanamke yoyote asiyejali kichwa chake.
Maumivu ya kichwa kwa kuvaa wigi????
 
Na pombe zetu za usiku tunaomba mtuvumilie,
[emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji3] [emoji1] [emoji1] [emoji1]

UNATUMIA NGUVU SANA KUTETEA MAWIGI, BUT KUSEMA UKWELI BE NATURAL NDO UNAPENDEZA ZAIDI! KULIKO KUVAA MAKATANI NA MANYWELE YA MAVUZINI TOKA KWA WAHINDI!
Hakuna madhara yoyote
Mba hupata wavaaji na wasiovaa pia.
Harufu kichwani ni uchafu na kutoosha vichwa pia huweza mpata mwanamke yoyote asiyejali kichwa chake.
Maumivu ya kichwa kwa kuvaa wigi????

Sent using Jamii Forums mobile app
 
[emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji3] [emoji1] [emoji1] [emoji1]

UNATUMIA NGUVU SANA KUTETEA MAWIGI, BUT KUSEMA UKWELI BE NATURAL NDO UNAPENDEZA ZAIDI! KULIKO KUVAA MAKATANI NA MANYWELE YA MAVUZINI TOKA KWA WAHINDI!

Sent using Jamii Forums mobile app
Nimeongea ukweli
Pia Kila kiumbe hai ana haki kuchagua.
 
Kwanza inaonesha jinzi ambavyo mwanadamu ameamua kumtukana Muumba wake. Ati angempa makatani badala ya nywele. Pili, kuvaa kofia muda mrefu kumletelezea kipara au nywele laini sana mwanamume, je hayo ma wigi na weusi wake si ndo balaa?? Ndo maana wanawake wengi mnapigwa makofi kwa sababu mmesha wehuka
 
Nimeongea ukweli
Pia Kila kiumbe hai ana haki kuchagua.
Dada yangu ni kweli kila mtu ana haki ya kuchagua, lakini kuna vitu dada yangu ninyi akina dada mnazidisha mno, mfano Mungu amewapa rangi tofauti wengine weupe wengine weusi mbona weusi wanataka kuwa weupe ili hali weupe hawana hata mpango wa kuwa weusi, haya Mungu amewapa nywele ndeeefu nzuri kuliko hata sisi wanaume mbona mwaenda kuchukua nywele za makatani na hizo zingine mbadili nywele zenu za asili? ki ukweli mwanamke mwenye uasili wake anapendeza kwa asilimia mia zaidi ya artificial....

naombeni kumbukeni asili yenu, Mungu akukosea kuwaumba hivyo, aliwaweka hivyo ili mpendeze usoni pa dunia!!

ahsante!

Mimi ni mweusi na sina mpango wa kujichubua hivvyo siwezi kuwasemea wapaka mikorogo.
Kuna mitindo mbalimbali ya nywele sijawahi kusikia ya ngozi.
Je wanaume hambadili mitindo ya nywele?? Waweka kalikiti? Waweka wavu bleach??
 
Yeah madhara yapo mengi, ila kubwa zaidi mhusika ataonekana baamedi kwa haraka haraka!
 
Mwenye nywele nzuri na zenye kukua vyema lazima hatopenda wigi lakini mwenye nywele zisizo nzuri na hazikui vyema atapenda wigi sababu zina mstiri.

Pia wakati mwingine wigi inaepusha gharama ukiwa na wigi na safari imetokea ghafla unavaa tu unaenda.

Kila mmoja abaki na fikra zake kuhusu wigi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Katika miongo kadhaa iliyopita, uvaaji wa wigi umekuwa fasheni katika sekta ya urembo na hutumika hususan na wanawake. Ingawa uvaaji wa wigi huwafanya wanawake hao kuonekana mithili ya mtu aliyevaa kofia ngumu (helmet), lakini yaonekana ni mapendeleo ya wengi.

Wanaume wengi hujiuliza , "Ni kwanini kinamama hupendelea kuvaa wigi na kusuka nywele za bandia?, wakati hupendeza na kuwa warembo zaidi wakiwa na nywele zao za asili"

Wigi huvaliwa zaidi na kinamama wenye asili ya Afrika au Wamarekani wa asili ya Afrika. Lakini tukiangalia moja ya chimbuko hasa la uvaaji wigi ni ubaguzi uliokuwepo wakati wa utumwa ambapo wale wenye ngozi nyeupe na nywele shombeshombe walipewa kazi za ndani na wale wasio na ngozi nyeupe na nywele zisizo shombeshombe walifanyishwa kazi ngumu za mashambani.

Watumwa waliopelekwa barani Amerika hawakuweza kuzihudumia nywele zao kutokana na hali ngumu, na mabwenyenye waliwashusha hadhi na kuwavunja moyo kwa kuwaambia hawakuwa na nywele bali ni "manyoya".

Lakini sababu nyingine inayodhaniwa kuwaathiri wanawake wa asili ya Afrika ni fikra kuwa mwanamke mwenye nywele ndefu pengine hadi mgongoni ni mrembo zaidi. Pia siku hizi warembo na wanaoshiriki katika mashindano ya urembo hujaribu kurefusha nywele zao ili kuwa na viwango na aina za mitindo ya ughaibuni.

Pamoja na kuwa wanawake wanajaribu kuwa warembo kwa uvaaji wa wigi, zifuatazo ni baadhi ya hasara au madhara kiafya ya uvaaji wigi na usukaji wa nywele za bandia. Uvaaji wa wigi au nywele za bandia waweza kukusababishia mzio(allergy), endapo malighafi au kemikali zilizotumika kutengeneza wigi hiyo zitasisimua mfumo wa kinga ya mwili wa mvaaji.

Kupata mba ni tatizo jingine kutokana na uvaaji wigi, hii hutokana na kukosekana kwa hewa ya kutosha ya Oksijeni katika ngozi ya kichwa(scalp hypoxia) na katika tishu za shina la nywele. Kwa hiyo kama utaamua kuvaa wigi uhakikishe imetengenezwa kwa viwango vya ubora unaotakiwa na inapitisha hewa ya kutosha ya Oksijeni.

Pia waweza kunyonyoka nywele hata kama una nywele nzuri zenye afya, na kama utachagua kuvaa wigi na unataka kuepuka madhara hakikisha kuwa nywele zako ni safi, usilazimishe kuvaa wigi iliyo ndogo na yenye kubana sana, hakikisha unapata muda wa kupata hewa na nywele zako zinapakwa mafuta kuepuka ukavu wa ngozi ya kichwa na nywele kukatika .

Maumivu ya kichwa ni tatizo ambalo laweza kusababishwa na uvaaji wigi au usukaji wa nywele bandia. Wigi iliyo ndogo husababisha mkandamizo kichwani na kusababisha maumivu ya kichwa ya mara kwa mara.

Upotevu wa muda na fedha ni dhahiri kwa kuwa ufumaji wa nywele za bandia waweza kuchukua muda mrefu, itamlazimu mvaaji wigi kubadili kwa kununua mpya kila baada ya muda fulani au kuwa na wigi nyingi kwa ajili kubadili kulingana na fasheni.

Harufu mbaya huweza kujitokeza endapo mba na jasho vitachanganyikana na hupelekea uwepo wa bakteria au fangasi na kusababisha muwasho mkali, hii yaweza kumkosesha raha mvaaji wigi na mwenye kufuma nywele za bandia hasa pale anapokuwa katika majumuiko ya kijamii.Kama utachagua kuvaa wigi hakikisha nywele zako zinasafishwa na shampoo au sabuni, zinakaushwa vizuri na kupakwa mafuta.

Endapo mwanamama atachagua kuvaa wigi, asisahau kuwa nywele zake za asili zinahitaji matunzo, na azingatie wakati wa kununua wigi au nywele za bandia, ahakikishe ananunua yenye ubora unaotakiwa ili kuepuka madhara ya kiafya anayoweza kutokana na uvaaji wigi au anapofuma nywele za bandia.

By Doctor Joh
Ki ukweli mie sipendi msichana kuvaa wigi bora asuke rasta yaan akivaa wigi daah nakosa mood nae kabisa, maana hata kwenye mambo yetu atakuwa anatoa ushirikiano hafifu kwa kuhofia wig kukaa vibaya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom