Inategemeana na matokeo ya uamuzi yalivyo athiri timu yako.
Kama VAR kwa upande wa timu yako iliamua kitendo ambacho kilienda kuinufaisha timu yako unauoishabikia basi hapo lazima uifurahie VAR
Ila kama ndio timu yako imekuwa victim kila tukio linaloamuliwa na VAR imekuwa ikiadhibiwa basi lazima uichukie.
Ila in general VAR imekuja kuleta radha kamili ya soka, mshindi apatikane kwa njia za halali.
Japo zipo baadhi ya acts unaona haziamuliwi ipasavyo na hili sio tatizo la VAR ni yule refa anayetafsiri hilo tukio.
Ndio maana watu wanafikiria uwezekano wa kuja na mfumo wa roboti lenye AI ambalo litakuwa programmed litaweza kuamua mechi bila kuwa na mihemko.