JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 685
- 1,124
Kwa mujibu wa taasisi ya FOPH (Kituo cha Afya cha Taifa) ya nchini Uswisi, uwezekano wa vitu hivyo kubeba maambukizi ni mkubwa endapo mtu aliyeathirika atashika kitasa cha mlango au simu huku akiwa na majimaji yaliyomtoka baada kukohoa au kupiga chafya
Endapo mtu asiye muathirika atashika vitu hivyo (vilivyoguswa na mwathirika) kisha akagusa mdomo, macho au pua yake basi atapata maambukizi ya #COVID19 kirahisi
Jambo la muhimu ambalo linasisitizwa ni kunawa mikono yako kwa sabuni na maji tiririka au utumie kitakasa mikono ili kuua #CoronaVirus
Epuka kugusa pua, mdomo na macho endapo mikono yako si misafi na salama. Na pia jitenge na wengine unapohudhuria kwenye mikusanyiko ya lazima