Je, vitambulisho vya machinga ni lazima au ni hiyari?

Je, vitambulisho vya machinga ni lazima au ni hiyari?

Matojo Cosatta

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2017
Posts
234
Reaction score
390
JE, VITAMBULISHO VYA MACHINGA NI LAZIMA AU NI HIYARI?

Kwa tafsiri yangu ya sheria ni kuwa Vitambulisho vya Machinga ni lazima na msingi wa tafsiri yangu ni rejea za sheria zifuatazo;

(1) Kifungu cha 22 A cha Sheria ya Utawala wa Kodi, Sura ya 438 kama ambavyo imefanyiwa mabadiriko na Kifungu cha 49 cha Sheria ya Fedha, 2017 (Sheria Na. 4 ya 2017) na Kifungu cha 44 cha Sheria ya Fedha, 2019 (Sheria Na. 8 ya 2019) hususani Kifungu cha 22 A (1) na (2) Sura ya 438 kama kilivyofanyiwa mabadiriko.

(2) Kanuni ya 6 ya Kanuni za Utawala wa Kodi (Usajiri Wafanyabiashara Wadogo na Watoa Huduma Wadogo), 2020 [the Tax Administration (Registration of Small Vendors and Service Providers) Regulations, 2020] ambayo ni Tangazo la Serikali Na. 36 of 2020 hususani Kanuni ya 6 (1) na (2).

Masharti ya Kifungu cha 22 A (1) cha Sura ya 438 pamoja na Kanuni ya 5 na 6 (1) za Tangazo la Serikali Na. 36 of 2020 yanamtaka kwa lazima Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (Commissioner General of TRA) kuwatambua na kuwasajiri Wafanyabiashara Wadogo na Watoa Huduma Wadogo (wachuuzi) ambao wanafanya biashara ndogo ndogo kwenye sekta ambayo sio rasmi wakiwemo wamachinga, mama ntilie, MCs, bodaboda nakadhalika

Mfanyabiashara mdogo na mtoa huduma mdogo akiwemo machinga akisajiriwa na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato basi ni lazima apatiwe Kitambulisho cha Biashara Ndogo Ndogo na ni lazima alipe Tshs 20, 000/= kabla ya kupatiwa Kitambulisho na haya ni matakwa ya .

Machinga akisajiriwa na Commissioner General of TRA basi ni lazima apatiwe Kitambulisho cha Biashara Ndogo Ndogo na ni lazima alipe Tshs 20, 000/= kabla ya kupatiwa Kitambulisho, na haya ni matakwa ya masharti ya Kifungu cha 22 A (2) na (3) cha Sura ya 438 pamoja na Kanuni ya 6 (2) na (5) za Tangazo la Serikali Na. 36 of 2020.

Imeandikwa na Matojo M. Cosatta.
 
Magu hajui mambo haya?

Rais sio Mwanasheria, hivyo, lawama zinapashwa kwenda kwa washauri wa Rais maswala ya sheria.

Mshauri wa Rais Maswala ya sheria katika Serikali na katika CCM na Mshauri Mkuu wa Serikali Maswala ya Sheria (Mwanasheria Mkuu wa Serikali) watakuwa wameshindwa kutimiza wajibu wao ipasavyo wa kumshauri vizuri Mhe. Rais na Mwenyekiti wa CCM Taifa.
 
Je, kuna ubaya gani kuwatambua wamachinga na kuwafanya walipe kodi sekta isiyo rasmi ni kubwa mno hapa nchini kusababisha kupoteza mapato au wachache walio sekta iliyo rasmi kubeba mzigo. Hili lisitumike kutafutia kura wapinzani.
 
Kama wewe ni machinga na hataki kitambulisho hulazimishwi kuwa nacho lakini usilete fujo
 
Je kuna ubaya gani kuwatambua wamachinga na kuwafanya walipe kodi sekta isiyo rasmi ni kubwa mno hapa nchini kusababisha kupoteza mapato au wachache walio sekta iliyo rasmi kubeba mzigo. Hili lisitumike kutafutia kura wapinzani.

Mimi binafsi ninaunga mkono kwa nguvu zote urasmisha wa shughuri ambazo sio rasmi kwa kuwa formalisation of informal sector ina faida nyingi kwa taifa ndo maana nimechukua fursa hii kuandika kuwa nilazima kisheria kutoa Vitambulisho kwa wamachinga.
 
Acheni Mzee Apumzike
Mtamuua Kwa Pressure
 
Vitambulisho gani havina details za mmiliki...??
Kwa mazingira hayo; vinamtambulisha nani?
Kama ni vya kodi mbona havikuuzwa na mamlaka husika...??
Je, TRA inaweza kuiambia dunia ni vitambulisho vingapi vimeuzwa na kiasi gani kimekusanywa hadi sasa...??
 
Sijawahi kuviona hivyo vitambulisho. Vina TIN za ya hao wamiliki?
 
Rais sio Mwanasheria, hivyo, lawama zinapashwa kwenda kwa washauri wa Rais maswala ya sheria.

Mshauri wa Rais Maswala ya sheria katika Serikali na katika CCM na Mshauri Mkuu wa Serikali Maswala ya Sheria (Mwanasheria Mkuu wa Serikali) watakuwa wameshindwa kutimiza wajibu wao ipasavyo wa kumshauri vizuri Mhe. Rais na Mwenyekiti wa CCM Taifa.
Siyo kweli!Rais ndiye alishauri hii sheria itungwe
 
Rais sio Mwanasheria, hivyo, lawama zinapashwa kwenda kwa washauri wa Rais maswala ya sheria.

Mshauri wa Rais Maswala ya sheria katika Serikali na katika CCM na Mshauri Mkuu wa Serikali Maswala ya Sheria (Mwanasheria Mkuu wa Serikali) watakuwa wameshindwa kutimiza wajibu wao ipasavyo wa kumshauri vizuri Mhe. Rais na Mwenyekiti wa CCM Taifa.

Kwa hiyo, Wakili Fatma Karume alikuwa sahihi kumshambulia AG?

Kwa hiyo, Fatma Karume kufutiwa uwakili kwa kosa la kumshambulia AG ameonewa?
 
Kwanini sasa hicho kitambulisho anachopewa kinakuwa hakina jina lake hicho ni kitambulisho chake kivipi maana yeyote akiokota kinakuwa cha kwake pia
 
Rais sio Mwanasheria, hivyo, lawama zinapashwa kwenda kwa washauri wa Rais maswala ya sheria.

Mshauri wa Rais Maswala ya sheria katika Serikali na katika CCM na Mshauri Mkuu wa Serikali Maswala ya Sheria (Mwanasheria Mkuu wa Serikali) watakuwa wameshindwa kutimiza wajibu wao ipasavyo wa kumshauri vizuri Mhe. Rais na Mwenyekiti wa CCM Taifa.

Sasa wangefanyaje kama wanaona ni kweli vitambulisho huwa haviuzwi kwanini wao wameuziwa Kwani wasingeweza kutambuliwa bila kutakiwa kulipia hicho kitambulisho. Alikuwa hana namna maana ushawishi wa Lissu ulikuwa unazidi kwenye hoja ya vitambulisho na sasa hoja imepoa
 
Mimi binafsi ninaunga mkono kwa nguvu zote urasmisha wa shughuri ambazo sio rasmi kwa kuwa formalisation of informal sector ina faida nyingi kwa taifa ndo maana nimechukua fursa hii kuandika kuwa nilazima kisheria kutoa Vitambulisho kwa wamachinga.

Lakini siyo lazima kukilipia kurasimisha shuguli za wamachinga hakuhitaji kuwepo kwa tozo sheria ingeweza kutungwa na vitambulisho wakapewa na kutambuliwa bila kutakiwa kulipia elfu 20
 
Lakini siyo lazima kukilipia kurasimisha shuguli za wamachinga hakuhitaji kuwepo kwa tozo sheria ingeweza kutungwa na vitambulisho wakapewa na kutambuliwa bila kutakiwa kulipia elfu 20

Kweli kabisa.
 
Back
Top Bottom