Maaskofu wameuliza swali; Je, watekaji wamevizidi nguvu vyombo vya Dola?
Kwanza tuangalie watekaji wanamiliki nini?
1. Magari ya kifahari, LAND CRUISER, NISSAN n.k., na plate no. za TANZANIA ambazo wanaweza kuvuka hata mpakani mwa nchi na nchi bila shida.
2. Silaha nzito za kivita wanazoweza kuzitumia popote pale nchini, hata kwenye makao makuu ya nchi DODOMA na wakafanikiwa kutokomea bila shida yoyote.
3. Vibali au vitambulisho vya kuwawezesha wapite njia au barabara yoyote nchini hata kama ni kutoka DSM hadi MBEYA bila kusimamishwa kwenye kizuizi cha Traffic police wala kuulizwa maswali.
4. Wanaweza kukufuatilia hata miezi kdhaa au wiki kadhaa kabla ya kufanyia wanachotaka kwa ujasiri na kwa uwazi kabisa, hata ukiwahisi vibaya ukaripoti Polisi picha zao, mawasiliano Yao, namba za gari yao au taarifa zao zozote nyeti, Polisi hawatachukua hatua yoyote Ile dhidi yao.
5. Wana uwezo wa kuja kukuchukua popote pale nchini hata katikati ya eneo lenye msongamano wa watu wengi na shughuli nyingi.
6. Hujitambulisha kama Polisi na hata watu watakao kuwa pamoja na wewe wakati huo wanapokuchukua wakiuliza "unapelekwa wapi?" Hujibu kituo cha ha Polisi.
Hizo ni baadhi ya rasilimali ambazo au aina ya uwezo ambao watu hao waliopewa jina la "genge la watekaji" wanamiliki
Historia ya matukio yaliyowahi kuripotiwa kutekelezwa na watu hao yanafanana kwa namna nyingi kama ifuatavyo;
A. Huwateka walengwa kwa namna inayofanana. Aidha kwa kupigiwa simu ya kirafiki, ya kikazi, au ya kukuhitaji kufika mahali flani kuhusu jambo ambalo umekuwa ukilifanya au kulifuatilia hivi karibuni. Lakini pia wanakuvizia ukiwa kwenye safari zako za kawaida za kila siku, au kwa kukufuata nyumbani kwako kabisa.
B. Wakiua au wasipoua watautekeleza mwili ama kukurudisha sehemu zinazofanana kimazingira. Aidha mbali na makazi ya watu, porini, au sehemu yenye utulivu isiyo na pilika za watu mara kwa mara.
C. Upelelezi wa matukio Yao haujawahi kukamilika.
D. Upelelezi wa matukio yao haujawahi kuleta suluhisho la kudhibiti matukio hayo, kukamatwa kwa wahusika wakuu au mpangaji na mratibu wa matukio hayo.
E. Hata ikisemwa upelelezi wa matukio hayo umekamilika kesi yake haijawahi kufikishwa mahakamani au mbele ya vyombo vya Sheria kama ofisi ya DPP kwa ajili ya hatua zaidi.
F. Baadhi ya wahanga wa matukio ya UTEKAJI wamelazimika ama kwa muda mrefu au kwa muda mfupi kuikimbia nchi na kwenda kuishi uhamishoni. Vinginevyo wamelazimika kuacha kufanya kile walichokuwa wanakifanya au kukisimamia awali.
Kwa mfanano huo, rasilimali, na uwezo walionao "genge la watekaji" ni dhahiri kuwa vyombo vya Dola hususani jeshi la polisi, vimezidiwa nguvu na genge hilo.
Ni dhahiri na hakika kuwa haitakuja kutokea kamwe kwa TISS (Idara ya usalama wa taifa) kukiri hadharani kuzidiwa nguvu na genge hilo.
Kwa sababu GENGE hilo limeundwa na SERIKALI nakuwezeshwa na kupewa sura ya WATU WASIOJULIKANA. Ambalo katika matukio yake jamii inaelekea kukubali na kuamini kuwa genge hilo ni "super power" kwamba lina nguvu na uwezo usioweza kuzuilika na vyombo vya Dola hususani jeshi la polisi.
Hilo ndio lengo kuu la waundaji wa kundi hili, shimo ambalo maaskofu wamekaribia kutumbukia ndio maana wamehoji, kwa sababu wanajua Haiwezekani kuvishinda vyombo vya Dola.
Ukweli ni kwamba, watu wengi hivi sasa tunajua IDARA YA USALAMA WA TAIFA inawafanyakazi kila nyanja. Hadi miongoni mwa walimu na Polisi wenyewe kuna watu wa usalama wa taifa. Kwaiyo ni ngumu tukio kufanyika halafu Usalama wa taifa wasijue.
Polisi wanaweza wasijue ila sio TISS, Kwa sababu TISS Wana agent kila Kona hivyo wako mbele ya matukio (hususani ya kutumia silaha) dakika 600 mbele!
Kwa sababu hiyo genge hilo la watekaji limejipatia nguvu kwa kutumia madhaifu yaliyopo kwenye muundo mzima wa vyombo vyetu vya Dola na namna upelelezi wa matukio ya UTEKAJI na jinai yavyofanyika.
Mfano mzuri ni kada wa CHADEMA wa Tanga kuchukuliwa na Polisi na wazazi wake kwenda kuripoti Polisi mtoto wao katekwa na watu WASIOJULIKANA Kisha Polisi hao hao ndo wafanye upelelezi, baadae wakakiri wako nae wanamuhoji kwa kosa la....😁
Au tukio la "afande" FATMA KIGONDO kupelelezwa na Polisi wenzake, ndio maana SACP MALLYA akasema "swala la afande ni general.... Si tumeamua kuliacha kama lilivyo" inawezekana kwa sababu ni Polisi mwenzake ndio maana akasema hivyo.
HITIMISHO: Kwa mazingira hayo hapo juu hakuna namna ya kuvitoa vyombo vya Dola na SERIKALI kutohusika na matukio haya ya UTEKAJI hata utumie Uzi huu kutunga swali kwa watu wasio ijua TANZANIA kabisa; Waulize wakisie nani Yuko nyuma ya matukio haya ikiwa walengwa ni wanasiasa wa upinzani, wakosoaji wa Serikali, wapaza sauti na wapigania haki ya umma tu???
Watakujibu wahusika ni serikali na vyombo vyake vya Dola😁
SULUHISHO: iundwe idara ya Usalama wa raia na upelelezi ambayo haita fungamana ama kuwajibika moja kwa moja kwa serikali.
Idara hiyo isiwe chini ya wizara yoyote Ile ya Serikali maana kuna ripoti maelfu kwa maelfu za tume mbalimbali na tafiti zimekaliwa wizarani haijawahi kumfanyiwa kazi wala kufunguliwa kesi kupata haki ya waathirika.
Idara ya upelelezi itakayoundwa isiwe chini ya jeshi lolote wala isiwe chini ya DPP kwa sababu hao wote aidha wamewahi kushutumiwa kwa namna moja au nyingine au wamekalia maelfu kwa maelfu ya majalada ya upelelezi.
IDARA YA USALAMA WA RAIA NA UPELELEZI ninayo ipendekeza iundwe chini ya mahakama na upelelezi utakaofanyika na matokeo yake uwasilishwe kwenye usikilizwaji rasmi wa kesi na si kwa hakimu wala Jaji yeyote. Kwa sababu upelelezi wowote unafanyika ni kwa kusudi la kuujua ukweli ili haki itendeke ( na chombo Cha kutoa Haki ni MAHAKAMA tu) na si kwa ajili ya uteuzi au utenguzi.