Afrika itaweza kuoiga hatua pale wazungu na mataifa yanayojiita makubwa watakapoacha kujidai wanaipa misaada au kuisaidia. Wakituacha miaka mi5 tu complete bila kutuingilia kabisa kwa namna yoyote, mtashangaa msingi imaea utakaojengwa.
Shida zinafanya watu wawe imara na kupiga hatua. Utegemezi unadumaza. China ilikataa utegemezi wakazaa kwa wingi lakini leo hii shuda ziliwafundisha maisha, wapo mbali sana.
Adui mkubwa wa mwafrika ni huyu mzungu asiyetaka mwafrika ajitegemee. Watuache tupate shida, kama ni kufa tufe, hatutaisha wote. Lakini hizo shida ndo zitatufanya tuumize vichwa na kuibuka na suluhisho la dizaini ya kwetu, narudia tena dizaini ya kwetu sio lazima suluhisho liwe katika mfumo wa kwao ao liwe kama la kwao.
Tumekuwa nyuma katika teknolojia, tiba, n.k kwa sababu ya kuletewa magonjwa na kulazimishwa tiba zao. Sio kwamba waafrika hatuna akili ya kutengeneza madawa tukajitibu wenyewe, ni kwa sababu wanatuletea madawa na wanatuaminisha kuwa madawa ni yale wanayoleta wao, ya kwetu ni upuuzi na hayawezi. Well, hata kama hayawezi kama ya kwao ila kama ya kwao yasingekuwepo tungeshagundua yanayotibu zaidi ya hayo ya kwao.
Imekuja covid, wangetuacha tu sisi wenyewe tupambane nayo waone. Ndani ya mwaka tu tayari Afrika ingekuwa imeshapata dawa tiba na kinga yake yenyrwe kwa dawa zake za asili (narudia tena sio lazima suluhisho letu liwe sawa na la kwao). Ni sawa tungeanza na dawa zenye uwezo mdogo kama tulizoanza nazo, ila baada ya muda tungegundua zenye uwezo mkubwa au kuboresha zile za mwanzo na kupata dawa zenye uwezo mkubwa sana. Ila angalia wanachofanya wazungu, wanaitumia WHO kuhakikisha dawa zote zisipewe kipaumbele kama sio zile zilizotengenezwa kwao.
Nawaambia tena waafrika wenzangu, waafrika sio kwamba hatuna akili kama mnavyokaririshwa na wala sio kwamba Afrika ina laana, hapana. Adui yetu mkubwa ni mkoloni wetu anayeendelea kuhakikisha hatujitegemei mpaka leo. Na amefanikiwa kututengeneza akili hadi tunajilaumu wenyewe na kulaumiana sisi wenyewe kwa wenyewe kuwa sisi ndio chanzo ila kiukweli mkoloni alianza kutywekea utumwa ndani ya vichwa vyetu kupitia dini, elimu, mifumo ya siasa, n.k. kilichobaki tunajiendesha wenyewe kujiharibia kwa manufaa ya mkoloni.
Kuzaa watoto wengi haijawahi kuwa sababu ya umaskini, bali ni sababu ya utajiri. Nchi zenye watu wengi kama watatengenezwa vuzuri ndio zinakuwa tajiri, angalia mfano Marekani, China, India, Nigeria, n.k. Ila mzungu ametuletea utumwa wa kutwambia kuzaa ni mwanzo wa umaskini ili tuache kuzaa tusipige hatua na mwisho wa siku tupungue na kuisha.
Shtuka mwafrika