Je, Waajiri wanatimiza sehemu yao kuhakikisha akina mama wanapata muda wa kunyonyesha wawapo kazini?

Je, Waajiri wanatimiza sehemu yao kuhakikisha akina mama wanapata muda wa kunyonyesha wawapo kazini?

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Joined
Aug 7, 2018
Posts
685
Reaction score
1,124
Je, Wajua unyonyeshaji ukifanyika ipasavyo, uwezekano wa Mtoto kupata Magonjwa hatari ya kuambukizwa au kuugua mara kwa mara hupungua na hivyo kupunguza Vifo vya Watoto?

Hata hivyo, tafiti mbalimbali zinaonesha baadhi ya Wanawake wanaonyonyesha wakiwa katika ajira wamekuwa wakishindwa kunyonyesha kila inapohitajika kutokana na kubanwa na Mazingira, ratiba au majukumu yao.

KINGA KUNYONYA.jpg

Kufahamu zaidi kuhusu Haki za Akina Mama Wanaonyonyesha wakiwa katika Ajira na Wajibu wa Waajiri, Shiriki katika Mjadala na Wataalamu wa Masuala ya Uzazi na Sheria, Agosti 7, 2024 kuanzia Saa 12:00 Jioni hadi Saa 2 Usiku kupitia XSpaces ya JamiiForums

Kushiriki Mjadala x.com

=======

Mjadala umeanza ambapo afisa programu wa Jamiiforums, David Magobeko alikaribisha waliojiunga na kuwatambulisha wachangiaji na Dkt. Mariam Nooran anaanza.

Dkt. Mariam Noorani (Daktari wa Watoto/Mtaalamu wa Unyonyeshaji - Aga Khan Hospitali): Tunapoongelea faida za Unyonyeshaji tunaongelea faida kwa jamii, kwa Mama, Mtoto na Kwa Nchi

Lakini nataka kuongelea faida za Unyonyeshaji kwa Mtoto

Unyonyeshaji wa Watoto hasa kwa Miezi 6 ya mwanzo una faida nyingi kwa mtoto

Kubwa zaidi ni kusaidia ukuaji wake na kumlinda dhidi ya Magonjwa kama Pumu na Magonjwa ya Ngozi

Mercy-Grace Seuya: Mwakilishi Chama cha Waajiri Tanzania (ATE): Waajiri wana nafasi kubwa sana katika malezi ya mtoto kabla hata hajazaliwa

Na ni wajibu wao kufuata Sheria zinazowaruhusu Wazazi kupata muda wa kunyonyesha Watoto

Mwajiri ana uwezo wa kutunga sera rafiki zitakazo mwezesha Mama kuweza kunyonyesha Vizuri

Mfano; kuna Ofisi ambazo zimetenga Maeneo maalum ya faragha ili kunyonyesha au kumwezesha Mama kukamua Maziwa kwa ajili ya Mtoto

Mary Yunge (Mwakilishi TUGHE): Lazima tufahamu kuwa kuna Sheria zinatuongoza Kazi

Mfanyakazi anapokosa likizo ya kunyonyesha anaweza kutoa Malalamiko katika Chama cha Wafanyakazi kilichopo katika eneo lake la kazi

Kwasababu moja ya sababu za kuanzishwa kwa Vyama vya Wafanyakazi ni kuhakikisha mazingira bora ya kazi.

Ni vizuri kuwa na Maxingira mazuri ya ushirikishwaji kati ya Waajiri na Wafanyakazi wa namna gani Wafanyakazi wanaonyonyesha waweze kupata nafasi

Kwasababu Mfanyakazi anayeyonyesha asipokutana na changamoto, utendaji kazi wake unakuwa hauathiriki hivyo ni faida kwa Kampuni.

Muhimu zaidi ni Elimu

Elimu iendelee kutolewa kwa Wafanyakazi waweze kuzifahamu haki zao zikiwemo za kunyonyesha

Pia Elimu itolewe ili Waaajiri na Wafanyakazi waweze kukaa pamoja na kupanga namna bora zaidi ya kurahisisha Mchakato wa Unyonyeshaji kwa Waajiriwa Wanaonyonyesha.

Kwa Mtumishi anayekuwa ameshindwa kunyonyesha vizuri kutokana na kazi yake na ana malalamiko anaweza kuwasilisha Malalamiko yake kwa Kamishna wa Kazi pia Kamati ya Usuluhishi (CMA)

Huko Sheria itatumika ambapo Shauri lake litashughulikiwa pasipo kuathiri ajira ya Mlalamikaji.

Dkt. Haika Malik (Mwakilishi Chama cha Madaktari wa Watoto Tanzania): Waajiri wanasema bado hawajaona Waraka wa Mabadiliko ya Sheria mfano; Likizo ya Mama aliyejifungua Mtoto Njiti

Kwa hiyo ni jukumu letu Wadau kutoa elimu ili kuhakikisha Mama anapata na anatumia haki yake ya kunyonyesha.

Mary Yunge: Chama chetu cha Wafanyakazi (TUGHE) huwa tunapokea Maoni na Ushauri kutoka kwa Wafanyakazi kuhusu unyinyeshaji

Kwa mfano suala la likizo ya Mama aliyejifungua Mtoto njiti, ni suala ambalo tumelipokea kwa muda mrefu

Sasa Mama akijifungua Mtoto njiti analazimika kukaa Hospitali muda mrefu, na hadi akitoka unakuta zile siku 84 zimeisha

Lakini Mei Mosi hili suala lilipata Ufumbuzi

Elimu itolewe kwa Waajiri kuhusu haki na Umuhimu wa Waajiriwa Kunyonyesha

Lakini pia Waajiriwa wapewe elimu ya haki zao za Kunyonyesha

Wakizijua haki zao ni rahisi kutambua zikivunjwa

Mercy-Grace Seuya: Sisi kama Chama cha Waajiri tunafanya kazi kubwa katika Kutoa Elimu kwa Waajiri na Waajiriwa

Pia katika Kila Ofisi ni muhimu kuwa na Sera ya Rasilimali watu. Na ni takwa la kisheria

Sera hii inatoa Mwongozo wa haki na wajibu wa Mwajiri na mwajiriwa. Inaeleza huyu asipofanya nini afanye nini.

Mwakilishi Chama cha Waajiri Tanzania (ATE): Tamko kutoka kwa Makamu wa Rais kuhusu likizo ya Mama anayejifungua Mtoto njiti bado ni tamko, bado halijawa sheria

Ni kweli ni tamko kubwa lakini linatoa gurudumu la utunzi wa Sheria kuhusiana na hilo.

Dkt. Haika Malik: Mama na Mtoto njiti huwa wanakuwa wanakaa Hospitali kwa muda mrefu zaidi kwa sababu wanahitaji uangalizi na ufuatiliaji wa karibu zaidi

Na wakiweza kunyonyeshwa vizuri tafiti zimeonesha inaweza kupunguza muda wa kukaa hospitali

Changamoto kubwa katika Hospitali za Umma hazina nafasi ya kumruhusu Mama kulala na Mwanae aliye njiti

Mama analazimika kutembea kutoka Wodi moja kwenda kwenye wodi ya Mtoto ili kumyonyesha

Hiyo inasababisha mama anakuwa hapumziki. Unakuta usiku kucha anaamka kutembea kwenda kunyonyesha.

Katika Hospitali nyingine wamewasaidia Wakina Mama kwa kuweka Friji Wodini

Yaani Mama anakuwa anakamua Maziwa yanahifadhiwa kwenye friji na mtoto akihitaji anapelekewa , japokuwa hii inategemea na ukubwa wa Mtoto

Njia hii inamsaidia Mama kupumzika kidogo, kutembea tembea kuna pungua.

Idda Katigula (Mtaalam wa Lishe na Mwanzilishi wa Shirika la Unyonyeshaji la JJ): Wakina mama wengi ambao wamejiajiri au wameajiriwa wamekutana na changamoto mbalimbali

Moja ni ukosefu wa elimu ya Ukamuaji wa Maziwa, hii inaenda hadi kwa Wenza na watu wanaomzunguka.

Unakuta Mama amekamua Maziwa kwa mujibu wa Maelekezo ya Wataalamu wa Afya lakini watu wanaomzunguka hawayaamini

Yaani unakuta Wifi, au Mama Mkwe haamini Maziwa yalikamuliwa na wanaona hayana umuhimu au virutubisho. Jambo ambalo sio la kweli.
 
Je Wajua unyonyeshaji ukifanyika ipasavyo, uwezekano wa Mtoto kupata Magonjwa hatari ya kuambukizwa au kuugua mara kwa mara hupungua na hivyo kupunguza Vifo vya Watoto?

Hata hivyo, tafiti mbalimbali zinaonesha baadhi ya Wanawake wanaonyonyesha wakiwa katika ajira wamekuwa wakishindwa kunyonyesha kila inapohitajika kutokana na kubanwa na Mazingira, ratiba au majukumu yao

Kufahamu zaidi kuhusu Haki za Akina Mama Wanaonyonyesha wakiwa katika Ajira na Wajibu wa Waajiri, Shiriki katika Mjadala na Wataalamu wa Masuala ya Uzazi na Sheria, Agosti 7, 2024 kuanzia Saa 12:00 Jioni hadi Saa 2 Usiku kupitia XSpaces ya JamiiForums

Kushiriki Mjadala x.com
Waajiri hawazingatii hilo
 
Je Wajua unyonyeshaji ukifanyika ipasavyo, uwezekano wa Mtoto kupata Magonjwa hatari ya kuambukizwa au kuugua mara kwa mara hupungua na hivyo kupunguza Vifo vya Watoto?

Hata hivyo, tafiti mbalimbali zinaonesha baadhi ya Wanawake wanaonyonyesha wakiwa katika ajira wamekuwa wakishindwa kunyonyesha kila inapohitajika kutokana na kubanwa na Mazingira, ratiba au majukumu yao

Kufahamu zaidi kuhusu Haki za Akina Mama Wanaonyonyesha wakiwa katika Ajira na Wajibu wa Waajiri, Shiriki katika Mjadala na Wataalamu wa Masuala ya Uzazi na Sheria, Agosti 7, 2024 kuanzia Saa 12:00 Jioni hadi Saa 2 Usiku kupitia XSpaces ya JamiiForums

Kushiriki Mjadala x.com
mbona sheria ipo wazi
anakaa nyumbani miezi mitatu
kisha akirudi kazini, kila siku anapewa masaa mawili KWENDA kunyonyesha hadi mieZI 6
 
Wanateseka mno!!! Workplace ya Tanzania haizingattii kuwa mwanamke anatakiwa kuwa na familia wengi wakifikia uzazi ubabaifu mwingii hujitokeza
 
Kampuni nyingi sana hazizingatii, wanachojali ni kazi zao zifanyike mpaka ziishe. Kuna kampuni moja ya Microfinance, kwao hata mtu alie omba muda wa kwenda kunyonyesha hapewi ni marejesho tu
 
Back
Top Bottom