MALCOM LUMUMBA
JF-Expert Member
- Jul 26, 2012
- 21,113
- 65,124
Habari za jumapili,
Naomba leo tupeane changamoto za kihistoria na kitamaduni ambazo zimejengeka kwetu. Iko hivi, ramani za zamani hata kabla ya kuzaliwa Kristo zinaonyesha (BC) zinaonyesha kwamba bahari ya atlantiki iliitwa Bahari ya Ethiopia. Wanahistoria wa kale wa Kigiriki waliita kwa jina la Okeanus Aithiopos na wale wa waroma kwa lugha ya kilatini waliita Oceanus Ethiopicus. Wanasema bahari hii iliunganisha ustaarabu wa watu weusi (Ethiopians) waliokuwa barani Afrika na barani Amerika.
Nini kilitokea hadi bahari ikabadilishwa jina, mimi sitasema chochote kile wala sintatoa nadharia. Lakini nitakachokisema na kuuliza ni hiki tu: Kama majina makubwa yenye umuhimu mkubwa wa kihistoria yalibadilishwa ni mambo mangapi yenye umuhimu wa kihistoria yatakuwa yamebadilishwa kuhusu dunia hii.
Naambatanisha ramani ya mwanajeographia wa zamani wa Marekani aitwaye Mathew Carey ambaye alifanya kazi kubwa ya kuandaa ramani mbali mbali za dunia mnamo miaka ya 1700's. Ukingalia kwa umakini jina la Bahari ya Atlantiki ilikuwa ni Oceanus Ethiopicus. Chanzo cha ramani hii The Library of the Congress ya Marekani. Hivyo ni moja ya chanzo cha kuaminika sana na kinathibitisha uhalisia kwa kielelezo cha ramani ya pili....
Hii ya pili ni ya miaka ya nyuma kidogo kabla hata ya haya mataifa ya Ulaya hayajafanya hata mapinduzi ya viwanda. Jina la Bahari hapa tena ni Oceanus Ethiopicus