Je, Wajua Barabara iliyopewa jina la Sam Nujoma inamuenzi mpigania uhuru wa nchi ya Namibia?

Je, Wajua Barabara iliyopewa jina la Sam Nujoma inamuenzi mpigania uhuru wa nchi ya Namibia?

neym8990a

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2017
Posts
244
Reaction score
196
Barabara inayotoka Mwenge kuanzia kwenye makutano ya barabara ya Bagamoyo inaitwa bara bara ya Sam Nujoma (Sam Nujoma road). Hili ni jina lililotOlewa kuenzi harakati za mpigania Uhuru na rais wa kwanza wa Namibia, Samweli Nujoma. Miaka ya 1960, sehemu kubwa ya bara la Afrika lilikua kwe-nye joto kubwa la harakati za Uhuru.

Harakati hizo zilizotapakaa karibu pembe zote za bara hili likazaa majina makubwa yaliyoacha alama kama Muham-mad Anwar El Saadat, Kwame Nkuruma, Julius Kambarage Nyerere, Steven Biko, Abraham Tito, Samora Machel, Patrice Lumumba, Joseph Kasavubu, Andimba Toivo ya Toivo na wengine wengi akiwemo Sam Nujoma aliyezaliwa Mei 12,1929 kijijini kwao Ongand-jera, mji wa Etunda mkoa wa Omusat kaskazini Magharibi mwa Namibia.

Eneo alilozaliwa linajulikana kama “Ovambo” likimaanisha ardhi. Ni mtoto wa kwanza kati ya watoto 11 wa mkulima na mfu-gaji Daniel Utoni Nujoma na kwa mkewe Helvi Mpingana Kondombolo. Alisoma shule ya misheni ya Okahao mpaka dar-asa la sita ambayo kwa wakati huo ilikua elimu ya juu. Jina hili alipewa kutokana wakati anazaliwa Namibia ni kipindi ambacho nchi hiyo ili-kua chini kipindi cha ukoloni mpya wa Uingireza toka kwa Mjerumani baada ya vita vya kwanza vya dunia.

Mwaka 1949 Nujoma alik-wenda kuishi Windhoek kwa mjomba wake Hiskia Kondom-bolo. Akiwa Windhoek alianza kufanya kazi katika shirika la reli la Afrika ya kusini (South African Railway-SAR). Akiwa anafanya kazi mchana usiku ali-kua anaingia darasani kusoma St. Barnabas hapo hapo Wind-hoek..Mwaka 1957 alifukuzwa kazini kutokana na tabia yake ya kupigania haki za wafanyakazi wa shirika la reli alilokua akifanyika kazi. Kufukuzwa huku kulitokana pia na lengo lake la kutaka kuanzisha umoja wa wafanyakazi wa reliBaada ya kufukuzwa kazi, alijitumbukiza rasm kwenye siasa, kwa kushirikiana na Chief Hosea Kutako, Samuel Witbooi, Theophilus Hamutumbangela, Toivo ya Toivo na wengine walianzisha chama cha Ovam-boland People’s Congress.

Mwaka mwaka 1959 walian-zisha chama kingine tena cha Ovamboland People’s Organi-zation na kuchaguliwa kua kiongozi wa chama hiko, mwaka 1960 alishiriki kuanzisha chama kilichoipa uhuru nchi hiyo cha Ukombozi wa Umma wa Afrika ya kusini Magharibi, SWAPO na kuchaguliwa kua mwenyekiti wa chama hiko. Akiwa kiongozi wa SWAPO alifanikisha Na-MAKALA SAMWELI SHAFIIHUNA NUJOMA- “SAM NUJOMA” baba wa Demokrasia Namibia kupigania haki za wafanyakaziwa shirika la reli alilokua akipgyg-fanyika kazi.Kufukuzwa huku kuchaguliwakuamwenyekiwa chama hiko.Akiwa kiongozgygwa SWAPO alifanikisha Nagmibia kujitenga kutoka Afrika kusini na kua nchi huru mwaka 1990.Nujoma aliyeungwa mkono† na mataifa mbalimbali pamoja taaisisi kikiwemo chama cha kikomunisti cha china na jeshi la ukombozi wa umma wa chi-na chini ya Mao Zedong na Bw. Zhou Enlai.k

Alifika Tanganyika kwa mara ya kwanza mwaka 1960 akiwakimbia wakoloni. Alitoroka toka Namibia hadi Tanganyika kutafuta hifadhi baada ya kushtakiwa kusababi-sha vurugu

Safari hii iliyomgharimu zaidi ya siku sitini (miezi miwili)ilikua ni ya shida sana akitumia ndege, treni,magari na hata kwa miguu akipita Botwsana ya leo (Zamani Bechuana land), Zimbabwe ya leo (zamani Rhodesia ya kusini), kisha Zambia ya leo (zamani Rhodesi ya kaskazini, Kongo Tanganyika.

Akiwa Tanganyika watu wa TANU walimficha mjini Mbeya kisha walimsafirisha kwa siri hadi Dar -es-Salaam alipokutana na Nyerere. Akiwa Dar es-Salaam kwa msaada wa Nyerere alipata nafasi ya kuzungumza na kamati maalum ya umoja wa mataifa New York nchini Marekani. Ilipoundwa kamati ya ukombozi wa iliyokuwa umoja wa nchi huru Afrika (OAU) mwaka 1963, Tanzania ikawa kituo cha wapigania Uhuru na mafunzo ya kijeshi. Alikua miongoni mwa wapigania uhuru waliojiunga na jeshi lilioweka kambi Kongwa mkoani Dodoma. Akiwa Kongwa Dodoma Tanganyika. Akiwa Kongwa alijifunza tamaduni mbali mbali za kabila la kigogo ikiwemo lugha ya kabila hilo.

Agosti 26, 1966 Nujoma ali-fanikiwa kuingiza mzigo wa kwanza wa silaha Namibia zilizotoka Algeria zikapitia Misri, Sudan, Tanzani Zambia na kisha kuingia nchini humo katika mji wa Uukwaluudhi mkoa wa Umusati na kuwa mwanzo rasmi wa mapigano ya ukombozi wa nchi hiyo.Tukio hilo la kuingiza silaha kwa mara ya kwanza nchini humo mpaka limebatizwa siku ya mashujaa (Heros’Day Agust 26). Mapigano hayo yalianza baada ya askari wa kikoloni kuwavamia wanaharakati wa SWAPO siku hiyo hiyo silaha zilipoingia nchini humo wakiwa kwenye kambi yao ya Omugulugwombashe.Mapigano hayo yalidumu kwa miaka 25 hadi mwaka 1971. Mwaka 1971 Nujoma alipohutubia baraza kuu la Usalama la Umoja wa mataifa mjini New York Marekani. Kupitia hotuba hiyo Swapo ilitambulika rasmi na baraza hilo na ukawa mwisho wa vita hivyo ingawa hakurudi nchini kwake.

September 1989 alirudi nchini Namibia rasmi baada ya miaka 29 ya kuishi uhamishoni. Na Machi 21 alitangazwa rasmi kuwa rais wa nchi hiyo kufua-tia uchaguzi uliofanyika nchini humo.

Nujoma alistaafu rasmi urasi wa Namibia machi 21, 2005 na alimpisha Rais Hifikepunye Pohamba na kisha kuachia nafasi yake ya uongozi wa chama cha SWAPO Novemba 30, 2007.

1547127775481.png
 
Yaah ndiyo ile inatoka mwenge inakuja mpaka Ubungo mataa
 
Back
Top Bottom