Je, wajua Dubai ililipa gram 2 za dhahabu kwa kila anayepunguza kg1 ya uzito wake

Je, wajua Dubai ililipa gram 2 za dhahabu kwa kila anayepunguza kg1 ya uzito wake

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Dubai ni mji ambao na matatizo ya wakazi wake wengi kuwa na uzito ulipitiliza ambapo katika kukabiliana na tatizo hilo wakaja na sera ya Uzito wako katika dhahabu.

Sera ilitaka mtu apunguze uzito kuanzia Kilogram moja ndani ya siku thelathini ambapo kila anayefanikiwa anapata gram mbili za dhahabu, aidha mtu akipungua uzto zaidi ya hapo dhahabu ziliongezeka.

Lilikuwa kama shindano na halikuwa na ukomo wa uzito ambao unapaswa kupunguza. Wataalamu wa Dubai waliamini kuwa hakuna kitu kinachochoma mafuta kwa haraka kama pesa. Ndio sababu walishauri njia hiyo.

Sera hiyo ilitekelezwa kwa siku 30 kuanzia Julai 17 hadi Agosti 16 mwaka 2013 na liliwahusu wakazi wa Dubai pekee
 
'Lilikuwa kama shindano na halikuwa na ukomo wa uzito ambao unapaswa kupunguza. Wataalamu wa Dubai waliamini kuwa hakuna kitu kinachochoma mafuta kwa haraka kama pesa. Ndio sababu walishauri njia hiyo'

Sijaelewa kitu hapo
 
Hakuna kitu umeongea, kwa vile lilitolewa na wataalamu basi data za mafanikio, kufeli na kiasi chake zipo. Kwenye uzi ziko wapi
 
'Lilikuwa kama shindano na halikuwa na ukomo wa uzito ambao unapaswa kupunguza. Wataalamu wa Dubai waliamini kuwa hakuna kitu kinachochoma mafuta kwa haraka kama pesa. Ndio sababu walishauri njia hiyo'

Sijaelewa kitu hapo
Kuna jamaa mmoja anaitwa Isac Ndodi alikua na kampeni ya kupinga vitambi na alikia anauza dawa zake za kijanja janja kupunguza vitambi.

Ajabu sasa ana bonge la mkitambi.😅😅
Kweli wajinga ndo waliwao
 
'Lilikuwa kama shindano na halikuwa na ukomo wa uzito ambao unapaswa kupunguza. Wataalamu wa Dubai waliamini kuwa hakuna kitu kinachochoma mafuta kwa haraka kama pesa. Ndio sababu walishauri njia hiyo'

Sijaelewa kitu hapo
Kichwa maji huwezi kuelewa
Nenda kajadili mambo ya ccm haya magumu huyawezi
 
Kusudio la mleta uzi ni hiyo mbinu iliyotumika sio matokeo faida wala hasara
Hapo utakuwa umelewa au vipi
Ambacho sikuelewa ni hii sentensi, ' hakuna kitu kinachoma mafuta kwa haraka kama pesa'.
 
Ambacho sikuelewa ni hii sentensi, ' hakuna kitu kinachoma mafuta kwa haraka kama pesa'
Hata mie sijaelewa,
Labda angeandika 'hakuna kitu kinachoma mafuta kwa haraka kama dhahabu' labda tungeelewa,
Nadhani Ametumia balagha ya juu kidogo
 
Back
Top Bottom