Je, wajua hili kuhusu Zidane?

DIDAS TUMAINI

JF-Expert Member
Joined
Nov 11, 2014
Posts
242
Reaction score
676
Katika michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2006 nchini Ujerumani, mechi kati ya Ufaransa na Korea kusini iliisha kwa sare ya 1-1. Mechi hii ilichezwa katika uwanja wa timu ya RB Leipzing (Leipzing Arena) timu inayoshiriki ligi kuu nchini Ujerumani Bundesliga.

Kitendo cha timu ya Ufaransa kutoa sare ya 1-1 na timu ya Korea Kusini kilimkera sana gwiji Zinadine Zidane na kwa hasira kali alipiga TEKE mlango wa chumba cha kubadilishia nguo (dressing room).

Meno ya viatu vya zidene yaliacha alama kwenye ule mlango. Lakini kwa mshangao, management ya uwanja wa Leipzing hawakufanya UKARABATI kwenye ule mlango na kinyuma chake walipazungushia eneo lile frame ya GOLD na kulifanya kuwa sehemu ya MAKUMBUSHO ndani ya Leipzing Arena.

Na mpaka leo hii eneo lile ni sehemu ya kivutio katika uwanja wa Leipzing.

Legend never Die.

Didas Tumaini
 
Anaitwa Zinedine yazid Zidane zizzou, babu kipara, akili mingi kichwani mpaka mguuni, kiumbe wa kwanza mwenye kipara lakini ana akili nyingi.. Si mnajua akili ni nywele, basi mwamba zilinyonyoka akawasikilizia na kipara ila akili zikazidi.. Mtu mpole ila ukimchanganya anakuvuruga, muulize mtoto wa kitaliano materazzi kilichomsibu, alikula ndosi moja ya kivan dame, kama anapigwa bondia mandonga ile tunamfukia na kumzika, amuulize luis enrique mwamba chupu chupu amtoe macho na pua.

Huyu kiumbe ni hatari na nusu, kiungo bora kukishuhudia..
Alikuwa anafanya mpira uonekane mchezo mwepesi, kawaponza wengi saana, kawatia saana hasara vijana wakimuona anacheza wanahisi mpira ni mwepesi kesho wanaenda kununua viatu, wakipasiwa mpira kutuliza, control ni chumba, sebule na choo chake. 😂
 
Kuna watu wakipita wapita inachukua miaka miingi kuja tena sample kama iyo.
 
...bila ya kumsahau our own JJ Okocha, naye alifanya mambo mpira wa miguu uonakane rahisi tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…