JE, WAJUA? Indira Gandhi hakuwa binti wa Mahtma Gandhi

JE, WAJUA? Indira Gandhi hakuwa binti wa Mahtma Gandhi

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2016
Posts
20,743
Reaction score
25,564
Watu wengi kwa kutokujua wamekuwa wakiamini kuwa waziri mkuu wa kwanza mwanamke wa India, Indira Gandhi alikuwa mtoto wa Baba wa Taifa la India Mahtma Gandhi. Indira hakuwa mtoto wa Gandhi bali alikuwa mtoto pekee wa waziri mkuu wa kwanza wa India, Jawaharlal Nehru na Mkewe Kamala Nehru.

Ubini wa Gandhi aliupataje?
Baada ya masomo ya awali nchini India, Indira alijiunga na chuo kikuu cha Oxford, Uingereza kati ya miaka 1930 ambapo alikutana na kijana(Kwa wakati huo) Feroze Jehangir Ghandy ambaye alikuwa anasoma London School of Economics. Hivyo wakawa marafiki wakubwa!!

Joto la harakati za kupigania uhuru lilipopanda, Feroze aliachana na masomo na kurudi India kuungana na harakati hizo. Feroze alikuwa ni mparsi(Dini) na aliamua kwa hiari yake kubadili jina lake "Ghandy" na kuwa "Gandhi" (Unaweza kujihakikishia hili kwenye kitabu India after Gandhi: kimeandikwa na Ramachandra Guha,(2011) ukurasa wa 809.

Mwaka 1941, Indira naye alirudi India bila hata ya kumaliza masomo yake. Hii ilitokana na kuumwa mara kwa mara. Lakini niliwahi kumuuliza Guha(Ni mwanahistoria mashuhuri wa India) sababu hasa akanieleza Indira alihitaji kuwa karibu na Feroze ambaye walishakuwa kwenye mahusiano.

Ilishtua mwaka 1942, Indira alipotaka kuoana na Feroze hii ni kwa kuwa Indira alikuwa ni Mhindu na Feroze ni mparsi ambao ni kikundi kidogo kabisa India. Walifanikiwa kufunga ndoa ya kihindu mwaka huo huo.

Kwa tamaduni za Kihindu, Ilimlazimu Indira Nehru kubadili ubini wake na kuwa Indira Gandhi akifuata ubini wa mumewe. Baada ya Miezi sita tu wote wawili walifungwa na serikali ya kikoloni kwa kujihusisha na Maandamano makubwa yaliyoongozwa na Mahatma Gandhi.

Baada ya uhuru, Feroze alishinda nafasi ya uwakilishi wa Rae Bareli(Kama Jimbo) mpaka mwaka 1957. Kulitokea mtafaruku kati ya Indira na Feroze wakiwa wameshapata watoto wawili Rajiv Gandhi (ambaye naye alikuja kuwa waziri mkuu wa India) na Sanjay Gandhi. Walitalikiana. Hivyo Indira alirudi kwao na kuwa msaidizi wa ofisi ya Waziri Mkuu Nehru, ambaye ni baba yake Mzazi.

Feroze alifariki kwa tatizo la moyo mwaka 1960. Kwa wakati huo Indira hakuwa anafahamika kabisa. Baada kifo cha baba yake (Nehru alifariki tarehe 26 Mei 1964), Indira aliibuka kama Waziri wa Mawasiliano na Utangazaji mwaka 1964. Haitoshi, Januari, 1966 alimshinda Desai baada ya kifo cha Shastri aliyechukua madaraka kwa Nehru.

Akiwa waziri mkuu wa India, Indira Gandhi alifanya ziara mbili za kiserikali kuitembelea Tanzania.
Ya kwanza ilikuwa kuanzia tarehe 11 mpaka 14 ya Mwezi Octoba mwaka 1976.

Ya pili ilikuwa tarehe 16 na 17 Aprili, 1980.

Ushahidi 2.
Wengi hudhani pia Mahatma Gandhi ni raisi wa kwanza wa India. Hapana, alikuwa ni kiongozi wa chama cha INC(Indian National Congress) na aliongoza harakati zilizoiletea uhuru India, Agosti, 1947.

Katika maisha yake yote, Mohandas Karamchand Gandhi hakuwahi kupata mtoto wa kike au Binti.
Gandhi alikuwa na watoto wanne wa kiume ambao ni…

Harilal (1888-1948) alizaliwa India,
Manilal (1892-1956) alizaliwa India,
Ramdas (1897-1969) alizaliwa Afrika ya Kusini( Gandhi aliishi huko kwa takribani miaka 21.
Devdas (1900-1957) pia alizaliwa Afrika ya Kusini.

Hivyo kwa hayo, Indira sio wa familia ya Gandhi inayofahamika zaidi.
Leo Novemba 19 ni 'birthday' ya Indira Gandhi.
______________
Maelezo ya Picha:
Indira akiwa na Mahatma Gandhi mwaka 1924. Gandhi alikuwa kwenye Mfungo.

126848944_3484494814976322_3630136201905535258_n.jpg


©Francis Daudi
 
Kenya Kenyatta... India Indira... Zanzibar Zanzibara... Tanganyika Danganyika
 
Back
Top Bottom