Madrid boy
JF-Expert Member
- May 21, 2017
- 895
- 615
Habar zenu wakuu nimatumaini yangu hamjambo.Inavyofahamika sasa jimbo la Texas lipo marekani hili jimbo ni moja ya majimbo yanayopatikana kusini mwa nchi ya Marekani limepakana na nchi ya Mexico.Hili moja ya majimbo yaleyale ya kusini yaliyokua yakitaka kuendelea kwa utumwa hata baada ya Marekani kupata uhuru chini ya Generali wao aliyejulikana kwa jina la Generali Robert E. Lee.
Mnamo October 2 1835 kabla ya vita ya Marekani (American civil war )hawa watu wanaliokua wanaishi Texas walikua wanafahamika kama wakoĺooni wa kimarekani waliokua wanakaa Texas kimabavu waliamua kushirikiana na baadhi ya Wamexico wazaliwa wa Texas waliojulikana kama (Tejanos) kuupinga utawala wa Rais Antonio Lopez de Santa Anna.Serikali ya Mexico wakati huo ilishajua ulikua ni mpango wa Marekani kujitanua kieneo kama ilivyo waasi katika mji wa Donenstky kule Ukraine mashariki ambao wanataka kujitenga kutoka serikali ya Kiev na kuwa ni jamuhuri yenye mafungamano na Urusi.
Basi serikali ya Mexico ya wakati huo ikasema itaingia vitani juu ya Mzozo wa eneo hilo Mnamo October 2 1835 vita vikaanza kati ya Mexico na Texas mpaka mwaka 1836 ambapo Mexico walishindwa katika hii vita baada ya huu ushindi Texas ikawa ni jamuhuri inayojitegemea kama ilivyo jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.Ikumbukwe wakati huu Texas haikuwa sehemu ya Marekani hata kidogo.
Rais wa Marekani wakati huo Martin Van Buren alijizuia kuinganisha Texas mapema iwe ni sehemu ya Marekani. Kwa hiyo Marekani ikawa na uhusiano wa kidiplomasia na Jamuhuri ya Texas kama taifa huru .
Rais Martin Van Buren
Mnamo mwaka 1845 rais wamarekani aliyeitwa John Tyler alianza mazungumzo ya kidiplomasia na Jamuhuri ya Texas kuinganisha iwe ni sehemu ya Marekani.Mnamo mwaka 1844 ndipo mazungumzo ya kuinganisha Texas iwe sehemu ya Marekani yalianza Mnamo mwaka 1845 chini ya Rais James k. Polk mkataba wa kuiongeza Texas iwe sehemu ya Marekani uliwekwa.
I ngawa Rais Tyler alikosa kura kutoka seneti kuhalalisha mkataba huo lakini baada ya kustaafu alijitahidi sana kuhakikisha Jamuhuri ya Texas inakua ni sehemu ya Marekani .Kwa upande Wamexico walikua hawataki kutambua kama Texas inakua tena ni sehemu ya Marekani
Rais John Tyler
NB:Nitaendelea wakuu maana ni ishu ndefu kidogo
Sent using Jamii Forums mobile app