Je wajua? Jinsi ya ku-extract Pure Gold kutoka kwenye vifaa chakavu vya electronics

Je wajua? Jinsi ya ku-extract Pure Gold kutoka kwenye vifaa chakavu vya electronics

kinegax

Member
Joined
Jan 3, 2015
Posts
13
Reaction score
21
Habari yako Mwana jukwaa mwenzangu. Rejea kichwa cha Uzi hapo juu.
Bila kupoteza mda.. Katika pitapita zangu kwenye mtandao nikakutana na hii kitu nikaona niwashirikishe wenzangu kwa akaeona inamfaa ataifanyia kazi.
Baadhi ya parts za electronics hasa Simu na motherboards za computer zimekuwa covered na gold layer. Parts hizi ni kama zifuatazo, CPU core, ram, connectors mbali mbali, line za simu, terminal za battery za Simu.
Unaweza ukaextract hii gold ukapata pure gold kupitia chemical processes mbali mbali.
Mfano: njia ya kwanza
Inaitwa nitric process:
Angalizo chemically zitumikazo ni hatari kwa afya hiyo lazima uwe na protective gears na ufanyie kwenye fume chamber au Nje.
Chemically zitumikazo, hydrochloric acid, nitric acid, salt powder, Copper solution.
- saga saga parts zako za electronics na weka kwenye container
-weka hydrochloric acid
-weka copper solution. Dhumuni ni kuitenganisha cold toka kwenye alloy yake yenye copper na nickel
- acha mchanganyo wako kwa siku saba
-chuja kwa kutumia filter paper
-utapata mchaga wa gold
-then chukua mchanga huo weka kwenye beaker changanya na vipande vidogo vya filter pepa
- weka tena hydrochloric acid
-then weka nytric acid , changanya vizuri.
- chuja vizuri mchanganyo wako kupata gold solution.
- then weka salt powder mpaka upate tope.
- chemsha tope hilo mpaka upate gold powder
- peleka kwenye furnace choma gold powder kupata myeyusho wako wa pure gold ambao unaweza kuushape unavyotaka ww.
Huu ni mfano wa laboratory. Lakini kuna viwanda vikubwa huko Nje wanavuna gold kwa njia hii na kuuza kwa pesa ndefu. Inawezekana hata chain au Pete unayovaa imetokana kwa njia hii.
Kwa kwenye mitaji mikubwa wanaweza kuwekeza kwenye biashara hii kwani hata kiwanda chake hakigharimu pesa nyingi sana.
Kwa anayefaham zaidi anaweza akatufahamisha zaidi...
Pia si gold peke yake hata silver unaweza kuextract.
Kazi kwako kufuatilia zaidi na kuandalia mchanganuo.. Asanteni
 
Changamoto ipo kwenye kupata izo parts za electronics za kutosha ambazo unaweza kusaga lkn kifaa cha kusagia ambacho kitapunguza upotevu wakati wa kusaga, Thanks anyway kwa elimu!
 
dasi besi haiitaji vifaa mechanized vya kusagia.. Unaweza kuvunja hata kwa nyundo.. Ni kidogo tu. Pia kila kitu kina changamoto kutoka ni kukabiliana na hizo changamoto
Unaweza kucheki video pia hapa kwa uelewa zaidi
 
Back
Top Bottom