Je, wajua kuhusu manukato, uturi na marashi?

Je, wajua kuhusu manukato, uturi na marashi?

Joined
Aug 5, 2017
Posts
15
Reaction score
11
Je, wajua kuhusu marashi, pafyume, uturi na manukato?

MARASHI ni vitu vyenye manukato vinavotumika kuandaa perfume km vile maua, matunda, majani nk.

PERFUME ni kimiminika kilichoandaliwa kutokana na marashi

Kuna aina tatu za perfume
1. Eau de Cologne na Eau de toilette, hizi ni kiwango cha chini cha manukato na huisha haraka, zina 7%-10% ya marashi

2. Eau de parfum, hii ina manukato ya wastani na hudumu kiasi, ina 15%-20% ya marashi

3. Parfum, hii baba lao ya zote izo. Ni ghali sana na ina manukato kiwango cha juu, kwa kawaida ni mfumo wa mafuta ina karibu 40% ya marashi. Ni nzuri sababu hudumu na kutoa manukato kwa muda mrefu hata baada ya kufua nguo.

UTURI hatua/kiwango cha pafyum yaani uturi wa kwanza/juu (Parfum), uturi wa kati (Eau de parfum) na uturi wa mwisho (Eau de Cologne na Eau de toilette)

MANUKATO ni harufu ya kunukia ya perfume au marashi. Mfano shampoo, poda au sabuni zina manukato lakini sio perfume.
 
Saafi sana. Unazo za kiasili? Yaani za kienyeji sio zilizopita kiwandani?
ni perume za kiwandani ila CONCENTRATED PERFUME OIL yaani haijapunguzwa ubora wake
hivo ziko ghali nami nafanya kupima pia ku design kwa kuchanganya kua na manukato ya kipekee
 
ni perume za kiwandani ila CONCENTRATED PERFUME OIL yaani haijapunguzwa ubora wake
hivo ziko ghali nami nafanya kupima pia ku design kwa kuchanganya kua na manukato ya kipekee
Makusudio yangu ni zile wanazotengeneza mabibi wa mashambani (sijui kama ni kweli lakini)
 
IMG_1222.jpg
[emoji106][emoji106]
 
Elimu nzuri maana wengi huwa hatuijui kutofautisha ili mradi iko kwenye kichupa na inatoa harufu kanyaga twende.
 
Mkuu, kwa wastani unatumia perfume aina ngapi kwa siku?
Mara nyingi moja au mbili tu, asubuhi moja na jioni moja. Siku nyingine moja tu.

Halafu nyingine zinaenda kwa msimu, Winter, Spring, Summer, Fall.

Nyingine za jioni na usiku, nyingine za mchana.

Nyingine za kwenda kwenye shughuli rasmi, nyingine za kushindia kila siku na kwendea kazini (mostly eau de toilette).

Nyingine nimejipiga mara moja tu nikaziweka bench.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom