Je, wajua kuwa licha ya kuwa manukato pafyumu zina faida kadhaa kimwili ikiwa ni pamoja na tiba?

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Je wajua kuwa licha ya kuwa manukato/uturi, pafyumu (perfumes) zina faida kadhaa kimwili ikiwa ni pamoja na tiba? Fahamu faida 8 za pafyumu

1. Ni tiba ya kutumia harufu (aromatherapy)

2. Harufu za baadhi ya pafyumu husaidia kupunguza maumivu ya kichwa

3. Yaweza kusaidia tatizo la kukosa usingizi

4. Huibua hisia (mood) kama vile ya kwenda kwenye pati, mtoko, kideti, nk

5. Huleta kumbukumbu ya matukio flani (mfano ulienda kideti kisha flani akakusifia kuwa umejipulizia pafyumu nzuri)

6. Harufu nzuri ya pafyumu humfanya hata mtu mwenye sura mbaya kuonekana mzuri...angalau kifikra

7. Huongeza kujiamini

8. Hufanya mwili unukie vizuri (zana muhimu sana kwa wenye "vikwapa."
 
Haswaaaa. Hapo umenena mkuu. Ila kuna madem sijui ni kipato au ushamba? Ukipishana nae utafikiri umepishana na kuli yaani harufu yake inaweza kuzalisha umeme.
 
Na inasababisha magonjwa ya kwenye mfumo wa hewa. Mfano pumu, kikohozi kikavu na pia ni mbaya kwa wenye allergy...
Anyway mi mwenyewe natumia manukato ila si nikiwa home kwa kuwa kuna watoto wadogo..
 
Na inasababisha magonjwa ya kwenye mfumo wa hewa. Mfano pumu, kikohozi kikavu na pia ni mbaya kwa wenye allergy...
Anyway mi mwenyewe natumia manukato ila si nikiwa home kwa kuwa kuna watoto wadogo..
Jaribu kutumia zenye harufu isiyo kali.
 
UNYUNYU una siri moja.

Wewe uliejipulizia UNYUNYU unaweza ukaona kama huu UNYUNYU sio mkali, kumbe wala si hivyo. Ni kwasababu PUA zako zimeshauzoea.

Wanaopata habari ya UNYUNYU wako uliojipulizia ni wale watakaokuwa karibu nawe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…