Salaam, Shalom.
Tanzania kuibeba Dunia, Hilo tu tayari ni HOJA fikirishi.
Kabla sijaenda ninakotaka kuelezea, ZIFUATAZO, ni sifa za Nchi hii ambazo, huwezi kuzipata Mahali pengine popote duniani katika macho ya kibinadamu katika Ulimwengu wa mwili.
1. AMANI
Pamoja na Nchi hii kuwa na makabila mengi kuliko Nchi nyingine yoyote duniani, Bado watu wa Nchi hii wameendelea kuishi kwa Amani.
2. UPENDO
Pamoja na tofauti za kiimani ,kitamaduni, nk nk,Bado Nchi hii unaweza kwenda popote na kupokelewa na yeyote popote na kukarimiwa.
3. UTAJIRI
Amini usiamini, Kuna watu wanasema kuwa congo ndiyo inayoongiza Kwa utajiri chini ya ardhi, Si Kweli, vilivyomo chini ya ardhi ya nchi hii, ambavyo havijavumbuliwa Bado, hakuna kama Tanzania.
4. UTULIVU
Mtanzania unaweza kumfananisha na Kondoo, Kwa nje ni kama dharau, lakini Kwa ndani ni silaha kubwa sana ya kulifanya Taifa kuwa hapa lilipo. Hata anapofanyiwa ubaya, hutulia, hata ukimdhulumu atanyamaza, na hata akiamua kufuatilia katika vyombo vya HAKI, ni Rahisi kusamehe na kumwachia Mungu.
5,6,7.......
Pamoja na sifa nyingi zinazoonekana Kwa macho, msingi wa Tanzania uko katika Ulimwengu usioonekana, na ndiko nitakapojikita zaidi.
Taifa hili, kama Kuna Nchi ambayo Mungu anaangalia Kwa ukaribu duniani baada ya Israel ni Tanzania.
Baada ya Messiah kuja duniani katika mwili wa mwanadamu, Alianza kuhubiri INJILI katika Israel, na akateua mitume, wanafunzi kuhubiri INJILI duniani kote,
INJILI hiyo imehubiriwa katika mataifa mbalimbali Kwa njia ngumu sana, wengi wa wanafunzi wa Yesu na wapeleka INJILI waliuawa na kukataliwa, na Kwakuwa, INJILI wanayoihubiri asili yake ni mbinguni, Dunia haikuipokea Wala kuwapokea wahubiri INJILI Kwa kiasi kikubwa.
KIVIPI TANZANIA IMEIBEBA DUNIA?
Kuibeba Dunia ni kufanyika LANGO. VIASHIRIA vyote nilivyoyaja pale juu, ni matokeo ya nchi hii kuwa center ya Amani na mazuri yote ambayo hupita na kubariki Dunia nzima.
1. KANISA LA MWISHO LITAKUSANYWA KUTOKEA TANZANIA.
Hapa katika Nchi hii, lile Kanisa la kwanza lililotawanyika Kutoka Israeli kwenda mataifa mbalimbali kuhubiri INJILI, litajikusanyia tena Kutokea hapa kwenda kuhubiri INJILI ya ufalme Kwa mataifa yote.
Kama ni mtu wa Roho, tayari harakati hizo zimeanza kuonekana.
Nitaendelea.........