Je, wajua kwamba Nyerere ni jina la utani?

presider

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2013
Posts
1,320
Reaction score
1,738
Katika kufuatilia historia yangu, ukoo wangu na baadhi ya watu maarufu wanaonizunguka ndipo nikagundua kuwa, kumbe 'Nyerere' ni jina la utani!

Nyerere ambaye alikuwa ni chifu wa pili wa Butiama baada ya ndugu yake Bhuhoro, alitawala kwa miaka 30 tangu 1912 hadi 1942. Baba yake, mzee Burito hakuwahi kuwa chifu wa Butiama kama wengi wanavyokanganya.

Jina halisi la Nyerere ni 'MBONOSI', lakini alipokuwa mkubwa kwa umri wa ujana wake, mwenyewe alijiita Nyerere.

Jina hilo linatokana na mdudu anayeitwa 'Kiwavijeshi'. Kiwavijeshi ni mdudu mharibifu mkubwa wa mazao mabichi shambani.

Mdudu huyu akivamia shamba hula jamani na matunda yote na pengine hata visiki vyake. Kwa kizanaki hicho kiwavijeshi kinaitwa 'enyerere'.

Nilipofuatilia kujua sababu za mzee Mbonosi kujiita Nyerere nilipata majibu mawili tofauti. Moja ni kwamba, yeye mwenyewe alijigamba kama vijana wengi walivyo hata leo katika jamii zetu wanavyojigambia 'nick name' zao. Yeye alijigamba kwamba, "Ninye Nyerere etariibhwe" (kwa kizanaki), yaani, "Ndimi kiwavijeshi kisicholiwa". Hakika kiwavijeshi hakikuweza kuliwa katika jamii ya Kizanaki, labda kwingineko mtatwambia.

Jibu la pili la kwa nini Mbonosi alijiita Nyerere lilielezwa kwa mtazamo wa vituko vyake alivyovifanya wakati wa ujana wake. Vituko hivyo vilivyomfanya akimbie Butiama kwenda kuishi Ikizu sitavielezea leo ila viko kwenye makala zangu maalum zihusuzo 'Ukoo Wa Kizanaki" na "Historia ya Wazanaki.

Mbonosi hakujigamba kwa kujiita tu Nyerere, kuna wakati alijiita "Ikumbamahuuna". Jina hilo lilimaanisha 'mkunja maduku', yaani mjenzi wa mabanda ya kuishi kwa dharura. Majina yote hayo yanasemekana yaliambatana na matukio aliyokuwa akiyafanya Mbonosi.

Tabia hii ya kutukuza majina ya utani au ya majigambo siyo ya Mbonosi tu, hata watu wengi leo majina yao yaliyotukuka ni ya utani au ya majigambo. Mtu mwingine maarufu niliyebaini jina lake la majigambo ni 'BUGOZI'.

Huyu ni mzee wetu, mkuu wa majeshi mstaafu David Bugingo Musuguri. Mzee huyu naye jina lake halisi ni Waryoba, akaitwa pia Bugingo kisha akajigamba kwa jina la mpiga mieleka maarufu wa enzi zake aliyeitwa Bugozi. Hili la David ni la nyongeza kama wengi wanavyojichagulia majina wakati wa ubatizo.

TUNAPOADHIMISHA MIAKA 19 YA KIFO CHA BABA WATAIFA, MWL JULIUS KAMBARAGE NYERERE, NI VEMA TUKAKUMBUSHANA JINA LA 'MBONOSI' KATIKA HISTORIA YA TANZANIA AU YA NYERERE.
 
Ngumu sana watu kuamini, ni kama vile uwaambie wasafi inamilikiwa Na kusaga, hawakuelewi au mbowe ni CCM damu damu wakati kuna element za ukwel
 
Hata kwetu mambo hayo huwa yalikuwepo sana. Japo sasa usomi na imani za kidini umeyapunguza sana.

Mfano kwetu watu wengi nickname zao hutokana na wanyama wakali na wababe porini.eg. Tembo, Fisi, kifaru, Simba, chatu nk.
Na ni kwa mifano hiyo, kwetu Mwl Nyerere walimbatiza jina la sungura, walimuona kama mtu mjanja sana na hivyo kumfananisha na sungura awapo porini ni mdogo lakini huwezi kumnasa kirahisi
 
E bwn presdaa, shukrani kwa kunijuza. Hiki kipande nitaki add kwenye fail la kihistoria la mwalimu.
 
Katika kufuatilia historia yangu, ukoo wangu na baadhi ya watu maarufu wanaonizunguka ndipo nikagundua kuwa, kumbe 'Nyerere' ni jina la utani!

Nyerere ambaye alikuwa ni chifu wa pili wa Butiama baada ya ndugu yake Bhuhoro, alitawala kwa miaka 30 tangu 1912 hadi 1942. Baba yake, mzee Burito hakuwahi kuwa chifu wa Butiama kama wengi wanavyokanganya.

Jina halisi la Nyerere ni 'MBONOSI', lakini alipokuwa mkubwa kwa umri wa ujana wake, mwenyewe alijiita Nyerere.

Jina hilo linatokana na mdudu anayeitwa 'Kiwavijeshi'. Kiwavijeshi ni mdudu mharibifu mkubwa wa mazao mabichi shambani.

Mdudu huyu akivamia shamba hula jamani na matunda yote na pengine hata visiki vyake. Kwa kizanaki hicho kiwavijeshi kinaitwa 'enyerere'.

Nilipofuatilia kujua sababu za mzee Mbonosi kujiita Nyerere nilipata majibu mawili tofauti. Moja ni kwamba, yeye mwenyewe alijigamba kama vijana wengi walivyo hata leo katika jamii zetu wanavyojigambia 'nick name' zao. Yeye alijigamba kwamba, "Ninye Nyerere etariibhwe" (kwa kizanaki), yaani, "Ndimi kiwavijeshi kisicholiwa". Hakika kiwavijeshi hakikuweza kuliwa katika jamii ya Kizanaki, labda kwingineko mtatwambia.

Jibu la pili la kwa nini Mbonosi alijiita Nyerere lilielezwa kwa mtazamo wa vituko vyake alivyovifanya wakati wa ujana wake. Vituko hivyo vilivyomfanya akimbie Butiama kwenda kuishi Ikizu sitavielezea leo ila viko kwenye makala zangu maalum zihusuzo 'Ukoo Wa Kizanaki" na "Historia ya Wazanaki.

Mbonosi hakujigamba kwa kujiita tu Nyerere, kuna wakati alijiita "Ikumbamahuuna". Jina hilo lilimaanisha 'mkunja maduku', yaani mjenzi wa mabanda ya kuishi kwa dharura. Majina yote hayo yanasemekana yaliambatana na matukio aliyokuwa akiyafanya Mbonosi.

Tabia hii ya kutukuza majina ya utani au ya majigambo siyo ya Mbonosi tu, hata watu wengi leo majina yao yaliyotukuka ni ya utani au ya majigambo. Mtu mwingine maarufu niliyebaini jina lake la majigambo ni 'BUGOZI'.

Huyu ni mzee wetu, mkuu wa majeshi mstaafu David Bugingo Musuguri. Mzee huyu naye jina lake halisi ni Waryoba, akaitwa pia Bugingo kisha akajigamba kwa jina la mpiga mieleka maarufu wa enzi zake aliyeitwa Bugozi. Hili la David ni la nyongeza kama wengi wanavyojichagulia majina wakati wa ubatizo.

TUNAPOADHIMISHA MIAKA 19 YA KIFO CHA BABA WATAIFA, MWL JULIUS KAMBARAGE NYERERE, NI VEMA TUKAKUMBUSHANA JINA LA 'MBONOSI' KATIKA HISTORIA YA TANZANIA AU YA NYERERE.
Kwa hiyo historia ya Nyerere na Historia ya Tanzania in sawa?
 
Back
Top Bottom