*BREAKING NEWS*
AIR TANZANIA na ETHIOPIAN AIRLINES wanatarajia kufanya mafunzo ya muda mfupi na ya bei nafuu kwa wachezaji na viongozi wa timu ya SIMBA ili kuwaelekeza namna ya kuingia kwenye ndege, kukaa kwenye viti na sehemu ya kuweka handluggage. Pia watafundishwa namna ya kuacha tabia zao za kung'oa koki, kung'oa viti kama walivyofanya uwanja wa Taifa.
Aidha mafunzo hayo yatawaelimisha kuwa wasije na vyakula vya safari kwenye ndege mfano kande, wali, ndizi, ugali nk. Idara ya Uhamiaji nayo itawapatia mafunzo ya siku moja namna ya kujaza fomu za kupata passport. Idara hiyo imewaomba wachezaji hao na viongozi wao kuomba msaada kwa wenzao Yanga a.k.a Wakimataifa ambao wana uzoefu wa kupanda ndege kwa zaidi ya miaka 5 na kupanda ndege kwao imekuwa kama kwenda Manzese.
Maswali yatakaribishwa na kujibiwa na inategemewa swali litakalotia fora kwa kuulizwa na wengi ni *"wapi sehemu ya kuchimba dawa"*.[emoji3][emoji3]