Uchaguzi 2020 Je, wajua Mgombea atakayetangazwa kuwa Rais hawezi kuwekewa pingamizi Mahakamani?

Uchaguzi 2020 Je, wajua Mgombea atakayetangazwa kuwa Rais hawezi kuwekewa pingamizi Mahakamani?

Status
Not open for further replies.

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Joined
Aug 7, 2018
Posts
685
Reaction score
1,124
Habari wanaJF,

Wakati tukielekea tarehe 28 Oktoba 2020 ambayo itakuwa siku ya kupiga kura kuchagua Rais, Wabunge na Madiwani.

Ni vyema ukafahamu yafuatayo:

Ibara ya 41(7) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaondoa mamlaka ya Mahakama yoyote kuchunguza juu ya kuchaguliwa kwa Mgombea.

Kutokana na ibara hii, iwapo mgombea wa kiti cha Urais atatangazwa na Tume kuwa amechaguliwa kuwa Rais basi hakuna Mahakama yoyote itakayokuwa na mamlaka ya kuchunguza kuchaguliwa kwake.
 
Upvote 1
Koo mnatuaminisha kuwa mahakama zetu na sheria zipo chini ya raisi, Tanzanian mpya.
 
Watanzania Leo Kuna jamaa yangu kaniambia yupo kwenye usimamizi wa uchaguzi

Sasa semina Yao ya siku mbili iliyoanza leo wamepewa 80000/=

Chakushanga maneno waliyoambiwa kwamba presha huku nje ipo kubwa sana

Kwanza walitolewa wote ambao walifatiliwa habari zao zikaonekana zinavinasaba vya upinzani.

Jaman tuweni makini uchaguzi huu ni hatari sana

Haki huinua TAIFA
 
Iyo sio katiba ya nchi yetu,,,,iyo ni katiba ya ccpinduzi.... naomba pia i katiba iwe ni somo kabisa mashuleni mda mwingine naisigi ni watu wachache mno wanaijua

Mimi myself sijui ata imeandikwa kwa wino wa rangi gani!!

Histor itolewe iwekwe katiba.

Nashangaaga mno et kwenye civics wameweka human rights ni sawa sikatai but huu mda watuwekee na katiba

Tumechoka lea mimba zao za chuki
 
Habari wanaJF,

Wakati tukielekea tarehe 28 Oktoba 2020 ambayo itakuwa siku ya kupiga kura kuchagua Rais, Wabunge na Madiwani.

Ni vyema ukafahamu yafuatayo:

Ibara ya 41(7) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaondoa mamlaka ya Mahakama yoyote kuchunguza juu ya kuchaguliwa kwa Mgombea.

Kutokana na ibara hii, iwapo mgombea wa kiti cha Urais atatangazwa na Tume kuwa amechaguliwa kuwa Rais basi hakuna Mahakama yoyote itakayokuwa na mamlaka ya kuchunguza kuchaguliwa kwake.
Kukiwa na uchakachuaji wa kura wiki hii, Mahakama itakuwa Nguvu ya umma
 
NEC wakishamtangaza mshindi, vyombo vyote vya ulinzi na usalama vinaingia kazini kumlinda huyo mtu. By then haijalishi kama NEC walikosea au la.

Pamoja na kudai Tume huru ya Uchaguzi, hiki kipengele cha Katiba kinapaswa kufanyiwa marekebisho moving forward. Otherwise ni ngumu sana hawa watu kumgawia mtu Urais kwenye sahani.

“Tunatumia Dola kubaki Madarakani”- Bashiru, Katibu Mkuu wa CCM.
 
Huu ndio udhaifu uliopo katika katiba ambao CCM haitaki uguswe!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom