JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 685
- 1,124
Sabuni hufanya kazi kwa kuharibu Molekyuli za kirusi cha Corona hasa Molekyuli za mafuta zinazounda ngao ya nje inayozunguka kirusi
Ngao ya nje ya kirusi ina mafuta ambayo hukisaidia kirusi kiweze kuishi kwenye mazingira kwa muda na kiweze kunata kwenye nyuso za vitu
Unapoosha na mikono kwa maji pekee kirusi kitaendelea kunata bila kutoka kwa sababu ngao inafanya kirusi kuwa kama tone la mafuta
Molekyuli za sabuni zinapofika kwenye kirusi huivunja ngao ya nje ambayo imeundwa na mafuta na kirusi hubomoka na kutokuwa na uwezo wa kuishi tena
Pia ni muhimu kufahamu kwamba unaponawa kwa sabuni na maji tiririka kwa muda wa sekunde 20 na kuendelea unatoa nafasi Molekyuli za sabuni kufanya kazi ya kuondoa virusi na chembechembe za uchafu kutoka kwenye sehemu zote za
mikono
#JFCovid19_Updates #Corona #CoronaVirus