JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 685
- 1,124
Tukianza na EPIDEMIC hii ni hali ya ugonjwa ambao huathiri idadi kubwa ya watu ndani ya jamii flani, nchi au eneo. Mfano: Kipindupindu, Chikungunya na Ebola
PANDEMIC ni pale ugonjwa unapotoka kwenye hali ya Epidemic na kuenea kwenye Mataifa mengi au mabara mengi. Mfano: #COVID19
ENDEMIC ni pale ugonjwa huwatokea watu wa jamii flani ndani ya nchi au eneo flani kwa kipindi kirefu. Watu huanza kuishi na huo ugonjwa katika jamii. Mfano: Malaria
OUTBREAK huu ni ugonjwa wa mlipuko ambao huwakumba watu wengi zaidi katika eneo fulani bila ya kutarajia. Kama hatua za kudhibiti hazitachukuliwa mapema basi ugonjwa upelekea 'Epidemic'. Mfano: Ebola
Upvote
5