Je wajua, zamani Wanawake ndio walikuwa wanatongoza mabishoo?

Je wajua, zamani Wanawake ndio walikuwa wanatongoza mabishoo?

bahati93

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2015
Posts
1,334
Reaction score
2,463
Kweli mambo yanaenda kasi sana wanabodi.
Sijui Manyangema hapo kale ya 2000s walikuwa wanakwama wapi, kwani nimekuja kugundua walikuwa hawatongozi kabisa, wao ndio walikuwa wanapigwa mistari sana na manzi wa enzi hizo.

Hawa Wanawake wanaotongozaa sijui wameishia wapi, yaan tokea nitongozwe primary school sijawahi tongozwa tena, ona sasa madhara yake nazeeka na utamu wangu. Wafwatao ni list ya wanaume waliotongozwa:-

1. Daz baba katika ngoma Naitaji wife. Daz anachekesha alitongozwa kwa barua jibu lake akasema Moyo wangu chukua.

2. Prof jay Huyu jamaa sijui ilikuwa ni fantasy au kweli, kuhusu yeye kupendwa na kutongozwa kibabe na Viki katika ngoma la Zari la mentali. Mwimbaji kiitikio Juma nature nae alitongozwa.

3. Juma Nature kwenye Inaniuma sana huyu alitongozwa na mwanafunzi wa chuo cha habari tena alifwatwa usiku, Juma alikuwa anajikanyaga wakati anapigwa mistari na Tina hadi kusingizia Dingi yake hataki atoke nnje usiku. Inahuzunisha sana

4. Mchizi Mox kwenye ngoma ya mikasi. Yaani Mox na sauti yakee ya mikwaruzo bado alikula mistari kutoka kwa Bahati.

5. Mwana FA huyu bitoz wa zamani yeye kwenye ngoma ya Unanitega analalamika kwanini manzi hamtongozi. Inashangaza sana! hawa mabrother walikuwa wanazingua sana sijui walikuwa wanataka kutufundisha nini.

6. Noorah jamaa kazinguaa sana kwenye ngomaa ya Ukurassa wa pili. Yaan jamaa literali analamika kutongozwa humo ndani anaringaaa vibayaa saana, mademu wengi sana kawapiga cha mbavu ..pumbavu sana huyu nyangema.

Wanabodii wapoo wengii sanaa waliokuwa wanatongozwa nikiwaandika wotee hapa hapatatosha hapa. Ndo maana Lady Jadee aliwachana wanaume kama mabinti. Nawaangaliagaa tuu hawaa mabraza
 
Mimi sijui nitakuwa tofauti ama vipi! Mimi kwangu umalidadi wa mwanamke ni "akili kichwani ziwemo". Hata kama mwonekano wa umbo na sura ni mrembo lakini kama ni wale wa "D mbili" ambaye hatuwezi tukakaa pamoja na kuongelea mambo yenye uhalisia katika nyanja za kiuchumi, kisiasa, kitamaduni, kisayansi, na zaidi awe hana swagger! Hiyo mbususu sihitaki kabisa!
 
Zamani ukiwa na ghetto tu na ghetto Hilo likawa na meza ya vioo, tv chogo inchi 18 , kabati ya mchina basi tambua umemaliza

Utawala mno wanawake

Saiz inabidi uwe na Subaru au crown aisee utawala mno wanawake

Lakini zamani ukiwa tu na baiskel ya gia umemaliza kazi
 
Zamani ukiwa na ghetto tu na ghetto Hilo likawa na meza ya vioo, tv chogo inchi 18 , kabati ya mchina basi tambua umemaliza

Utawala mno wanawake

Saiz inabidi uwe na Subaru au crown aisee utawala mno wanawake

Lakini zamani ukiwa tu na baiskel ya gia umemaliza kazi
Yani ukionekana una hizi gari, kata kama mstaraabu utaonekana mshenzi
 
Wasanii wanapendwa na wanawake sana na kama hautafunga zipu utaishia kupata ungonjwa wa "moyo au kifua".
 
Back
Top Bottom