balimar
JF-Expert Member
- Sep 18, 2015
- 7,743
- 13,657
Wadau habari,
Napenda ifikie wakati tufungua mjadala mpana wa uwepo au kutakuwepo kwa Bodi ya Kitaalamu ya Walimu Tanzania (Tanzania Teachers' Professional Board) TTPB.
Tumekuwa na sintofahamu kadhaa hasa kwa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) kuona TTPB itaongeza utitiri wa vyombo vinavyomsimamia mwalimu achilia mbali tozo za ada ya kila mwaka ambayo italipwa moja kwa moja na mwalimu na ada za leseni na kuona kama Teachers' Service Commission (TSC) inatosha kabisa kufanya na kuendelea na majukumu hayo.
Ni ukweli usiopingika kuwa KUTOKUWA na bodi maalumu ya kusimamia Professional ya Ualimu imekuwa ni sababu ya kutoheshimika kwa taaluma hii ukilinganisha na taaluma zingine kama za udaktari, uhasibu, sheria n.k. Ukiangalia kwa umakini nchi zinazoheshimu taaluma ya ualimu wanazo bodi za Kitaalumu za Walimu ambazo kazi yake kubwa ni kuweka Viwango na kusimamia na Kuishauri Serikali au mwajiri yeyote wa taaluma hii kuhusu taaluma na weredi husika.
Huu ushauri wa kitaalamu unaoletwa na bodi ndio unamsaidia muajiri kujua nini afanye na nini asifanye kwa mwajiliwa mwenye taaluma husika.
Mapungufu makubwa kwenye taaluma ya Ualimu kwa sasa ni kukosekana kwa viwango (standards) za taaluma hasa kwenye mishahara, uzoefu na elimu za walimu. Tofauti ni kubwa sana. Walimu tunatofautina hata mkiajiriwa na kwa level ya DEGREE tu, ukija shuleni mshahara ni tofauti na ukienda vyuo vya kati na tofauti ni kubwa zaidi ukienda kama tutorial assistant kwenye Elimu ya Juu. Lakini kibaya zaidi ukijiendeleza ndio kama umejichongea utasikia wewe ni kama umejifurahisha tu yaani Masters degree ya Ualimu na ukipata PhD unaambiwa wewe ni Over-qualified.
Nadhani sasa ni wakati wa kuangalia kama serikali inania ya kuleta bodi basi wadau wa Elimu hasa CWT na TSC walimu na wadau wengine wakae chini kwa muono mpana kuona faida ya sasa na vizazi vijavyo kwenye taaluma ya Ualimu na tunazohisi kuwa ni changamoto basi tuzijadili na kuzitatua kwa katika hatua za mwanzoni kabisa za uanzishwaji wa Bodi hii ya Kitaalamu ya Walimu.
Hata hivyo Bodi itasaidia sana maana kutakuwa na standard ambazo ndicho kilio chetu kikubwa kwa sasa ambacho nimekosea majibu. Mathalani madarasa yamefurika wanafunzi, walimu ni wale wale, walimu wanafanya kazi zilizopitiliza, hakuna usawa hata wa madaraja tu ya mishahara kwenye HALMASHAURI walizoajiriliwa, richa ya kuwa na mshahara usioendana na mahitaji ya kawaida ya kiuchumi (njiwa), kukaa muda mrefu bila ya mwajiri kukupandisha daraja, stahiki, uhamisho, matibabu na mwisho ni madharau wanayopewa na Wakuu ambao baadhi yao hawana hata sifa za kuwa hapo waliopo ila kwakuwa ni watoto wa mjomba na Shangazi.
Naomba kuwasilisha mjadala huu mzuri