Ni kosa la kimaadili kwa wakili kuvujisha siri za mteja wake, na kama una ushahidi wa namna hiyo unaweza kumshtaki ndio katika kamati ya nidhamu ya wanasheria..kwa urahisi unaweza peleka malalamiko yako katika chama cha wanasheria Tanganyika huko utapewa namna ya kufanya..
Kama binadamu mwingine mwenye tamaa, wakili anaweza kukugeuka kwa kufanya kazi chini ya kiwango - pia unaweza kumshtaki kwa uzembe wake wa kitaaluma...ila njia nzuri ni kumkataa kama utagundua mapema kuwa hana nia ya dhati kufanya kazi yako