Je,Wakili ni Mwanasheria?

Je,Wakili ni Mwanasheria?

Mr Focus

Member
Joined
Jan 25, 2014
Posts
13
Reaction score
1
Je,wakili ni mwanasheria? nakama jibu ni ndiyo inakuwaje ana uwezo wa kumtetea mtenda dhambi ilhali anafahamu ukweli?
 
Je,wakili ni mwanasheria? nakama jibu ni ndiyo inakuwaje ana uwezo wa kumtetea mtenda dhambi ilhali anafahamu ukweli?

Sina uhakika kama kila kosa ni dhambi mathalani kuchelewa kazini ni kosa lakini sitaki kuamini ni dhambi. Pili kuhusu Wakili kutoa huduma ya utetezi kwa mtuhumiwa kabla hajatiwa hatiani ni sawa na Daktari anapo toa tiba kwa Mwizi ili asife
 
Wakili ni mtu aliyepewa kibali na Mahakama Kuu kukufanya kazi kama mtu binafsi ya kuwatetea watu ua kundi la watu. Mwanasheria ni mtu ambaye hana kibali cha kuwawakilisha watu, yaani hana kibali cha kufanya kazi independently!
 
Ata mim huwa naona mawakili ni wanafiki sana!

ama sivyo, sheria hapo imetengeneza UFA WA haki kupotea kwa mfumo WA uwakili!
 
Je,wakili ni mwanasheria? nakama jibu ni ndiyo inakuwaje ana uwezo wa kumtetea mtenda dhambi ilhali anafahamu ukweli?
subiri ukamatwe ukae rumande kama mwezi hivi halafu ndipo utajua umuhimu wa hawa wadudu.
 
Focus si kila mtenda kosa anachukuliwa ni mkosaji na hivyo kabla ya kuhukumiwa ni lazima apewe nafasi ya kujitetea na kuwakilishwa na mtetezi. Kumbuka hata Adam na Eva walipokosea pale bustanini Mungu aliwapa haki ya msingi ya kujieleza kabla hajawapa adhabu. Ss kujua mtu kakosea ama laa ni mpaka asikilizwe-presumption of innocence-every person is presumed to be innocent untill the contrary is proved. Ss kujua hawa wadudu wanao umuhim gani hebu jarib fanya kosa na afande Kova akusweke rumande yake pale central km wiki hivi thn ukakae na Keko wiki mbili utapata majibu yako yote. Ni mtizamo wangu tuuu

Sent from my BlackBerry 9360 using JamiiForums
 
mi waliniacha hoi walivyomtetea zomba kuwa hakuua na mahakama ikakubali kweli hakuuwa
~~NA walivyomtetea aliyemuua meya wa mwanza licha ya kuwa ushahidi ulikuwa wazi mchana kweupe,lakini nasikia mtuhumiwa aliuza gorofa akawa anagawa rushwa hadi akaachia huru
 
Back
Top Bottom