Doctor Ngariba
JF-Expert Member
- Jan 28, 2020
- 588
- 951
Nawasalimia wapendwa kwa salamu ya kikombati.
Moja kwa moja kwenye mada kama ilivyo kwenye kichwa cha habari
Juzi nilipita Mbagala na usafiri wangu wa asili (sina gari,boda wala baiskeli) nilichokiona kilinifanya nifikiri labda gen z ya Tanganyika ina jambo lake kupitia wamachinga.Jamaa wamepanga bidhaa zao kuanzia njia ya watembea kwa miguu hadi robo ya barabara ya magari.
Najiuliza maswali haya:-
1. Wamachnga wameshindikana au serikali imeamua kuwahurumia wananchi wake ili wajipatie riziki zao halali?
2. Hawa viranja wa maeneo yale hawajui kuwa miongoni mwa sababu za foleni kuanzia Zakhem hadi Kanisani ni hao wamachinga waliojinyakulia hiyo road?
3. Vipi kuhusu usalama wa watembea kwa miguu ambao wanalazimika mara nyingine kutembea barabarani ili kupisha biashara za wamachinga?
4. Je, wamachinga wenyewe wamejishukuru kwamba wanaona poa tu kupanga biashara zao barabarani?
Maswali ni mengi lakini nadhani niishie hapa maana nisije onekana nina roho mbaya kwa wapiga kura.
Picha wakuu sijapata nilihofia kunajisi biashara za watu au kumbulia kipigo bure.
UHURU BILA MIPAKA NI UTUMWA.