Ndg zangu.siku za hivi karibuni watanzania tumeshuhudia mwenendo mbaya wa bunge letu kiasi cha baadhi ya watu kutumia maneno ya kashfa na matusi wanapo Adress bunge. mfano ni michango ya watu wanaopiga simu kwenye vipindi vya redio wengi wameonesha kuchoshwa na mwenendo huu wa bunge letu. kama nitakumbuka vizuri sehemu ya kwanza ya katiba yetu inazungumzia wananchi kuwa ndio waamuzi wa mwisho kuhusu mustakabali wa nchi hii( dola) kwa neno la kisheria PEOPLES SOVERGNITY sasa naomba kujua kama ambavyo sheria inaruhusu mtu kuishitaki serikali anapoona haki yake imevunjwa pia wananchi wanaweza kukata rufaa kupinga hukumu ya mahakama fulani sasa je mwanachi/wananchi tunaweza kulishitaki bunge ? ili tuzuie matumizi mabaya ya rasilimali za nchi ambayo yanapotezwa na wabunge wetu wanapotumia bunge kujionyesha mavazi yao na kufanya kazi ambazo hatujawatuma naomba legal opinions.