Je, wanasiasa na wasomi wote wa Tanzania wakizeeka wanakuwa na ubunifu wa kufanana?

Very true wengi wao huwa wanashinda ofisini wakistaafu ndio wanakunbuka kumbe ofisi siyo mali yao ndio wanasnza kuangalia njia mbadala
 
Wazee wamekomaa Vijana wawe wabunifu haya kijana katokea kabuni Gobole la kuulia Tembo Wazee hao hao wanaosema Vijana wawe wabunifu wanamdaka kijana wanamtia ndani yeye na ubunifu wake sasa Wazee hatuwaelewi nyinyi mnataka Vijana wawe wabunifu au mnataka Vijana wafanyaje?

Tuache hio Wazee wanasema Vijana muwe wabunifu kuna Jamaa humu alileta Mada akafungua uzi kuhusu suala la internet yeye alikuja na wazo akalipeleka TCRA kuelezea kuhusu ubunifu wake alichoambiwa ni kulipia mamillion ya shillings ndio ubunifu wake ufike mbali na aweze kutambulika, halafu hapo hapo kuna lizee kesho linaamka kutoka kwenye LC 300 iliyochangiwa na Vijana linaanza kuropoka Vijana kuweni wabunifu Vijana kuweni wabunifu, yeye huyo Mzee ukimuuliza Wewe mpaka uzee wako huo ulionao tuonyeshe hata kimoja tu ulichobuni Wewe km Wewe kilichoinufaisha Dunia useme, hana sasa ananyanyukaje kuwaambia Vijana wawe wabunifu ikiwa yeye hana hata kimoja alichobuni mpaka uzee wake?
 
Inakuwa afya kama mzee amemobea kwenye banking system anapostaafu anakuwa amebuni kitu chake cha kibenk kinachomuendeshea maisha, hata akienda kijijini ni kula maisha sio kuyatafuta.

Hiki ndio namaanisha na ndio inakuwa na motisha kubwa sana kwa vijana.
 
Motivation speakers hao
 
Kwa bahati mbaya wanakuja kulima hali ya kuwa hawakuzibadili sera za kilimo pindi wakiwa vijana, jambo linalopelekea sera hizo kutokuwa wezeshi kwa umri wao.
 
Usifananishe hao matajiri wakubwa na waalimu wastafu. Fananisha na waalimu wa huko. Kawaida mtu akistaafu anatakiwa kutulia kula pensheni, kusafiri na kutalii. Kama anafanya kazi iwe ni hobby. Huku kwetu mtu akistaafu ndiyo anataka aanze kutimiza ndoto zake. Ndiyoa anaanza kufanya kazi masaa mengi na kwa nguvu kuliko alipokuwa kazini.
 
Mtu anayekaribia kufa, hana morari wa kubuni
 
Hatari
 
Ndio uwaambie Wazee sasa sio Wazee wamekaza ndevu zao za shaba kuparamia Vijana kwamba Vijana wawe wabunifu wakati wao na PhD yao ya mchongo hata hakuna walichobuni cha maana na kinachoonekana ukimuuliza Wewe Mzee unakomaa Vijana wabuni wabuni Wewe kwenye hii Dunia umebuni nini cha maana, hakuna alichobuni chochote
 
Motivation speakers hao
Wazee wamekomaa Sura Vijana kuweni wabunifu msisubiri ajira za Serikali ajira Portal PSRS Utumishi kuweni wabunifu Vijana kuweni wabunifu Vijana yaan Mzee kakomaa Sura kuweni wabunifu Vijana wakati yeye hajabuni hata njiti ya kiberiti isiyowashwa kwa kusugua na box la kiberiti Mzee hajabuni hata jiko linalotumia Maji badala ya Mafuta au mkaa au umeme au Gesi ila Mzee kakomaa Vijana kuweni wabunifu nyambafu
 
Wabantu asili yao ni wakulima au wafugaji.
Wanarudi kwenye asili yao. Jasili haachi asili.
Sisi waafrika ilitupasa kuwekeza sana kwenye elimu ya mazingira, maisha yetu yanategemea sana mazingira.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…