Je, wasanii wanaposhiriki kutoa burudani kwenye matamasha ya kiserikali huwa wanalipwa?

Je, wasanii wanaposhiriki kutoa burudani kwenye matamasha ya kiserikali huwa wanalipwa?

ESPRESSO COFFEE

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2014
Posts
6,170
Reaction score
7,665
Nianze kwa kukiri wazi kuwa, Tangu Nianze kufuatilia Matamasha ya Wasanii wanayo yafanya kwenye Jamii, Nimeona WASANII WA KITANZANIA wanaongoza Sana Kufanya PERFORMANCE zao Kwenye Matamasha/Mikutano Ya Kiserikali Kuliko Nchi Yoyote Ile Duniani.

Mbaya Zaidi na Zaidi, Nimeona WASANII WENGI WA KITANZANIA wakitumia Umati wa Watu walio hudhuria Kwenye Tamasha/ Mikutano Ya Kiserikali kuweka na kuonesha wakifurahia kile walicho kifanya Na KUJIAMINISHA kwa Watu Kuwa WANAPENDWA NA MASHABIKI ZAO. Lakini Ningependa Tujiulize Swali Moja, Wasanii Kwenda Kuperforme Kwenye Mikutano Ya Kiserikali, Kuna Jenga Sanaa Yetu Au Kunabomoa?

Nina Uhakika Asilimia 86% Wasanii Wote Wakitanzania Ambao wanashiriki kwenye mikutano ya Kiserikali Hufanya Hizi Performance BURE bila Malipo Yoyote yale, Bila Kupewa Nauli, Wala Gharama zingine zozote.

Ninaona Na Ninahisi Kabisa Wasanii, WANAONEWA, WANAIBIWA na WANADHURUMIWA haki Zao Na Viongozi Wa KISERIKALI na Hili ni Baya sana Kwa Ukuaji wa Mziki wetu na thamani ya wasanii wetu.

Msanii Ni Lazima na Ni vyema Akaweza Kuji BRAND na Kuwa na Misimamo yake, kam viongozi wa Serikali Watamuhitaji Msanii X basi Taratibu zifuatwe kama Vile promoter Anapohitaji Msanii.

Wasanii wamekuwa Wakitumika Na Viongozi wengi wa kiserikali kuwa Mabalozi wa vitu mbalimbali, Lakini Je Hawa Wasanii wanalipwa? Kama Viongozi wa Serikali Wanaongoza Katika unyonyaji wa Wasanii ni Nani Atakuja Kuwasaidia wasanii kupata Haki zao?

Ni wakati sasa Wa Wasanii wa Tanzania Kubadirika na Kuweza kuwa na Misimamo hadi kwa Serikali. Sanaa ni Kazi yenu kama Zilivyo kazi Zingine. Kiongozi wa serikali akienda kwenye mkutano anapewa au Analipwa Hela Ya Siku, iweje Msanii ukafanya show bure?

Wasanii ni wakati wenu wa kubadirika na kutambua Thamani zenu
 
Sidhani kama hawalipwi.... Wanalipwa na ushahidi ni Steve Nyerere alishadai kua kuna kipindi Polepole alibania fungu kwa baadhi ya wasanii waliokua wanamsapoti mama.
 
Yawezekana wanalipwa lakini kiasi cha kawaida kulingana na brand zao faida nyingine labda ni kama ile ya kondeboy alimpigia simu hayati direct ndo akapewa alichokuwa anataka Kutoka WCB
 
Sidhani kama hawalipwi.... Wanalipwa na ushahidi ni Steve Nyerere alishadai kua kuna kipindi Polepole alibania fungu kwa baadhi ya wasanii waliokua wanamsapoti mama.

Hivi ile Kampeni Ya Mama Ongea Na Mwanao walilipwa?
 
Back
Top Bottom