Je, wasio waislamu wanaweza kufunga mwezi wa Ramadhani?

Je, wasio waislamu wanaweza kufunga mwezi wa Ramadhani?

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Kwa uchache sana.

Naomba kuelimishwa kama mtu asiye muislamu anaruhusiwa kufunga Ramadani.

Kama ndio, naomba mwongozo wa taratibu za mfungo.

Mungu wa mbinguni awabariki!
 
Nivyema kushirikiana pamoja mana wote ni watoto wa ibrahimu..ila kimisingi hakunaga mfungo bali ni kubadili ratiba ya kula kutoka mchana kwenda usiku.

Ndio mana wanalia bei za chakula zisipande mana wanakula hao usiku kucha..sasa kuna mfungo hapo au kubadili ratiba tu ya msosi.

#MaendeleoHayanaChama
 
Kwa uchache sana.

Naomba kuelimishwa kama mtu asiye muislamu anaruhusiwa kufunga Ramadan.

Kama ndio, naomba mwongozo wa taratibu za mfungo.

Mungu wa mbinguni awabariki!
Wanaweza funga bila shaka muhimu watie nia na hiyo funga take.
 
Kwa uchache sana.

Naomba kuelimishwa kama mtu asiye muislamu anaruhusiwa kufunga Ramadan.

Kama ndio, naomba mwongozo wa taratibu za mfungo.

Mungu wa mbinguni awabariki!
Unaelewa maana ya kufunga?

Km unaelewa huwezi kuuliza hili swali!

Watu wengi wanabadiri mida ya kula ama kushinda njaa kwa sbb ya kufunga kwa mazoea na taratibu zilizowekwa na kanisa!

Kasome Isaya pale uone funga anayoitaka Mungu ikoje!



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unaelewa maana ya kufunga?
Km unaelewa huwezi kuuliza hili swali!

Watu wengi wanabadiri mida ya kula ama kushinda njaa kwa sbb ya kufunga kwa mazoea na taratibu zilizowekwa na kanisa!
Kasome Isaya pale uone funga anayoitaka Mungu ikoje!



Sent using Jamii Forums mobile app
Badala ya kujibu wewe unaniuliza maswali!!
 
Kwann unafunga? Kama unafunga ili kukamilisha ratiba ni bora uache tu maana kufunga ni zaidi ya kuacha kula na kunywa.

Jibu: mnaruhusiwa kwan kufunga ni swala binafsi mbali na dhehebu ulilopo
 
Badala ya kujibu wewe unaniuliza maswali!!
Isaya 58:3-10..
3Husema, Mbona tumefunga, lakini huoni? Mbona tumejitaabisha nafsi zetu, lakini huangalii? Fahamuni, siku ya kufunga kwenu mnatafuta anasa zenu wenyewe, na kuwalemea wote watendao kazi kwenu.

4Tazama, ninyi mwafunga mpate kushindana na kugombana, na kupiga kwa ngumi ya uovu. Hamfungi siku hii ya leo hata kuisikizisha sauti yenu juu.

5Je! Kufunga namna hii ni saumu niliyoichagua mimi? Je! Ni siku ya mtu kujitaabisha nafsi yake? Ni kuinama kichwa kama unyasi, na kutanda nguo za magunia na majivu chini yake? Je! Utasema ni siku ya kufunga, na ya kukubaliwa na BWANA?

6Je! Saumu niliyoichagua, siyo ya namna hii? Kufungua vifungo vya uovu, kuzilegeza kamba za nira, kuwaacha huru walioonewa, na kwamba mvunje kila nira?

7Je! Siyo kuwagawia wenye njaa chakula chako, na kuwaleta maskini waliotupwa nje nyumbani kwako? Umwonapo mtu aliye uchi, umvike nguo; wala usijifiche na mtu mwenye damu moja nawe?

8Ndipo nuru yako itakapopambazuka kama asubuhi, na afya yako itatokea mara; na haki yako itakutangulia; utukufu wa BWANA utakufuata nyuma ukulinde.

9Ndipo utaita, na BWANA ataitika; utalia, naye atasema, Mimi hapa. Kama ukiiondoa nira; isiwepo kati yako, wala kunyosha kidole, wala kunena maovu; 10na kama ukimkunjulia mtu mwenye njaa nafsi yako, na kuishibisha nafsi iliyoteswa; ndipo nuru yako itakapopambazuka gizani; na kiwi chako kitakuwa kama adhuhuri.
 
Unaelewa maana ya kufunga?
Km unaelewa huwezi kuuliza hili swali!

Watu wengi wanabadiri mida ya kula ama kushinda njaa kwa sbb ya kufunga kwa mazoea na taratibu zilizowekwa na kanisa!
Kasome Isaya pale uone funga anayoitaka Mungu ikoje!



Sent using Jamii Forums mobile app
Ni nini maana ya kufunga!? Tujuzane

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Unaweza kufunga boss kwani kuwaunga mkono ndugu zako waislam na kufuata tamaduni zao ni uungwana usiomithirika

Kama alivyotuamrisha mwenyez Mungu wa haki katika Qur'an sura ya 2 aya ya 183
JPEG_20220325_102219_5430807946406488656.jpg
 
Hawafungi Bali wao hawali mchana kutokana na mzingira mfano unaishi nyumba ya kupanga kwa waislam Sasa unaanzaje kupika na kula?

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
Zanzibar hawana utaratibu wa kupangisha vyumba kama huku.

Wanafunga from childhood age, na wanahesabu siku walizofunga, watoto wakitaja wamefunga ngapi na wao wanataja idadi ya siku walizofunga. Mm nazungumzia experience nilioishuhudia.
 
Back
Top Bottom