#COVID19 Je, watafiti wa chanjo ya UVIKO-19 wamefuata taratibu na masharti ya kisayansi

#COVID19 Je, watafiti wa chanjo ya UVIKO-19 wamefuata taratibu na masharti ya kisayansi

Nyumisi

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2010
Posts
13,499
Reaction score
19,292
Baada ya kiini macho cha chanjo kupatikana ndani ya mwaka mmoja bila kuwepo kwa takwimu zisizotia shaka za majaribio kwenye wanyama kama panya na baadaye binadamu ambao lazima wapewe taarifa sahihi kuhusu chanjo inayofanyiwa utafiti na watoe ridhaa yao wenyewe (informed consent) na kulipwa fidia mbalimbali kwa kushiriki tu kwenye utafiti. Kila hatua lazima watoe matokeo kwenye majukwaa ya kitaaluma na kwenye mashirika ya afya ya kitaifa na kimataifa.

Mwishoni baada ya kukamilisha hatua zote za kitafiti chanjo hupata kibali kutoka WHO na mashirika ya nchi mbalimbali, mfano Marekani cha kuzalishwa ili itumike kwa watu wote waliokusudiwa.

Ninachoona hapa chanjo ghafla imefikia hatua ya majaribio kwa binadamu ndani ya mwaka mmoja pekee, halafu watu wanaombwa watoe ridhaa yao ili wachanjwe bila maelezo sahihi kuhusu hizo chanjo (uninformed consent) na bila fidia yoyote.

Na badala ya watafiti wenyewe kuhusika na huu utafiti, kinachoonekana ni serikali za mataifa mbalimbali kuhusishwa kuhamasisha watu washiriki kwenye majaribio haya.

Je, watafiti wa chanjo wamefuata maadili ya kitafiti (Research ethics involving humans) na kukamilisha taratibu na masharti yote ya kupata kibali (final approval) kutoka kwenye mashirika ya afya ya kitaifa na kimataifa? Karibuni kwa maoni...​
 
Ndugu yangu hata gazeti la tamthilia huwa na mpangilio,
 
Gaidi Mbowe yupo chini ya ulinzi salama wa Polisi, nchi nzima imetulia hakuna matukio ya ajabu ajabu kama Uamsho walivyowekwa sehemu salama na Zenji ikatulia.
 
Ndugu yangu hata gazeti la tamthilia huwa na mpangilio,
Mkuu facts zote zipo hapo, mimi siyo mtaalamu wa lugha namna ya kupangilia sentensi.....wajuvi tayari wanajua nini nilichoandika hapo, bila shaka watakuja na maoni yao.
 
Gaidi Mbowe yupo chini ya ulinzi salama wa Polisi, nchi nzima imetulia hakuna matukio ya ajabu ajabu kama Uamsho walivyowekwa sehemu salama na Zenji ikatulia.
Nafikiri hii imekosea njia...
 
Inashangaza...VAERS(VACCINE ADVERSE EVENTS REPORTING SYSTEM) ya Marekani inaripoti vifo 12,000+ kutokana na chanjo lakini bado wanazipigia debe...Huko nyuma nchi hiyo hiyo walishawahi kuacha kutumia chanjo kisa vifo 25 tu...
 
Back
Top Bottom