makongorosi
Member
- Apr 24, 2009
- 49
- 4
Nikisoma hizi comments napata picha kuwa inaonekana kuna beef kubwa kati ya wabongo waliobahatika kutoka na kuendelea na shughuli zao ughaibuni V/S waliojaribu kuondoka na kugonga ukuta, walionyimwa visa, na wanaotamani kuondoka lakini inawawia vigumu, ama wanaoendelea kupigika bongo na waya mkali.
Ukiwa nje siku hizi huasaidii ndugu zako, unasaidia mafisadi. Ni bora uisaidie nchi inayokupa hata kibarua cha kubeba boksi, hapa nyumbani wapi unaweza kwenda kubeba boksi? Serikali inawakatisha tamaa, kama ingekuwa na mpango mzuri watanzania pia wanaweza kufanya vizuri.
Watanzania wanatumia money on "envelop system" sababu kutuma kwa njia zinazofahamika kama Western union, Money Gram kwetu bongo bado tuko gizani. Ukisikia mshikaji anakwenda bongo basi unampatia dollar kadhaa akawape nduguzo kwenye bahasha. Envelop system huwezi ingiza kwenye hizo takwimu nina amini watanzania wanasaidia zaidi ya wakenya na waganda. Kuna jamaa fulani waliacha kufanya kazi kabisa wakitegemea mafuba toka kwa kaka yao aliyekuwa Greece.
Ni hoja nzuri lakini nakushauri ungeuliza balozi za Tanzania katika hizo nchi ambazo ndiko kuna wabongo wengi. Labda wataweza kukupatia data zenye usahihi.
Mfano;Cheki na ubalozi wa bongo palee DC, sababu tulipokuwa tunabadilisha passport mwaka 2006 walichukua personal info zetu wabongo wote tuishio US.Naamini watakupa picha halisi ni watanzania wangapi wanaishi nje ya nchi, asilimia ngapi tunapiga boksi na wangapi wanapiga white collar schedule.
Halafu you be the judge.Halafu kama bado unakerwa na hizo data then cheki na balozi za Kenya, uganda au hata Nigeria uliza idadi ya watu wao wanaoishi nje, na details zao nyingine halafu linganisha usahihi wa hizo takwimu.
Mzee si ungetoa kabisa hizo details kama unazo kuliko kutoa homework ambayo hamna mtu ataifanyia kazi.
hapa ni jungu kuuAma kweli hili ni jukwaa la siasa.
Hizi takwimu lazima zina walakin, haiwezekani Waganda warudisha nyumbani kwao $850 million halafu Tanzania iwe $17m tu. Yaani pesa wanazorudisha Waganda kwao ni mara 50 ya pesa ambazo Watanzania walio nje wanazileta Bongo.
Hahaahaa!
Kaka hizi takwimu nizaukweli kabisa mimi kaka yangu tangu aende marekani miaka ya 80, mpaka leo hajawahi kutuma hata dolla1.Hizi takwimu lazima zina walakin, haiwezekani Waganda warudisha nyumbani kwao $850 million halafu Tanzania iwe $17m tu. Yaani pesa wanazorudisha Waganda kwao ni mara 50 ya pesa ambazo Watanzania walio nje wanazileta Bongo.
Watanzania wanaoishi nje wanapeleka wapi pesa zao
WaKenya ambao waaishi huku Tanzania na kwingineko duniani, mwaka uliopita walirudisha nyumbani kwao zaidi ya dola za Marekani $640 million. Wauganda nao walirudisha kwao $850 million mwaka jana. Pesa hizi zinatumika kununua nyumba, kulipa ada za shule, matibabu, nk na zinachangia sana kwenye pato la kigeni la nchi hizi jirani zetu.
Huko Kenya, pesa zinazotumwa na raia walio nje ndiyo chanzo kikubwa cha nne cha mapato ya kigeni baada ya mauzo ya nje ya chai, mauwa na utalii.
Benki Kuu ya Tanzania wala haijishuhulishi na pesa zinazotumwa nje na Watanzania na wala haitoi takwimu zake. Kwa mujibu wa makadirio ya Benki ya Dunia, Watanzania wanaoishi nje (diaspora) wengi wenu mkiwa wachangaji wakubwa wa mada humu JF, mwaka jana walitarajiwa kurudisha nchini kwao $17 milion tu?!
Hii ina maana mbili. Watanzania walio nje ni wachache sana au ni wengi lakini siyo skilled workers wanaoweza kupata kipato kizuri kutokana na taaluma zao. Pengine wengi wenu mnafanya kazi za kibarua, hourly shifts kubeba maboksi and flipping burgers MacDonalds na KFC hivyo hamna pesa za kutuma kwenu nyumbani kwa ajili ya maendeleo na kusaidia ndugu zenu. Si mrudi basi Bongo?
Au maana nyingine ni kuwa pesa hizo zinatumwa kwa wingi lakini Benki Kuu haifanyi utaratibu wowote wa kuzirekodi. Au zinatumwa kienyeji kwa kufichwa kwenye barua na mizigo mingine. Ama Watanzania mnaendekeza anasa tu huko majuu wakati Wakenya na Waganda wanajenga nchi zao? Nawaza sipati jibu.
Unafahamu tafsiri ya hilo neno mabulungutu ya dollar? unaijuwa dollar wewe?Ni kweli wenzetu nje hawachagui kazi kama sisi kwani kupata kazi ya maana nje ni ndoto. Hii sio kwa Waganda na Wakenya tu bali hata Watanzania pia. Tuje kwenye hoja ya msingi mimi nadhani swala kubwa hapa ni utunzaji wa takwimu kwani kama kawaida sidhani kama BOT inatilia swala hili mkazo sana. Pia nakubaliana na hoja iliyotolewa na mmoja wa wachangiaji humu kuwa watanzania wanaaminiana sasa na hupenda kutumia zaidi njia za kutumana na kupeana mabulungutu ya dola hivyo ni vigumu fedha hizi kuingia kwenye record za BOT.