A
Anonymous
Guest
JE! KAMA WATANZANIA TUNAJUA HISTORIA ZA MACHIFU WETU VIZURI?
Historia ni nini kwa ufupi zaidi Historia ni mkusanyo wa maarifa kuhusu wakati uliopita na ujao, pia historia ni mfululizo wa habari za mambo ya kale yaliyotokea pamoja na sababu zake. Binadamu anaziandika ili kuelewa maisha yake, yaani ametokea wapi, amepata mafanikio gani na matatizo gani. Historia pia inatufundisha kuishi kumbukumbu za mambo ya zamani ambayo yanatuwezesha kuendelea vyema na kujua tulipotoka.
Nimekuwa nikiona watu wanawakejeli wazee wetu/ machifu wa zamani kwa kusaini mikataba mibovu, au maamuzi waliyafanya na wakoloni mfano hai ni wa chifu Mangungo je tunafahamu haswa historia yetu au tunaishi na historia ambayo kwa upande mkubwa imeandikwa na wakoloni, ambao kimsingi wameandika mambo ambayo wanafunzi wanayasoma na wakiamini kuwa kama wa Tanzania au Tanganyika au vyovyote ilivyotambuliwa miaka hio kwamba tulikuwa wajinga, wachafu na wasio na maendeleo, msanii mmoja wa Afrika kusini Mama Miriam Makeba alieleza alipofanya mahojiano na kusema naomba ninukuu kwa ufupi ‘The conqueror writes history, they came, they conquered and they write. You don't expect the people who came to invade us to tell the truth about us.’ (Kwa tafsiri fupi isiyo rasmi ni kwamba wakoloni walikuja na kututawala kwa hio usitegemee mtu aliekuja kukuvamia akaeleza ukweli kuhusu wewe) hapo kuna swali la kujiuliza je historia yetu tunayoisoma ina ukweli na uongo kiasi gani?Labda hii inaweza kuzua mjadala. Hapo awali nilizungumzia kuhusu chifu mangungo juu ya mikataba ya ulaghai kwa ufupi kabisa katika jamii yetu ya leo mtu akikuita mangungo au kinjikitile ngwale huo ni ugomvi maana kwa tafsiri isiyo rasmi inaonekana kama ni wajinga hivi je hii ni kweli? na hawa ni baadhi ya machifu wetu wa zamani ambao kiufupi wanadharauliwa.
Huu ni mwaka wa 2024 sasa wataalamu wetu wa historia wapo wapi au bado tunaishi na historia tulizoandikiwa na wazungu(wakoloni) nadhani ni muda sahihi uchunguzi wa kina kufanyika ili kulinda heshima ya wazee wetu kuulinda utamaduni wetu.
Nikikurudisha nyuma kidogo au ukisoma kwenye majarida mbalimbali juu ya chifu mkwawa ambaye kwa upande wangu alikuwa chifu mzalendo mwenye uchungu wa himaya yake ambaye alipinga vikali utawala wa wakoloni kama watoto wetu wadogo mashuleni wanajua kuwahusu mashujaa hawa?, lakini tunasoma historia kidogo sana kuhusu mashujaa wetu waliopigana na wakoloni tunabaki kuwadhihaki bila kujua ukweli husika. Nina mengi juu ya mashujaa hawa ambapo ningeprnda kuwasimulia au kuwajua lakini nabaki sina neno ngoja nimalizie kwa kusema au kuomba wataalamu wetu wa historia kufanya mapitio ya vitabu vyetu vya historia ili kuandika historia yetu wenyewe ambayo ifundishwe kwa shule za msingi na sekondari hasa kabisa kwenye shule za msingi. Tufahamu historia yetu ili tudumishe mila na desturi zetu tuwaenzi mashujaa wetu ambao waliumizwa na watawala wakikoloni kwa kupigania uhuru wao kwa kunyongwa/ kuuliwa tunapaswa kujua haya ili tuweze kusonga mbele na Nchi zilizowatesa wazee wetu kwa kuwaumiza ni kweli wanapswa kuomba radhi kwa maumivu haya
Mwisho.
Naandika orodha fupi ya machifu wa enzi hizo.
-Chifu Mangungo wa Msovero
-Chifu Mkwawa Shujaa aliyewaongoza Wahehe kupinga utawala wakoloni wakijerumani kikoloni, kutokana na historia iliyoandikwa kumuhusu Inaaminika kwamba alijitoa uhai mwenyewe mnamo 1898 wakati alipokuwa mafichoni.
-Mtemi kinjekitile Ngwale ambaye Alinyongwa na dola ya kijerumani, kwa historia Alikashfiwa kwa kuchangia kwa vifo vya watu wengi baada ya kuwadanganya kwamba maji yangewakinga dhidi ya risasi. Inakadiriwa kwamba kati ya watu 180,000 na 300,000 walifariki wakati wa vita vya Maji Maji kutokana na mapigano.
- Chifu Mwangupile wa Mbeya
- Chifu Mkotani wa Bukoba
- Chifu Songea Mbano wa Ruvuma
- Chifu Mazengo wa Dodoma
Hao ni baadhi tu Unaweza kutaja wengine wengi ambao wamesahaulika ambao kila mmoja ana historia nzito juu ya maisha walioishi kipindi cha ukoloni pia kuwatambua tu haitoshi bali kuwaheshimu na kutambua mchango wao katika Tanzania yetu ya sasa pia ni vema kama Taifa tukatambua na kuheshimisha viongozi wa kimila ambao hadi sasa wapo ila hawatambuliki.
Stories of Change #Historia #storieschange #storiesofchange2024 #maarifa #storieschange #jamiiforum #historiayetu #mashujaa #viongoziwakimila #machifu
Source The African royal families, BBC Swahili.

- Kitu kingine ambacho kinanishangaza na ni swala la kujiuliza Je ushawahi kujiuliza kuwa kama ni kweli wakati wa vita ya majimaji ile dawa iliyotengenezwa na kinjekitile ngwale ilikuwa ikifanya kazi kweli na unadhani wajerumani wangekubali kuandika hilo? Kwamba waafrika ambao hawajui kusoma na kuandika wana uvumbuzi wa kitaalamu nqmnq hio? Nafahamu kuwa watu wengi walikufa katika vita hio lakini ujawahi kujiuliza juu ya kufanikiwa kwa dawa ya kinjekitile? Kwa historia Vita ya Maji Maji ilikuwa na dhana ya upingaji mkali wa waafrika dhidi ya utawala wa kijerumani katika maeneo ya kusini mwa Tanganyika sasa Tanzania na kupitia mtemi wao waliamini ukisema maji basi silaha inageuka kuwa maji kweli. Unaweza ukapata Maswali mengi ukijaribu kufikiri nje ya boksi anyway swala langu kubwa ni kuhusu kujua historia yetu je tunaifamu vizuri au bado tunaamini binadamu wa kwanza alikuwa sokwe inachekesha na kuhuzunisha pia, kwamba tunasoma tu kwa sababu ndio vitu vilivyopo kuandika vya kwetu aaah mbonw tunasoma ya wenzetu na kuuita the great history of mankind vipi vya kwetu? mpaka lini tutasoma vutabu vyao ambavyo kuna uwezekano kuwa viliandikwa uongo.