Je, Watanzania tunanufaika na rasilimali yetu ya gesi ya Mtwara?

Je, Watanzania tunanufaika na rasilimali yetu ya gesi ya Mtwara?

MUSHEKY

JF-Expert Member
Joined
May 9, 2014
Posts
2,812
Reaction score
2,760
Wakuu shwari?

Nipo maeneo flani napiga zangu togwa hapa iliyochanganywa na mapumba yasiyochachwa, asikuambie kitu mtu.

Tuachane na hayo,

Wakati naendelea kupata najaribu kujiuliza

* Hivi ile gesi yetu ya mtwara tuliyoambiwa ni neema iliyotushukia watanzania imetufaidisha kitu gani so far?

* Halafu mbona ni kama haizungumziwi tena kwa lolote? Ukimya huu ni ishara kwamba imeisha na kama imeisha tumemuuzia nani na pesa yake tumefanyia nini?

* Wananchi wa mtwara walikua na upeo mkubwa waliposema "hatutaki gechi iende dachlam" walikua wana maana hawataki kuyasikia mema ya gesi kwenye video bali walitaka kuyaona na kuyagusa wao wenyewe kwanza kisha gesi iendelee na safari ya daslam

* Sina uelewa je gesi hii haiwezi kusindikwa na kutumika katika mitungi ya kupikia ikauzwa kwa bei ya chini sana 'yes bei ya chini sana si yetu!

Hii itatupunguzia watanzania kuepukana na matumizi ya mkaa na kuni ambayo kwa jiji la Dar es salaam pekee inakadiriwa kufikia matumizi ya gunia laki 5 za mkaa kwa siku moja "sawa na gunia milioni15" kwa mwezi.

Si vibaya mimi kama mtanzania kufahamu, kama kuna anayefahamu jinsi watanzania tunavyonufaika na rasilimali hii muhimu na adimu aliyotupa Mungu kwenye nchi yetu basi anijuze na mimi pengine ni ishu ya uelewa tu.
 
Mzee wa msoga alituuza wamakonde akakimbilia USA msala kamuachia mfipa
 
Ukisikiliza hizo taarifa zao utapasua kichwa bure.
Wewe pambana kivyovyote mambo yaende vizuri.
 
1. Ile Gesi haifai kwa kupikia hata uifanyeje. Kwasababu ni gesi_mlipuko.

2. Kufaidika; Tunafaidika. Sema wengi wetu hatuwezi kuona.

3. Kuhusu Taarifa; Hakuna ambaye yuko tayari kukisanua maana harufu itakayotoka hapo ni mtafutano.

4. Tafuta Uzi unasema Kampuni ya Shells na Gesi ya Mtwara.
 
Back
Top Bottom