Gani?Maajabu
Gani?
Jana nilikuwa nafuatilia habari za anti/pro natalist movement. Kitu kimoja kilichopigiwa mstari ni idadi ya watu ilivyofumuka miaka ya karibuni.Ukisoma maandiko ya kale hata kupitia Vitabu vyetu vya kiimani ni kama utaona Dunia ya kitambo hicho ilikuwa nyuma sana ki teknolojia.Hawakuwa na mashine za kuwarahisishia kazi.
Na ukifuatilia gunduzi nyingi zilizopo leo zinaanzia hapo miaka ya 1700 hivi,na kadri tunavyoenda na ndivyo gunduzi haswa za kisayansi nazo zinaenda mbio kwelikweli.
Leo tunazungumzia mambo kama AI n.k. Muda si mrefu yatakuja mengine tena ya kustaajabisha na kushangaza.
Sasa ni vipi kwa Walioishi miaka ya nyuma ya hapo?Ni teknolojia ipi ya kustaajabisha tuliyoipokea kutoka kwao?.Nini hatima ya hii spidi ya teknolojia maana kila siku kuna jipya, na kasi ni kubwa sana.
Na hapa tusichanganye teknolojia na miujiza.Watu wa kale wengi wanajivunia miujiza zaidi.
Sasa kama walijenga na haikuwezekana kuacha taarifa ni vipi walijenga ndio haswa msingi wa hoja yangu.Ni kwa nini wameshindwa kurithisha taarifa?mbona teknolojia nyingine za kale zinapatikana vitabuni?.Watu wakale walijenga mapiramidi kule Misri.
Na mpaka leo bado inashangaza ni namna gani waliweza kubeba yale matofali makubwa nakuyapangilia vile.
Miaka mia si kesho tu,vipi miaka 1000 kutoka sasa?Hata kwa hiyo miaka 100 tu iliyopita taarifa zake mbona zinapatikana na kinachofanyika sasa ni kuendeleza tu,kwa mfano Tv,Camera,Simu,Redio n.k,ila huko 1700 kurudi nyuma taarifa za gunduzi za kiteknolojia ni hafifu sana.Watazungumzia zana za kale za mawe n.k.Watakaokuja miaka 100 tu ijayo watatuona sisi kuwa tulikuwa vilaza maana wakati huo kila kitu kitakuwa automated, watakuwa na koloni la kudumu Mars, AI sijui itakuwa imefikia hatua gani na si ajabu teknolojia ya propulsion itakuwa imewezesha kuunda vyombo vya usafiri vya kasi zaidi...
Ni dunia ya kuachiana hii
Maarifa kwa sasa yanaongezeka eksiponenshale. Huko nyuma tulikuwa tunajikongoja. Hii AI na maendeleo katika immunology, microbiology, quantum computing, DNA splicing na fission propulsion yanakwenda kubadili kila kitu - ndani ya miaka 50 - 100 tu ijayo!Miaka mia si kesho tu,vipi miaka 1000 kutoka sasa?Hata kwa hiyo miaka 100 tu iliyopita taarifa zake mbona zinapatikana na kinachofanyika sasa ni kuendeleza tu,kwa mfano Tv,Camera,Simu,Redio n.k,ila huko 1700 kurudi nyuma taarifa za gunduzi za kiteknolojia ni hafifu sana.Watazungumzia zana za kale za mawe n.k.
Hakuna balance kabisa kiteknolojia kuanzia miaka ya 1800 mpaka leo na ile ya nyuma yake kuanzia Damu na Hawa.Ingaws kuna hoja ya kimaandiko kama alivyo mention mdau coscated hapo juu