sky soldier
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 5,407
- 19,264
ila watu wa mijini na kwenye majiji kuna haja ya kujitafakari.
Mwana DSM ukienda mikoani huko au vijijini ukifika ni kawaida sana kukuta ndugu zako walikuwa wanakusubiri stendi zaidi ya saa ufike, umefika utachinjiwa kuku siku ya kwanza, utaishi hata mwezi na hakuna mtu atakupa maswali ya unaondoka lini, misosi utakula utasaza, ukiondoka utapewa hata debe la unga au maharage na hapo ukunbuke wewe ulipeleka tu mkate, unavyoondoka unasindikizwa kabisa wengine wanakubebea begi, kiufupi watu wa huko wengi ni wakarimu.
Ishu inakuja kwa watu wa Dar sasa, yani hata ndugu kaja kumpokea tu ni mtihani, mwenyeji anatoa maelekezo mgeni ampe simu bodaboda na malipo atalipa mgeni ambae hata hio hela haikuwa kwenye bajeti, akifika msosi ulioandaliwa ni ugali tembele yani ugeni wake ni kama hauthaminiki kama sio kumkomoa, baada ya salamu mwenyeji atakua bize na simu au mke wake kitu kinachoanza kukaribisha upweke kwa mgeni, mgeni akikaa siku 2 tu anaanza kuulizwa anaondoka lini, siku ya kuondoka pekee labda ndio mgeni husindikizwa maana ndio anasepa ni kama mzigo umetoka.
Sasa nauliza hivi watu wa huko mikoani nao wakiamua kwenda kwa style hizo kama zenu, je patatosha?